Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

Continued..........

isipokuwa wawajibishwe kwanza.

Maneno ya Mzee Dr. Hans Kitine yasipite hivi hivi, yafanyiwe kazi ili hizi PhD feki za akina Nchimbi et al, ziondolewe mara moja.

Mbona Kihiyo alishikiwa bango WHY NOT Nchimbi et al
 
Hivi ni kwa nini hawa wote wenye hizi PhD za kupika inaonekeana wote wamesoma katika vyuo vya IDM, IFM and the like? Just curious!

Kuna moja wetu amesema haoni tatizo kwa wanasiasa kuchipachika hizi PhD. Mimi nafikiri ni tatizo kubwa sana kwa viongozi kujiingiza katika mkumbo wa udanganyifu. Tutawaogopa sana. Maana hata mambo wanayoyaongea tutawaamini vipi?

Mzee ES ungetusaidia sana kama ungeongea na waheshimiwa wenzake ili hatimaye hili jambo lifike bungeni na litatuliwe once and for all. Hili ni donda ambalo lazima litibiwe haraka. Vinginevyo tunatoa taswira mbaya kwa vijana wetu, kwamba elimu ni rahisi kiasi hicho, unaweza kununua tu madamu una hela! Nafikri ushahidi uliokwisha kutolewa unatosha kabisa.

Kwa maelezo ya Assad, sidhani kama Mkandara atanyanyua mdomo na kalamu tena katika hili, itabidi ajifiche tu!
 
mwanasiasa,

Katika post ya 49 unadokeza mmoja wetu kusema haoni tatizo kwa wanasiasa kujipachika hizi PhD. Ninadhani unajaribu kunukuhu vile nilivyosema mimi. Mimi nilisema "Hili la wanasiasa kuwa na PhD hizi sio baya kama lile la hawa walimu wa vyuo vikuu." Nikuhakikishiye kuwa sihafiki kabisa mtu yeyote kujipachika mambo feki haya ila nilichokuwa nikikiongelea hapa ni ngazi ya ubaya pale ambapo hawa walimu tunaowategemea pia wanafundisha kwa uzito au niseme wepesi wa vijivyeti hivi. Utashangaa pale Mzumbe eti nao wanatowa PhD za Public administration. Hebu jiulize ni "professor" yupi huyo ambaye atakuwa anawasupervise wanafunzi wa PhD hizo kama si yule yule mwenye ile ya Public administration ya PWU. Hii ni hatari kubwa.

Mimi pia ninashangazwa na hawa jamaa kwani karibu wote wenye PhD feki utaona wamesomea shahada zao za bachelors na masters kwenye vyuo vinavyoeleweka. Kweli badda ya usomi wote huo wanashindwa hata kujuwa kuwa hizi PhD zao ni feki - tuseme basi hata kusomea hizo shahada nyingine waliyumbayumba tu madarasani. Wanajitowa kwenye daraja ya msomi wa chuo kikuu, wanashindwa hata kujuwa kuwa kuwa na cheti ni ushuhuda wa kufuatilia programme ya shahada fulani, bali si ushuhuda wa usomi. Msomi hufanya na kutenda kufuatana na elimu yake.
 
Mwanasiasa
usitegemee sana kwenye makala ya Dr.Assad kwani yeye yuko one sided ameshindwa kuwataja watu anaofanya nao Idara moja ambao wa PHD feki mfano Baisi lakini amekazana kusakama Mzumbe university! nimemjibu vizuri tu kwenye mada ya Mzumbe na lecturers feki.
 
Nungwi
Ni kweli mwandishi (Dr. Assad) hakukataa kuwa UDSM hamna mchezo huo. Huo mchezo upo kwenye vyuo vingi vya ndani na nje ya nchi.

Tatizo alilozungumzia Assad ni ufeki wa Degree zenyewe na sehemu zilizopatikana na nafasi yake kwenye vyuo vyetu.

