Tanzania: Vyeti bandia, elimu za kununua na watumishi vihiyo

Matata

Member
Mar 28, 2006
23
10
Jamani wanajumuiya ya Wa-Tanzania tuishio British Virgin Islands tumeshutushwa na habari kuwa kuna baadhi ya viongozi wetu serikalini wana shahada za PhD kutoka kisiwani hapa. Ukweli hapa hakuna chuo kama hicho. Hiki kisiwa ni kidogo mno kuna wakazi wapatao 23,000. Kisiwa hiki kina secondary 2 na community collage moja.

Uchumi wa kisiwa hiki unategemea sana Utalihi na Financial services which includes offshore banking and registration of companies. Baada ya kutembelea web site ya Commonwealth Open University, Ni kweli nimegundua kuwa imekuwa registered hapa. Cha ajabu address yao ni ya hapa(box no.) lakini, Palm Chambers ambalo ni jengo halipo hapa. Kuonyesha kuwa ni fake, hawakutoa simu yao, ila wametoa fax number. Kutokana na fax number hizi number ni za USA (Florida).

Baadae nilikwenda kwa msajiri wa makampuni nilielezwa kuwa Commonwealth Open University imekuwa registered kama kampuni lakini haina Learning Institution yoyote. Baada ya kuuliza zaidi information hizo, niliambiwa nijaze form harafu nitapewa details baada ya kulipia $ 25.

Registry Of Corporate Affairs,
P.O . Box 418,
Road Town, Tortola, British Virgin Islands.
Fax 1 284 494 6331:
Simu 1 284 494 5491:
E-mail corporateregistry@bvifsc.vg Website www.bvifsc.vg

Sikuweza kulipia ili nipate maelezo hayo. Baada ya kujadiliana na wenzangu hapa tumejua kuna watu wajanja wachache wanatumia mwanya huu kuwaibia fedha watu na kuwapa degree baada ya kuwalipa pesa. Hicho chuo hakipo, hao jamaa ni matapeli.

Naomba serikali, Wizara ya Elimu, UTUMISHI mjue kuwa hakuna chuo kama hicho hapa. Kama kingekuwa ni chuo basi tungeweza kuona hizo ofisi zao hapa. Kuna Mtanzania mwenzetu ambaye amekaa hapa zaidi ya miaka kumi. Hajawahi kuona ofisi hiyo (Palm Chambers).

Tuko tayari kushirikiana na mtu yoyote ili kukomesha ununuaji wa yeti fake hasa kwa viongozi wetu.

Shukrani.

===========
Nov 10, 2014:

Watumishi 1,360 wakutwa na vyeti feki

UDANGANYIFU katika vyeti wakati wa kuomba ajira umeendelea kukithiri nchini, ambapo ndani ya mwaka mmoja tu, kuanzia Julai mwaka jana mpaka Juni mwaka huu, watumishi 1,360 wamekutwa na vyeti visivyo halali. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, alisema hayo jana mbele ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, wakati wa uzinduzi wa bodi mpya ya baraza hilo.

Katika uhakiki huo, baadhi ya watumishi wakiwemo wa Serikali walikutwa wakitumia vyeti vya kughushi ambavyo imebadilishwa matokeo, wengine walikutwa na vyeti vya bandia huku wengine wakitumia vyeti vya watu wengine.

Hii si mara ya kwanza kwa Serikali kuelezea uozo huo katika elimu, ambapo Julai mwaka jana Msemaji wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Riziki Abraham, alitoa taarifa ikieleza kuwa Sekretarieti hiyo ilibaini kuwepo kwa udanganyifu wa vyeti 677, kwa watumishi serikalini.

Aidha, Oktoba mwaka jana Ofisa Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Sekretarieti hiyo, Kasim Nyaki, alieleza kuwa vyeti vya Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi (Veta) ni miongoni vyeti vinavyoongoza kutumiwa katika udanganyifu kwa watu wanaoomba kazi kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Nyaki alisema kuwa kati ya watu 517 waliotumia vyeti vya Veta kuomba ajira kupitia sekretarieti hiyo, watu 304 walitoa vyeti halali, lakini watu 213 walighushi.

