measkron
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 3,782
- 2,406
Madaktari na Madaktari Bingwa wanaomaliza mafunzo yao katika chuo cha sayansi ya tiba Muhimbili hawapatiwi vyeti vyao wakati wa Graduation tofauti na vyuo vingine vya Bugando na KCMC. Kwa sasa waliomaliza mwaka 2009 bado vyeti havijatoka wengune wamemaliza internship na kuajiriwa kwa utambulisho wa barua toka kwa Dean kwamba wamehitimu masomo yao na kutambulika kama madaktari na madaktari bingwa. Swali ni kwa nini vyeti visiandaliwe na kutolewa siku ya Graduation kama inavyofanyika Bugando na KCMC? kama kuna anayeweza kunipambanulia sababu humu jamvini naomba msaada.....nimepata kazi nje inayotaka cheti wakione na niwapatie kivuli cha cheti. sijaweza fanya hivyo. Shida ni uongozi wa chuo hauthamini wanafunzi kupata vyeti vyao kwa wakati?