Tatizo kubwa Mzumbe ni kwamba wote wamepata hizo Degree kwa muda mmoja na kutoka Sehemu moja na hata bila kutoa mguu ndani ya ardhi ya Tanzania. It is impossible to do any PhD purely online.
Pia swala lingine ni hao wahusika kudai walipata Masters zao kutoka Mzumbe University angali tunafahamu na kutambua kuwa Mzumbe University hakuwahi au haikuwa na madaraka ya kutoa degree mpaka ilipotishwa mwishoni mwa 2001 na mahafali yake ya kwanza ya Degree yalikuwa Academic year 2002/2003.

Infact hata department wanazodai kupata hizo degree zao ni kwamba nyingine mpaka sasa hivi bado hazipo.

Tatizo hapa siyo kwamba wana feki PhD tu kutoka nje bali wengi wao pia wana fake Degrees kutka kwenye hicho chuo chenyewe.

Yaani kama tumefikia hatua ya kuwa na Vice Chancelor kihiyo na mwizi wa degree, tunategemea nini kutoka kwa wale ambao tunaongozwa na huyo mhusika.

kwa mtindo huu, sioni taifa lenye maendeleo.
 
Hivi huko Mzumbe kuna nini jamani, nakumbuka wakati ule watu waliokuwa wakishindwa kupata za kuingia UDSM, walikuwa ndio wanaomba kujiunga na Mzumbe...........................bado najiuliza maswali mengi tu
 
Tatizo hilo la kuwa na walimo bogus kwenye chuo kama Mzumbe kinatokana na kule ku upgrade Institutes kuwa full fledged universities bila ya kuwa na strategic plan ya capacity building. Chuo kama Mzumbe hawakuwa wanabanwa sana kuwa na calibre fulani ya academic staff. Kwa mfano vyuo kama UDSM na SUA bila kuwa na PhD unakuwa kama umeandikwa na penseli, kwa maana chief academic office hatakuacha kwa amani mpaka uregister shule either with au nje ya nchi. Kwenye vyuo hivi hasa SUA sina uhakika na UD hauruhusiwi kuwa Prof mpaka uwe na PhD. Sasa ukiangalia Mzumbe, Chuo cha Ushirika Moshi na may be IFM kuna maprof ambao wana Masters. Mgogoro unakuja wanapo upgrade kuwa chuo kikuu, hawa maprof wazamani kwenda shule shule tena inakuwa mgogoro. Matokeo yake ndio hivyo wengine wanaamua kuchukua shortcut ya PWU.

I really admire chuo cha Mzumbe, muda si mrefu with a proper strategy chuo kina potential ya kukua haraka. Lakini sasa huu uozo wake wa fake qualifications za members wake wa academia casts a shadow of doubt on calibre of its graduates.

Nungwi acha ushabiki, kama kweli una mapenzi na chuo chako shout at them to clean their house. They have a duty to the public as they are funded by tax payers money.
 
mTZ,

Good points, nafikiri Nungwi ataelewa unachosema.

Hizi academic ranks, inategemea sana na system husika, suala muhimu ni ktk machapisho ya kitaaluma ktk majarida mbali mbali yanayoeleweka kielimu/kitaaluma na kuandika vitabu. system zingine hutangaza nafasi za U-Prof, wakati system kama ya UDSM ambacho ni chuo mama kwa SUA niwazi lazima uwe PhD holder ili uje kuwa Prof.,
Kuna exceptionals kama kwa Prof Jengo (huyu aliifanya PhD baadaye), Mar. Prof Kairuki etc kutokana na kazi zao kuwa exceptional na wakatunukiwa na Vyuo vinavyoheshimika kielimu duniani.

Mzumbe ilibidi wapitie mbinde zilizowakuta then ARDHI INSTITUTE now UCLAS, kuna watu wakti huo mpaka Mkuu wa Chuo walijipachika U-Prof, wengine Senior Lecturers, walipokuwa affiliated na UDSM tu walibaki wachache sana wenye ranks zao, Mkuu wa Chuo naye alipigwa chini etc etc.