Mbali na hao, alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa kati ya watu 13,554 walioomba ajira katika miaka mitatu yaani 2010, 2011 na 2012, watu 816 walibainika kudanganya kwa kutumia vyeti vya taasisi mbalimbali za elimu, vyeti vya kuzaliwa na vinginevyo.
Kutokana na hali hiyo, Dk Msonde alisema Baraza hilo limeamua kushirikiana kwa karibu na mamlaka za ajira na udahili, ili kuhakikisha uhakiki wa vyeti vinavyotolewa na baraza hilo, unafanyika kabla ya mtahiniwa kuajiriwa au kudahiliwa.

Mbali na ushirikiano huo, Baraza hilo limeazimia kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu madhara ya kutumia udanganyifu katika vyeti.

Aidha, Baraza hilo pia limeanza kutoa vyeti vyenye picha ya mmiliki kuanzia 2008, ili kupunguza kasi ya udanganyifu huo.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limeanza utaratibu wa kutoa vyeti mbadala kwa watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa waliohitimu kuanzia mwaka 2008 ambao vyeti vyao vilikuwa na picha.

Dk Msonde alisema hatua hiyo ya kutoa vyeti kwa waliopoteza, inatarajiwa kupunguza changamoto zilizokuwa zikiwakabili watahiniwa waliopoteza vyeti vyao kwa sababu mbalimbali kwa kupata vyeti mbadala, huku likiweka utaratibu madhubuti kuhakikisha fursa hiyo haitumiwi vibaya.

Akizungumzia kudhibiti wizi na udanganyifu katika mitihani, alisema Baraza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamedhibiti na kuondoa kabisa tatizo la wizi wa mitihani ya taifa na kwa kiasi kikubwa na kudhibiti udanganyifu wakati wa ufanyaji mitihani.

Alisema Baraza hilo linakabiliwa na upungufu wa fedha za kuendesha mitihani ya taifa, ambao usipofanyiwa kazi, utaathiri uendeshaji wa mitihani ya kidato cha sita na ualimu.

Ukata huo alisema pia utaathiri uongezaji wa viwango vya posho za wasahihishaji kwa mitihani ya kidato cha nne, sita na mitihani ya ualimu kama ilivyokuwa imepangwa.

Alisema katika mwaka wa fedha 2014/15, kulikuwa na umuhimu wa kuongeza posho ya wasahihishaji kwa kuwa posho hiyo imekuwa ikilalamikiwa na washiriki kwa kuwa ni ndogo ikilinganishwa na posho zinazolipwa na mamlaka nyingine, ikiwemo Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa shughuli za mitihani.

Akizindua bodi hiyo, Waziri Kawambwa alisema wakati matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yakianza kutolewa kwa mfumo mpya wa Wastani wa Pointi (GPA) ni vema kutoa elimu wakati huu kabla na baada ya mtihani, ili kuzuia mtafaruku.

Alisema utoaji wa elimu kwa wadau wote wa elimu, wanafunzi na wazazi utasaidia kudhibiti upotoshaji mara utekelezaji utakapoanza.

“Hili lifanywe kwa juhudi na umakini ili kuepusha upotoshaji unaoweza kufanywa na baadhi ya watu, elimu kuhusu mfumo mpya wa kutunuku matokeo itolewe kwa kutumia aina zote za mawasiliano na umma kabla, wakati na baada ya mitihani.

Bodi hiyo mpya inaongozwa na Mwenyekiti wake, Rwekaza Mukandala na wengine ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Taaluma), Profesa Makenya Mabhoko, Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Watoto, Benedict Misani na Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Shule Binafsi, Mahmoud Mringo.

Wengine ni Mkurugenzi wa Baraza la Mitihani la Zanzibar, Ameir Selemani Haji, Mkuu wa Skuli ya Ualimu wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar, Dk Maryam Jaffar Ismail, Mkurugenzi wa Idara ya Sekondari, Asia Iddi Issa, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Shaban Kamchacho, Mkuu wa Sekondari ya Kisimiri Meru, Emmanuel Kasongo na Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Kimara Baruti, Rehema Ramole.


