VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
1. Tutorial Assistant (TA)-Huyu niyule Mhadhiri wa chini kabisa ambaye yeye ana Shahada ya Awali tu kwenye fani yake.
2. Assistant Lecturer ( AL)-Huyu ana Shahada ya Uzamili(Masters) katika fani ake husika
3. Lecturer (L)-Huyu ana Shahada ya Uzamivu(PhD) Lakini,bado si mkongwe kwenye Shahada yake hiyo au bado hajaandika na kutafiti vya kutosha
4. Senior Lecturer (SL)- Huyu ana Shahada ya Uzamivu na ni wa muda mrefu kuliko L.Yeye angalau ameandika na kutafiti kwa kiasi fulani.
5. Associate Professor (AP)- Huyu ni mbobezi katika kufundisha kuliko SL. Yeye ameshafanya uandishi na utafiti wa kutosha katika fani yake kuliko SL.Naye ana Shahada ya Uzamivu.
6. Professor (P)-Huyu ni mbobezi katika kufundisha,kutafiti na kuandika katika fani yake kuliko AP. Ni cheo cha juu kabisa katika ngazi za Wahadhiri Vyuo vikuu.
NB: 1.Vyeo hivi hupandishwa na Mabaraza ya Vyuo kulingana na sifa walizojiwekea hasa za utafiti na uandishi wa vitabu,sura za vitabu nk.
2. Kitivo cha Sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,tangu kuanzishwa kwake 1961,kimebarikiwa kuwa na Maprofesa kamili (P) wanne ambao ni Prof. Issa Ghulamhussein Shivji, Prof. Gamaliel Mgongo-Fimbo,Prof. Chris Peter Maina na Prof. Josephat L. Kanywanyi. Prof. Shivji hafundishi tena.Waliobaki bado wapo wakifundisha kwa mikataba.
Asanteni kwa kunisikiliza...