Mh. Msolla heshima yako Mkuu,
Hebu fanya kweli ili elimu yetu, iwe na heshima yake, na sio watu kujipachika pachika huku wakididimiza elimu nchini.
 
Nungwi mi naona we unatuzingua hapa, unataka kudivert attention. Naomba utueleze wanabodi kama tuhuma hizi kuhusu member wa academia Mzumbe ni ni za uongo? Personally nilishasema kwenye one of the my previous post how I admire MU, that Uni has a potential for high reputation. Tatizo ni hao watu wachache with their bogus qualifications, Nungwi hii kitu ruins the academic reputation of MU regardless of how great Mzumbe is or will be!

Naomba tusifanye mud slinging ya watu, nimecheki kwenye web profiles za Chijoriga na Baisi http://udec.udsm.ac.tz/associates.php

Dr. Marcellina Chijoriga is a Senior Lecturer in the Department of Finance, Faculty of Commerce and Management, University of Dar es Salaam. She holds a B.Com degree in Accounting from the University of Dar es Salaam, Tanzania, an MBA in Finance from the Catholic University of Leuven, Belgium, and a Ph.D. in Economics and Finance from the University of Economics and Business Administration Vienna, Austria. She also holds a Postgraduate Diploma in Institutional Economics from the University of Connecticut-USA and a Diploma in Business Administration from the College of Business Education, Dar es Salaam.

Mutahyoba Baisi is a Lecturer in the Department of Finance in the Faculty of Commerce and Management at the University of Dar es Salaam. He has worked for the University of Dar es Salaam since 1982 when he graduated with a B.Com honors. Prior to joining the University Mr Baisi worked as a Trade and Industrial Assistant with the Ministry of Industries and Trade for two years. Mr Baisi holds an MBA in International Business and Finance from the University of Antwerp ( Belgium) and an MBA in Finance and Accounting from Florida A & M University (USA). Currently, he is finalizing his PhD in Finance at the University of Dar es Salaam.

Sasa hawa jamaa ni chuo kipi walichosoma ambacho hakitambuliwi kama ilivyo hao "vihiyo" wako?

Naomba usishabikie mambo tu kwa vile wewe ni alumni wa Mzumbe, we all want MU to reach its anticipated academic achievement for the beterment of our nation.
 
Prof Msolla decries forged certificates in EA

DASSU STEPHEN
Daily News; Tuesday,December 12, 2006


THERE has been an increase in forgery of academic qualifications, examination leakages and emergence of persons with dubious academic certificates, including degrees and diplomas in East Africa.

In view of this, the Minister for Higher Education, Science and Technology, Prof Peter Msolla, has challenged members of Inter-University Council for East Africa (IUCEA) to double efforts to arrest the situation.

Prof Msolla was speaking yesterday during a workshop on the development of quality assurance handbook for East African universities attended by representatives of the three countries’ higher education accreditation councils, universities’ quality assurance bodies and the Germany International Exchange Programme (DAAD)

He said: “I challenge you to take up the issue of bogus providers of higher education and other frauds in all forms and manifestations. Already Tanzania, and I believe Kenya and Uganda, are experiencing increasing incidences of forged academic documents, examination leakages and emergence of persons accessing providers of and obtaining certificates, diplomas and degrees of no academic quality or validity.”

Prof Msolla urged the regulatory organs in the countries to take necessary measures to protect the public. “This would inhibit persons with fake qualifications to access opportunities for and obtaining admissions in higher education, job positions and promotions, and even assuming undeserved academic titles. If this trend is left unchecked, it would lead our countries into wrong destinations,” he cautioned.
He also called for concerted efforts to confront educational challenges of the day.