CHANZO: Habari Leo
 
Last edited by a moderator:
Umefanya vema ndugu yangu matata,

mwendo uwe ni hu huu kuwafichua mafedhuli.

Mh.Mkandara,
nafikiri sasa utakuwa umepata mwanga kidogo kuhusu degree za wakina Nchimbi
 
Ogah,

Na wewe usiwe mtu wa kukubali kila kitu,huoni kwamba huyu mtu kaleta hapa makusudi?... Anachosema Palm chambers ni jengo ambalo halipo sijui katembelea wapi kisiwa kipi -Tortola au Virgin Gorda kwani Palm Chambers ipo Tortola yote nimekwisha yafanyia uchunguzi siku nyingi.
Ogah, Ukiona mimi nashindwa kumbana mtu basi jua nimepita kila sehemu na kukuta nashindwa mimi.

Napenda sana kumbana Nchimbi na elimu yake kama kweli kagushi lakini kusema Commonwealth open haipo kwa sababu huyu jamaa hakuona jengo la Palm chambers ama sababu ya fax ya Marekani. Kwa taarifa zaidi, karibu kila kampuni alizozitaja jamaa zote zinazojishulisha na hayo mambo ya offshore, International business na Mutual funds n.k, zote ni office jina tu hakuna wafanyakazi wanye mashirika wote wanaishi Marekani na kazi zao zipo Marekani sio Virgin Islands.

Do they deliver?.... Yes they do kama mashirika ya meli yanayosajiri Ghana na Liberia. Kwa hiyo kama mtu unataka kusoma Commonwealth open fanya ku-apply kisha nambie hawakukupa jibu.
 
Wanabodi kwa taarifa yenu mimi nimeishi hapa kwa muda mrefu nina uzoefu wa registration wa makampuni hapa visiwani na ni sehemu ya kazi yangu iliyonileta hapa. Kuna baadhi ya kampuni zinaji-register hapa kukwepa kulipa kodi nchi usika.

Pia makampuni mengi ya kitapeli yanajificha huku kwani sehemu hii si rahisi kukamatwa. Sasa kama Commonwealth Open University sio fake kwa nini wasitoe address yao kamili, Tembelea website yao kama utakuta wamekuwekea simu zao. http://www.commopu.org/ Nimeenda hata kuchunguza box number yao nimekuta ni ya Law Firm moja. Labda kwenye hiyo Law Firm ndipo kuna mtu anashirikiana nao matapeli ambao mimi na amini wako USA. Mimi na wenzangu tuliona limejadiliwa sana kwenye Forum Bcstimes ndiyo maana nikalileta hapa kutoa mwangaza.

Bwana Mkandara inaonekana unaijua sana Virgin Islands(UK) lakini hiyo sio sababu ya kusema chuo hicho sio fake.

Sio Commonwealth Open University peke yake kuna vyuo vingi vinaendeshwa na wahindi na wanigeria wanatoa degree fake hawana hata walimu. Nilikutumia hata private message kuhusu mwanzo wa upelelezi wangu. Kwa taarfa yako all financial services are based in Tortola Road Town.

Mjue hapa tunapeana mawazo kama serikali italiona hili kuwa ni tatizo itachunguza, isipoona ni tatizo, basi wenye hizo degrree wache watambe.
 
Matata,

Inabidi nikupe picha kamili ya biashara hii ya Elimu nchi hizi za magharibi. Virgin Islands bado dunia ya tatu kwa hiyo vitu kama hivi lazima watu wanaona kama miujiza ya Mussa.

Kuna kitu kinaitwa University without walls (UWW). Hapa labda nikupe mfano kwa nyumbani.

Mfanyabiashara mmoja aamuwe kuwakusanya maprofesa wetu ktk masomo mbali mbali toka baadhi University na kuweka utaratibu wa mafundisho, nidhamu na n.k kwa kuzingatia ngazi zote za ufundishaji toka Universities nyingine. Kisha kundi hili wasajiri kampuni hiyo ktk wizara ya Elimu kama wanavyosajili hizo zahanati hapo Dar hali madaktari wake ni wafanya kazi wa Muhimbili au Hindu Mandal...

