Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,967
- 11,212
Naomba kutoa hoja kwa wanafamilia wa JF,mimi naona kuna ulazima kwa mamlaka husika kuunda tume itakayoshirikisha wakuu wa vyuo vyote vilivyopo hapa nchini na kuwasiliana na wale wa vyuo vya nje ili kufahamu au kujilizisha na vyeti vya baadhi ya waajiriwa serikalini, juzi tumesikia waheshimiwa wawili tena wenye vyeo vya juu wakituhumiwa kwa kuwa na vyeti bandia na hivyo elimu yao kutilia shaka, mimi naamini si hao tu wapo wengi wenye vyeti bandia au vya marehemu wakivitumia kujipatia ajira isiyowahusu, Tanzania haiwezi kuendelea, mtu mwenye cheti bandia hata kazi zake nazo ni bandia tuuu...
Yaani hii ndivyo inavyoonekana si ajabu tunabaki tunashangaa taifa limejaa viongozi wasomi mbona amna maendeleo kumbe wengi bandia tu.
Ndio maana wasomi wa-kweli huwekwa kwenye mabalozi yetu ugenini na hawa bandia ndio wame jaa humo serikalini. Its about time nakubaliana na mapendekezo yako moja kwa moja, lakini je is it possible kwetu kufanya hilo jambo.