“We need a regional quality assurance handbook that is nationally, regionally and internationally credible. I believe that a proposed handbook will serve both our regional and international purposes, that will assist our universities to improve their commitment to quality education,” he noted.

IUCEA is a regional inter-governmental organisation whose mission is to encourage and develop mutually beneficial collaboration between universities in East Africa, and between them and governments and other organisations, both public and private.

As part of efforts to promote quality education, several universities in the region have been engaged in exchange programmes.

The Vice-Chancellor of Saint Augustine University of Tanzania (SAUT), Fr Dr Charles Kitima, told the Daily News: “We are collaborating with other universities such as the University of Dar es Salaam and Georgetown University based in the US. SAUT has sent at least ten lecturers abroad as part of an exchange program, this year,” he said, adding that it has become difficult to send a big number of students abroad due to high costs.

He also said SAUT had been striving to ensure the university’s curricula suited current demands. “We review our curricula after every three years to cope with changing purposes and needs.”

Another member, Prof Mayunga Nkunya of the University of Dar es Salaam, challenged IUCEA members to share and harmonise ideas that will ultimately assure quality education to the people.


Kama madai ya Prof. Msolla ni ya kweli na yeye ni waziri wa elimu ya juu.. basi aneshe mfano kama kuna mtu yeyote Bungeni au katika Baraza la Mawaziri mwenye shahada hewa!!!
 
Yeye nafikiri katoa changamoto. Ni jukumu la hizo accreditation bodies kuhakikisha kuwa hali iliyoelezwa haiendelei tena. Sidhani kama ni jukumu la waziri kwenda kuwashika mashati wahusika. Atakuwa amekosea pale atakapovikwaza hivi vyombo kutekeleza wajibu wao.
 
Kitil Mkumbo,
Alichokitoa Prof. Msola sio changamoto, kwani ni marudio ya wimbo uleule, huitaji kuwa Dr. au Prof, kufahamu alichokisema Msola, anachokifanya ni kujikosha tu kana kwamba yeye hausiki wakati wizara yake ndiye muhusika mkuu.
 
Hizo namba za simu za kwenye website ya bunge hawazitumii siku hizi, kwani Wabongo wanatumia kuwabeep na kuwapiga mizinga isiyokwisha. Badala ya kuwaeleza matatizo ya msingi wanaendelea kuwakumbusha, mzee mimi ndio yule kijana niliyekuwa nikikuimbia wakati wa kampeni sasaa......
 
Dar MPs’ fake degrees being probed as concern rises over bogus universities

A JOINT REPORT
The EastAfrican


At least seven legislat-ors in the Tanzanian parliament are having their qualifications investigated on suspicion that they have been obtained from unaccredited institutions.

According to information obtained by The EastAfrican, among the seven legislators who are the subject of an internal inquiry by a House committee are ministers, deputy ministers and ordinary MPs.

Moreover, the actual number may turn out to be higher given the fact that more public figures are said to be holding diplomas and degrees from questionable institutions, most of which offer online courses.

Reports have it that the matter has now been referred to the Speaker of the National Assembly, Samuel Sitta.

A good proportion of Tanzanians in the parliament and in the East African Legislative Assembly (EALA) are holders of Masters degrees and PhDs.

However, Deputy Speaker Anna Makinda told The EastAfrican last week that it was not the duty of the parliament to scrutinise the authenticity of the “degrees” because the only academic requirement for an MP is to know how “to read and write.”

She added that once the National Electoral Commission (NEC) announces the names of MPs, “our duty as parliament is to receive them. If there are allegations of academic fraud, it’s not the duty of parliament to investigate,” she said. Such issues are dealt with by other relevant authorities.”

The problem of fraudulent academic achievements is not confined to politicians or those in public service; it is endemic even in the medical field, engineering and other professions.

The most notable case was that of a Ms J Gewe, who four years ago not only masqueraded as a pathologist at the Dodoma regional hospital, but also attended theatre operations for a year in the same hospital without being detected.