Kwa hiyo usajiri unakuwa kama Open university yaani masomo kwa njia ya Mtandao! hapa nadhjani ndipo wengi wanapote kwani tumezoea kuona zahanati nje ya hospital.. lakini nchi hizi kuna madaktari ambao wamesajiri Udaktari na huendesha shughulki zao nje ya Hospital au Zahanati. Hospital yake ipo mkobani, na address ni nyumbani kwake...na simu yake. Anywaya kufupisha story nirudi ktk mada, Baada ya usajiri wa hii Association hawa jamaa waitangazaeTZ nzima kama University ambayo huna haja ya kukaa darasani lakini maprofesa wote wakali wa UDSM wapo ndani kukusomesha kwa kupitia Mtandao. Hapa mshikaji hakuna majengo ila software yao yenye kila hatua ya mafunzo (publishers of materials) pia kuna huduma za online, multimedia, text kwa mtanzao na video, pia e-learning.

Yote haya yanatengenezwa hususan kwa elimu fulani na wataalam kwa kushirikiana na hao walimu wake. Sijui kama bado nipo na wewe?...

Sasa nirudi ktk swala la COU. Mwenye kila kitu hapa ni British learning Association (BLA) toka Uingereza ambao ndio wenye vitu vyonse!.. kisha wao huuza membership kwa mtu yeyote duniani mwenye kutaka kuwasaidia watu ktk elimu... iwe ngumbaru ama wale ambao hawakujaliwa kuwa na uwezo wa kulipia elimu. Yaani iwe na malengo ya kutoa huduma ya elimu kwa wananchi.. imekuwa kama mfano wa franchise kwa hiyo COU wao wamejiunga na BLA ili kupata ile UWW... kisha wanauza elimu hiyo kwa watu dunia nzima. Unaweza kukuta COU ina wanafunzi 200,000 across the world kila mwaka, na wote wanasoma kupitia mtandao na hupewa kasha la -CD (software) ambazo zitakuchukua wewe hatua kwa hatua na pia utajadili muda wa mafunzo yako toka hapo ulipo. Mathalan ukisema wewe upo Dar basi wao huwa na profesa wao ktk mitaa hii ambaye huchukua muda kukusaidia. Na kila anapokusaidia huingiza zake inategemea.

Kwa hiyo, COU kweli wamesajiri Virgin Islands kwa sababu ya kodi maanake wanazichota kishenzi. Mapato kama yao Uingereza, Marekani na nchi yeyote ile ya Kibepari wangeshika adabu maanake hawa jamaa hawana matumizi zaidi ya kulipia software ambayo BLA wameitengeneza. Hizi software zinauzwa kwa mamillioni sio kama windows na kila mwaka hufanyiwa marekebisho ama kutolewa toleo jipya. Huwezi kuipata software hiyo unless wewe ni member wa hiyo association.

Kwa hiyo COU wao hawana haja ya kuwepo Virgin Islands kwani lecturer wote wapo karibu na wewe popote duniani. Na kinachokuunganisha wewe na hao lecturer ni hiyo software kama vile unavyoingia MSN ama yahoo! Hapo COU hawapo tena wameisha kusanya mapeni na kazi yao ni kuwalipa hao maprofesa kwa kila kazi wanayoifanya...

Nadhani haya yametosha kwa lleo.
 
Mwanasiasa,

Sijui hoja yako inalenga wapi Kwani sidhani kama unawafahamu maprofesa wote duniani. Kumbuka saa hupimwa kwa marefu ya nyuzi - meridian kwa hiyo hapa Profesa aliyeko karibu nahuyo Kamala sijui ni yupi unayemtaka na atoke nchi gani ili upate kukubaliana na biashara hii ya Elimu.

Nimekwisha sema njia rahisi kabisa ni mmoja wenu a-apply shule tena kwa masomo yaleyale ya hao akina Nchimbi na Kamala kisha utawapata hao maprofesa na kuzipata data zao.

Ebu niwaulizeni hivi kweli ukiumwa na ukatibiwa nyumbani kwa daktari ambaye ni msataafu Kenya huwezi kupona kwa sababu tu hana address ya Muhimbili au Zahanati?...Je, huyu daktari tena Profesa atakuwa na upungufu gani ikiwa ataamua kufundisha medical ktk chuo kilichosajiliwa Marekani! hali hakuna mtu Marekani anayefahamu walimu wake..

Jamani tunajaribu kutafuta kitu gani hapa?... Digri ya Tumaini haitambuliwi Marekani, Je hii ina maana digri hiyo ni fake? Naa hata kama ina address na majina ya maprofesa wa Tumaini hii itamsaidia nini msomi wa Marekani?

Nachosema mimi Commonwealth open na vyuo kibao vya aina hii vinatambulika ktk baadhi ya nchi na institutions. Sijaona sheria ama sehemu inayosema taasisi fulani ya Elimu Tanzania haitambui cheti cha COU na sababu kubwa ni kuwa open university!

Mwanasiasa, Ukiangalia madai ya wote humu ni hayo ya COU kutokuwa na address, mshikaji siku hizi biashara inafanyika watu wakiwa angani na wengine kaburini... biashara sio address, leo hii ktk IT kuna kampuni kibao ukipiga simu unaongea na mtu toka Delhi, India ama Accra, Ghana akizungumza kama yupo vile Frolida, Marekani na kukupa ushauri wa ktk ununuzi wa share. Dunia ya mtandao ni kasi mpya tofauti kabisa na ile yetu tuliyokulia ya kucharazwa bakora na kukaa darasani masaa manane!..


Kukaguliwa uniform, meno na kucha na kupewa adhabu ya kutorudi shule mpaka umekuwa safi... familia maskini hakuna anayejali wala sii swala la shule. Ufugaji kucha siku hizi ni ulembo kwa akina mama, wengine wana meno ya dhahabu na vipini ktk ulimi. Lakini zina-charge kishenzi! Dunia mpya hii jamani kubalini changes mpango wa UDSM na Havard siku hizi siii majengo tu unaweza kusoma hata Havard kwa kupitia mtandao na address yake kwa elimu ya mtandao ikiwa tofauti kabisa na hiyo unayoifahamu wewe.
 
Mkandara:

Ukifuatilia vizuri huu mjadala utagundua kuwa issue hapa sio tu hiyo address. Hawa watu CWU wamekanwa na kila mtu anayejihusisha na utoaji wa elimu ya juu. Juzijuzi (11-13 March 2005) nilihudhuria mkutano wa Association of Commonwealth Universities (ACU) mjini London. Nilitumia wasaa ule kumuuliza boss wa ACU kama kuna taasisi inayoitwa Commonwealth Open University, akaenda akavuta lijitabu kubwa sana lenye all universities in the commonwealth na zingine wanazoshirikiana nao. Huyu mnyama COU hayumo.

Ili kujiridhisha zaidi akaniunganisha kwa maafisa wake ili kujua hiki chuo ni cha kina nani hasa na kipo wapi, hawakuona kitu, isipokuwa zile skeleton kwenye website yao. Mbaya zaidi wakaniambia mara nyingi taasisi yeyote inayotumia neno 'commonwealth' huwa ni moja ya taasisi za commonwealth organizations-bahati mbaya huyu mnyama COU si moja ya hizo taasisi. Kwa kuwa hawa wenzetu ni wafuatiliaji, kuna binti pale commonwealth secretariat aliachiwa kazi ya kutafuta zaidi information za COU na watawasiliana nami. Hii ni kwa sababu niliwaeleza jinsi hii issue ilivyo critical nchini mwangu.

Sasa Mkandara sijui tueleze nini tena; mimi nafikiri nitakuwa sina tena cha kuchangia katika huu mjadala maana data zote muhimu zipo hadharani. Kuna mwenzetu mtu amemuandikia Sabaya (Mkurugenzi mtendaji wa Baraza la Vyuo Vikuu Tanzania) ili watoe msimamo kuhusu accreditation ya hiki chuo. Sabaya hajajibu bado.

Akijibu nitaweka mambo humu humu ndani.
 