She was later arrested and prosecuted.

The media has also not been spared as some journalists are said to have obtained their degrees from a university in the UK over a relatively short period, leaving many questions unanswered.

Already, an MP from the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) has been reported to the Director of Public Prosecutions (DPP) over his academic qualifications.

Minister for Science and Higher Education Prof Peter Msolla has cautioned that many people in public life have questionable academic qualifications.

Tanzania Commission for Universities (TCU) executive secretary William Sabaya told The EastAfrican last week that the Commission was now assessing certificates, diplomas and degrees to awarded by various institutions to determine their authenticity before taking legal measures against the culprits.

Mr Sabaya said there were many people in the country with PhDs obtained under dubious circumstances without following the curricula stated in the TCU regulations.

“The issue is sensitive, because withdrawing such degrees and diplomas from those holding them is like snatching the bread from their mouths,” he said. “We have instructed all holders of MA and PhD degrees obtained from abroad to present their certificates to TCU for authentication.”

According to Mr Sabaya, TCU has categorically instructed all concerned that to get a certificate from any institution, whether overseas or locally, one must have studied for a year, while for an ordinary diploma, one should study for two years and between two and three years for an advanced diploma.

For a first degree, a student must have studied for three years, while a Masters degree, takes between one and two years.

For a PhD, one must study for not less three years, depending on the discipline.

Mr Sabaya said the Commission has published a document — Degree Mills — detailing the various illegal means of obtaining qualifications.

Recently, the Minister of State in the Vice President’s Office in charge of Environment, Prof Mark Mwandosya, warned over the problem.

Speaking during the commemoration of the African University Day on December 19, Prof Mwandosya said the “Rapid developments in information and communication technologies have accentuated a problem that is as old as university education itself, that of degree mills and fake diplomas.”

Prof Mwandosya said that fraudulent institutions have cropped up offering degrees in a short time, with much less work than would otherwise be required, and placing emphasis on work or life experience in the provision of credits.

“They will invariably develop a customised degree for the applicant in order for him or her to complete, say, a doctorate, in the shortest time possible — usually a year —and at a least cost,” he said.

Prof Mwandosya said degree mills develop interesting websites, but usually have a disclaimer, such as the one put up by the Commonwealth Open University: “We cannot guarantee that a Commonwealth Open University Degree will be accepted or recognised.”

He further said that many unaccredited colleges or fraudulently credited ones come up on various websites that caution about doubtful academic credentials.

Yet a number of lecturers in African Universities, public servants and “us politicians are recipients of these fake degrees from these institutions,” said Prof Mwandosya.

“The mushrooming of new universities in our country could easily fall prey to those degree mills,” he warned. “Older, established universities such as the University of Dar es Salaam have a duty to assist new universities and the public to screen bogus degrees, and to help higher education accreditation councils come up with legal frameworks to deal with this problem, which could turn out to be a major threat to sustainable development,” he said.


Reported by Joseph Mwamunyange and Mike Mande
http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/News/Regional010120071.htm
 
Internet fuels explosion in ‘degree mills’

By A STAFF WRITER
The EastAfrican

"Degree and diploma mills” have been around for hundreds of years, and they are still flourishing all over the world.

These are bogus universities and colleges that sell diplomas or degrees — a piece of paper itself rather than the educational experience.

Tanzanians, and the East African region in general, have not been spared this bogus education. Degree or diploma mills are unaccredited, usually online “colleges” or “universities” that offer fraudulent and worthless degrees in exchange for payment alone or for payment and very minimal work — often a “research paper.”

These degree and diploma mills often claim accreditation from fraudulent “accrediting agencies” to mislead prospective students and employers. In most cases, the bogus accrediting agencies are operated by the same people who own and run the mills.