Kitila Mkumbo,

Na kushukuru sana kwa kufatilia hii issue hii na utafiti wako. Swala COU sikulianzisha mimi bali limekuwa linajadiliwa kwenye forum mbali mbali. Kwenye utafiti wetu tutagundua ukweli wa hili swala. Aksante sana.

Mkandara;
Nashukuru kwa maelezo yako. Karibu kila kitu ulichokieleza na kifahamu, isipokuwa kuna baadhi ya watu wanatake advantage IT na Globalization kudanganya watu. Mfano, kuna baadhi ya watu wanatumia nembo ya UN (United Nations) kutangaza kazi za wazi. Mimi mwenyewe kidogo ni ukwae mkenge. Hawa matapeli walitangaza Kazi za Assistant UN Resident representatives, walituma kwenye mashirika mbali mbali ambayo waliona yanashughulika mambo ya Economic Planning/ Finance. Institution yangu ni moja wapo iliyopata hilo Tangazo kwa Fax.

Mimi nilituma maombi baada ya week 2 nilipata mail yao kunieleza kwamba nimefanikiwa, mshahara wenye bila malupu ilikuwa US $110.000 kwa mwaka (tax free) bila malupulupa. Wakanieleza mipango ya visa ya US kama sina wakasema wataifanya, isipokuwa walisema napashwa kuhudhuria training ya miezi sita Washington kwenye Institution fulani. nilitakiwa nilipe $ 3,000 kwa ajili ya training kwenye Bank Account fulani, hela hizo walisema nitarudishiwa na UN baada ya kuanza training. Hapo nilishutuka nilianza kutumia watu ambao ni rafiki zangu wanafanya UN New York wakanieleza kuwa ni matapeli. Walinieleza nitume information na evidance za mawasiliano kwenye UN Security office ili waweze kuwapata watu hawa.

Uki- visit UN websites zote upande wa Vacancies wanatoa onyo kwa waombaji wote, kuwa kuna institutions kama hizo za matapeli.

Kwa watu ambao wana upeo wa kuelewa ndiyo maana wana dought na COU na institutions hewa wanazotumia matapeli. Kwa hiyo ndugu yangu Mkandara tusichukulie kila kitu for granted mtandao upo tuutumie kufanya utafiti na kuelemishana.

Samahana kwa kuwa-boar.
 
Mwanasiasa,

Sintachoka kukufahamisha kuhusu issue hii. Na hapa nitakujibu ktk vipande viwili, kwanza nikianza na hilo la kuihusisha COU na Association of Commonwealth Universities (ACU). Mkshikaji hakuna sheria duniani inayomkataza mtu kutumia jina linaloambatana na neno Commonwealth. COU haihusiani kabisa na jumuiya hii ila wametumia jina hilo ktk kisajiri biashara yao. Ni sawa kabisa na miwani inayotengenezwa Ulaya kwa jina la Serengeti, huwezi kukuta kampuni hiyo imesajiriwa ama kufahamika Tanzania kwa sababu tu eti jina ni la Kitanzania. Kuna hata club za pombe zenye majina kama Zanzibar. Mimi nimekwisha fanya hivyo na kujikuta nimekwama kwani COU inatambulika na Kitengo cha Council for Education in the Commonwealth kama mwanachama, pia kuna uhusiano mdogo na kitengo cha Commonwealth Training Consultants ambacho kipo independent kwa kazi zake...

Kwa hiyo hata swala linaloihusu UN inabidi mtu ufahamu kitengo gani kinachoshughulikia swala fulani na sio kweli kwamba kila mfanyakazi wa juu UN atajua kila kitu ndani ya taasisi zake wala ushirikiano kati ya taasisi hizo na vyombo vingine. Anaweza kukupa sheria inayohusiana na swala zima.

Nakuomba pitia ukurasa huu utaona watu gani wanaohusika ama kushirikiana na COU ktk elimu na hao ndio wa kuwauliza. Mwenzako nimeisha fanya hivyo na nimekwama... napenda sana kumweka Nchimbi na huyo Kamala kitimoto lakini elimu ndugu yangu siku hizi haina upeo.

http://www.commopu.org/commopu.htm.