During the 1980s, in the US, the number of bogus schools significantly diminished as a result of the famous “Dipscam” diploma-mill task force set up by the Federal Bureau of Investigations (FBI). Its operations helped secure indictments and, in many cases, convictions of a great many people who operated scores of fake colleges and universities.

But today, with the advent of inexpensive laser printers, colour copiers, faxes, computer bulletin boards and other technology, most significantly the growth of the Internet, diploma mills have made a massive comeback, both in the US and Europe.

There are now many places in the world where one can buy Bachelor’s, Master’s, doctorates, even law and medical degrees, with no questions asked, on payment of fees of anywhere from a few dollars.

One of the reasons that fake universities continue to exist is that it is difficult to legally define exactly the term “diploma mill” or “degree mill,” although any university that will send someone a PhD by a return mail on payment of say $100, with no questions asked, is obviously a fraud. To make matters worse, it seems, “one man’s degree mill is another man’s alternative university.”

By the late 1980s, there were less than 50 bogus colleges open to the public in the US, but the number now exceeds 750. They maintain impressive websites and advertise heavily online.

Another area where degree mills are rampant is religious institutions, mostly in the US. Because constitutional safeguards in the US guarantee separation of church and state, most states have been reluctant to pass any laws restricting the activities of churches — including their right to grant degrees to all who make an appropriately large donation.

According to acknowledged experts in both legitimate and degree mills, Dr John and Mariah Bear from the Michigan State University, in some areas in the US, like Louisiana and Hawaii, “If you established your own one-person church yesterday, you could start your university today and award a PhD in nuclear physics tomorrow.”

Dr Bear says there are three types of people who enrol in degree mills programmes: “People who know and don’t care, those who have suspicions but take a chance and those who are fooled. However, the last category is a small minority.”

A number of degree mills operate out of England, selling their products only to people in other countries, primarily the US, Africa and Asia. The perpetrators continue to advertise in nearly every issue of major newspapers and magazines in the world. Degrees and diplomas issued by diploma mills are frequently used for fraudulent purposes, such as obtaining employment, political advancement, salary raises, or to recruit customers on false pretences and at times in terrorist activities.

Most of these fraudulent colleges are also short-lived, making detection even more difficult. They can start up, collect large sums of money from consumers, go out of business, change their name and emerge as a new entity in a short period.

This is occurring at the same time that there is more pressure on individuals to earn degrees, not only Bachelor’s degrees, but Master’s and doctoral degrees as well. Jobs and promotions increasingly go to individuals with the greatest educational qualifications, even when individuals’ work experience may be more relevant to the job than a degree. This is what creates pressure on individuals to obtain degrees, tempting some to take the easy route to a degree — the degree mill.

The primary reason to be concerned about degree mills is that they demean the value of learning and the importance of educational standards by treating degrees only as a commodity to be bought and sold. Degree mills also defraud individuals who are misled by the promises made by such schools that the degrees they earn from the schools are valuable.

Such individuals with bogus degrees also present a danger to the public. This is particularly true of those who receive bogus credentials in the fields where they could present a threat to health, safety or well-being. The Internet is becoming a haven for degrees and diploma mills.

A quick look at the degree mills advertising on the Internet shows that they offer degrees in fields such as nursing, nutrition, electrical and mechanical engineering, biochemistry and accounting, at significant risk to the public. Also, degree mills are unfair to the millions of individuals who have worked hard to earn legitimate degrees.


Source: http://www.nationmedia.com/eastafrican/current/News/Regional010120072.htm
 
Siri ya wahadhiri wasiofaa yafichuka

Rehema Isango
HabariLeo; Monday, January 01, 2007

KUAJIRIWA kwa wahadhiri katika baadhi ya vyuo vikuu bila kuhusisha Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) ni moja ya sababu za kuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha vyuoni. Pia upungufu wa wahadhiri nchini, umesababisha baadhi ya vyuo vikuu binafsi kuajiri wahadhiri wa kigeni bila kufuata taratibu zilizopo.

Katibu Mtendaji wa TCU, William Sabaya aliiambia HabariLeo hivi karibuni kuwa kama Tume yake ingekuwa inashirikishwa, basi kusingekuwa na matatizo hayo. “TCU imeshuhudia tatizo hilo kwa baadhi ya vyuo binafsi vilivyoanzishwa kwa kuwa vilikosa wahadhiri wa kutosha na wenye sifa kutoka nchini , hivyo kuingia gharama ya kuajiri wahadhiri na waendeshaji kutoka nje ya nchi” alisema Sabaya.

Sabaya alifafanua kuwa ,hatua ya kuajiri wahadhiri hao ilifanyika kwa kuzingatia taratibu zilizopo za Serikali, lakini vilishindwa kuihusisha TCU ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kuhakiki ubora wa elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.

Sabaya alisema kuwa ,baada ya kubainika kwa tatizo hilo, hivi sasa TCU inashirikishwa katika shughuli za kutathimini sifa za wahadhiri kutoka nje ya nchi wanaoomba vibali vya kufundisha katika vyuo vikuu nchini.

TCU imetaja sababu za wahadhiri wasio na sifa na uwezo wanaodaiwa kuwepo katika vyuo vikuu vya binafsi kuwa hali hiyo inatokana na upungufu wa wataalamu wenye sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu katika soko huria.

Hivyo kusababisha kutegemea wahadhiri wachache wanaopatikana katika vyuo vya umma, kwa mpango wa ajira ya muda mfupi au kuajiri wataalamu wasio na sifa za kufundisha masomo ya vyuo vikuu.

Sababu nyingine ni uwezo mdogo wa wenye vyuo binafsi katika kupunguza gharama za uendeshaji, kwa kushindwa kulipa mishahara na marupurupu ya kuwavutia wahadhiri wenye taaluma na uzoefu kutoka ndani na nje ya nchi.

Sabaya alisema kuwa ,baadhi ya wamiliki wa vyuo katika kulinda mambo yao kadhaa kama vile imani, maadili na pengine siri za biashara na mwelekeo mzima wa chuo, kumekuwa na hali ya kutokuwa huru kuajiri wahadhiri na wafanyakazi ambao wanaweza kuwa tishio kwa mambo ambayo mmiliki ana wasiwasi nayo.

Sababu nyingine imetajwa kuwa ni kukosekana kwa uzoefu wa kuendesha vyuo vikuu kwa baadhi ya wamiliki, hivyo kushindwa kutafsiri vema katiba ya Jamhuri ya Muungano, sheria na kanuni za miongozo ya TCU hususan zile zinazoelekeza taratibu za kuajiri na udahili wa wanafunzi.

Alivitaja vyuo vilivyowahi kukabiliwa na upungufu huo kuwa ni Chuo Kishiriki cha Zanzibar, Chuo Kikuu cha Bukoba ambacho kimesitishwa toka mwaka 2000 na Chuo cha Kimataifa cha Teknolojia ya Udaktari (IMTU).

Sabaya alifafanua kuwa, TCU ilibaini kuwa IMTU ilikuwa na wahadhiri wasio na sifa za kufundisha baadhi ya masomo tangu mwaka 2003, na ilikiagiza kusitisha udahili wa wanafunzi katika kozi hizo kwa muda wa miaka miwili ili kupata muda wa kujiandaa kutafuta wahadhiri aliotakiwa.

Hata hivyo, HabariLeo imeshuhudia kuwepo na wahadhiri kadhaa katika vyuo binafsi ambao hawana sifa za kufundisha katika Chuo Kikuu maarufu kilichopo mkoani Iringa(Jina tunalo) na wengine wanaofundisha katika Taasisi ya uandishi wa habari na masuala ya biashara ya jijini Dar es Salaam.


Chanzo: http://www.dailynews-tsn.com/habarileo/page.php?id=179
 
Back
Top Bottom