Swala la Pili kuhusu Maprofesa:-
Nimetumia neno mathalan kwa hiyo yote niliyoandika ni kwa MFANO..., Tanzania labda hadi leo hatuna Open University inayoendesha huduma hii kwa kupitia Mtandao. Nadhani ktk ukurasa niliokupa hapo juu kuna majina ya baadhi maprofesa (chini mwisho kabisa), pitia labda wanaweza kujibu swali lako.
 
Haya ndugu zangu. Aibu kubwa ndani ya CCM.

Wabunge wanahojiwa kwa kufoji vyeti vya Elimu.

Sasa huu ni wakati mwafaka wa kuwaanika wote wa aina hiyo.

Nakumbuka kuna ndugu mmoja aliwahi kutoa orodha ya wabunge
na vigogo wanaojiita madaktari(wana PhD). Naomba wamwagwe hapa kijiweni tuwashughulikie. Vidhibiti vikipatikana vitafikishwa kwa wahusika mara moja. Maana watu wa aina hii ni hatari sana. Hawana tofauti na majambazi wanaoua. Maana hawa wanatuua tukiwa bado tunatembea.

Ndiyo wakwanza kuingia mikataba feki, kama IPTL. SONGAS, bandarini,
n.k. Kwa taarifa kamili kuhusu aibu hii KUBWA soma: Kashfa ndani ya Bunge!

ALASIRI
2006-06-02 16:40:32
Na Simon Mhina, Jijini

http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2006/06/02/67655.html
 
kumekucha leo nimesikia katika redio, lakini wanasema imeandikwa kwenye gazeti la mwanchi kuwa wanaotakiwa kuhojiwa ni wengi hadi sasa wanayo majina 10.

Na wasema orodha ni kubwa na wanatakiwa kuongeza kasi ya kuwahoji kabala kikao kijacho tarehe 10/6/2006 cha bunge. Lakini majina yao hayajawekwa wazi. Wanapekekwa katika mtaa wa ohio na Ghana wakiwa kwenye tinted cars ili wasijulikane. watajulikana tu inawezekana ile orodha ndefu ya BCSTImes ikawa kweli.

Ngoja tusubiri!
 
Bandugu,

Kama kawaida yangu naangalia tena upande mwingine wa shilingi.
HAWA JAMAA HAWAKUFOJI VYETI. Vyeti wamepewa, sasa kama ni feki au la, nyinyi ndio muwaambie!!

Kwahiyo sakata hii itaishia hivi: Serikali inapenda kutoa tamko rasmi kuwa imewahoji wahusika na kugundua kuwa hawakuwa wanafahamu kuwa vyeti vitolewavyo na vyuo..a,b,c etc havitambuliwi kimataifa/kitaifa. Hivyo basi watuhumiwa wanatakiwa wasitumie vyeti hivyo na wengine walisoma kwenye vyuo hivyo waache mara moja kutumia vyeti hivyo.
Period!

Subirini

FD
 
Bandugu

Nasikia mkuu wa chuo(sijui vice au?) kikuu cha Mzumbe nae ana udakitari wa falsafa FEKI.

Jamani nani ana taarifa kamili kuhusu hili?

FD
 
Ninasikia pia kuna rais mmoja toka maziwa makuu naye na degree ya aina hiyo!

Soma hapa lakini bwana mnyika hajaweka jina la huyo rais. Ila mimi NINAKUBALIANA NAYE KUWA TAIFA LISIPOKUWA MAKINI! GIGO(GABBAGE IN GABBAGE OUT) INA MADHARA MAKUBWA! ni imani yangu safari hii viongozi hawatakuwa viziwi au vipofu kuhusu hili! kwa manufaa ya taifa la baadaye.
 
miye nasubiri nione ni panya gani huyo shujaa atakayekuwa tayari kumfunga paka kengele!! vingenevyo ni mazingaombwe...
 
Ama kweli nchi maskini maskini tu....

Tunapoteza muda na fedha za walipa kodi ati kutafuta WABUNGE wanaogushi vyeti?..Hivi Mbunge anatakiwa kuwa na cheti gani?... badala ya kuweka nguvu hiyo ktk kuwaangalia wataalam wetu ktk taasisi mbalimbali (hasa walimu) tumeweka kwa wabunge ambao huchaguliwa kwa kura za wananchi na sio vyeti vyao..... what a crap!

Ikiwa kuna mtu kati yenu ataweza kunipa list ya vyuo vyote vinavyotambulika Tanzania na sio list ya Mareakani ama Uingereza naweza kusikiliza. Hata hivyo kisheria list hiyo haimkatazi mtu kutundika cheti chake ukutani ama kutangulia jina lake. Hakuna kati yenu anayeweza kusema EN hakusoma kabisa kupitia internet na kupata shahada hiyo wala hakuna mtu anayeweza kusema NI lazima usome miaka mitano kupata shahada fulani.
KUGUSHI cheti ni kununua cheti bila mhusika kupata elimu ya cheti husika. Mengine yote hayahusiani na mtu yeyote isipokuwa mwajiri wa mtu huyo.....Mbunge hakuajiriwa na Sitta.

Dhumuni kubwa la kutambulika ama kutotambulika kwa cheti ni ktk kuweka utaratibu wa elimu unaokubalika nchini humo ktk kufungua biashara, ajira na wakati mwingine kuendelea kimasomo. Kila shule, tajiri na hadi nchi zina mapendekezo yake na hayafanani kabisa.

Prof. Sarungi pamoja na vyeti vyake hawezi kufanya kazi Marekani ama Canada kama daktari, kwa sababu vyeti vyake havitambuliki. Hii haina maana Prof. Sarungi kagushi vyeti, pia Hukohuko marekani ama canada hawana sheria ya kumtakataza Sarungi kutotanguliza Prof. mbele ya jina lake ktk hati ama sahihi anazoweka nchini Marekani. na magazeti yote yatampa cheo chake cha U professor ingawa haruhusiwi kufanya kazi kama Daktari nchini humo.

Huyu huyu Dr. sarungi anaweza kabisa kukubalika nchi nyingine na vyeti hivyo hivyo kwa kupata kazi ama kufungua biashara.

Ikiwa swala ni muda wa kuhitimu masomo, hili ni tatizo letu sisi, halihusiani kabisa na nafasi ya ubunge.

Tumeletewa wataalam kibao toka nje ambao ni feki, kazi zote kubwa zinafaywa na vijana wetu wanaolipwa robo ya misharaha ya wataalam hawa - hatusemi kitu. Wakenya na waganda kibao wana vyeti feki sehemu za uzalishaji hatusemi kitu, madawa toka india yote feki hatusemi kitu, chakula kinachoagizwa toka nje feki hatusemi kitu - ila tumekisia Mbunge fulani ana cheti feki (pale panapotukuna) basi nchi nzima imekuwa deal hali watu ndio wanazidi kufa kwa njaa umaskini na kila adha.
 
  • Thanks
Reactions: y-n
Mkandara ninakubaliana na wewe kuwa watalaam wengine pia wafuatiliwe!

Ila kusema wabunge ni kupoteza muda NA HELA ! hapo sikubaliani na wewe.

Hawa wabunge ndiyo wanaotunga sheria za nchi?

ndiyo wana kamati mbali mbali mfano mipango ya uchumi.

Na WAMO KATIKA kamati nyingi tu muhimu kwa nchi yetu tembelea website yao!!

wanatakiwa kuangalia mikataba ya nchi yetu nk!

wanapitisha bajeti ya kuendesha nchi!!!

Baada ya wao kufanya hayo maamuzi makubwa na mazito ya nchi NDIPO WATALAAM WENGINE WANAKUJA KUTEKELEZA!

KWA MTIZAMO WANGU MDOGO NINAKUPINGA! ILA INAONEKANA UMEINDIKA KWA UCHUNGU KIFALSAFA!
HAWA WANAOSOMEA PHD ZA KUNUNUA KWA MWAKA MOJA KWELI WATAMBULIKE DR? AU NI DEGREE ZA HESHIMA? PHD NI AT LEAST TWO YEARS FULL TIME NA MWENYE EXPERIENCE!
 
Back
Top Bottom