Vyeo vya "Mkuu wa Nchi" na "Mkuu wa Serikali" vigawanywe kati ya Rais na Waziri Mkuu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Sasa hivi vyeo hivi vimewekwa kwa Rais. Yeye ndiye "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State" na vile vile yeye ndiye "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government". Kama mkuu wa nchi ndiye amiri jeshi jeshi mkuu, na ndiyo alama ya umoja wa serikali na alama ya nchi. Lakini kama Mkuu wa Serikali yeye ndiye anayeunda baraza la mawaziri na kuliwajibisha na vile vile ndiye mkuu wa serikali hiyo.

Waziri Mkuu wa Tanzania siyo Mkuu wa Nchi wala siyo Mkuu wa Serikali. Anashiriki kwenye kuunda baraza la mawaziri kwa kushauriana na RAis tu lakini rais ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kuundwa kwa baraza hiilo na baraza hilo haliwajibiki kwa Waziri Mkuu bali kwa rais. Waziri Mkuu ni kiongozi tu wa "shughuli za serikali" tena ni kiongozi wa shughuli hizo "Bungeni"! Nje ya bunge ni Rais ndiye mkuu wa shughuli hizo na anasaidiwa na rais na waziri mkuu.

Sasa tufanye vipi:

Rais abakie kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri jeshi mkuu -na apatikane katika uchaguzi wa kawaida. Atakuwa na madaraka mengine mengi tu yakigawanywa kati yake na Waziri Mkuu. kwa mfano, Rais anateua wale wenye kushika nafasi za kitaifa tu katika Mahakama, Majeshi, na Taasisi nyeti wakati Waziri Mkuu anateua watendaji wa civil service nyingine n.k

Waziri Mkuu awe Mkuu wa Serikali - achaguliwe na wabunge baada ya kupendekezwa na chama chake kilichoshinda uchaguzi wa rais). Akishaguliwa ndiye anaunda baraza la mawaziri na anapeleka majina yake kwa rais kwa kukubaliwa "approval" na rais apewe muda fulani - not more than 7 days - kukubali baraza hilo. Akilikataa mbunge mwingine anapewa nafasi ya ukwa waziri mkuu na kuunda baraza jingine. Akikubaliwa basi Baraza linatangazwa chini ya Waziri Mkuu na baraza hilo litakuwa likisimamiwa na kuongozwa na Waziri Mkuu huku WM akiwa na uamuzi wote juu ya baraza hilo ikiwemo kumfukuza Waziri au kumbadilisha Waziri. Waziri Mkuu akijuzulu, baraza linajiuzulu lakini rais anabakia kwa muda wote wa kipindi chake; rais akiondolewa au akiondoka kwa sababu yoyote Waziri Mkuu anabakia wakati makamu wa Rais anakuwa rais na chama chake kupendekeza jina la Makamu - kama ilivyo sasa.

Kwa kufanya hivyo - Waziri Mkuu atajiwabika kwa baraza aliloliunda yeye na Rais atawajibishwa kwa nafasi yake. Waziri Mkuu ataweza kuulizwa maswali kuhusu mawaziri akiwa na madaraka ya kuwawajibisha mawaziri wake au yeye mwenyewe kuondolewa.
 
Mzee Mwanakijiji.
Umeongea point tupu.
Tunachotakiwa hapa ni tufanye maandamano nchi zima, then tuitoe serikali ya ccm, then tufanye 'COPY AND PASTE' ya katiba ya KENYA, hapo utaona kitakachotokea...
 
Tujaalie kuwa Akiwa Rais, Yeye ndiye awe "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State". Na Waziri Mkuu awe ni "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government".Lakini Wabunge hawana imani na Waziri mkuu itakuwaje?
 
Sasa hivi ukiangalia kutokuwa na "imani na Waziri Mkuu" kuna maana gani wakati Waziri Mkuu haundi baraza la mawaziri,hawezi kumfukuza waziri wowote wala kumbadilisha, watumishi wote wa umma wako chini ya Katibu Mkuu kiongozi au moja kwa moja kwa rais, kitu pekee ambacho WM anaweza kufanya ni kumuambia Rais 'x, y, na z' nje ya hapo hana lolote - si umeona alivyopata shida kwenye sakata la Jairo na kwa Daktari. Kimsingi Pinda yuko sahihi!
 
Kwa hiyo yeye ni Waziri mkuu lakini kakalia Kuti Kavu? Waziri Mkuu jina tu hana uwezo wa kutowa uamuzi Wowote ule ndani ya Serikali? ndio maana Wabunge hawana imani nae. Itabidi Rais aachie uongozi mmoja kati ya hivyo vyeo 2 (Rais. Yeye ndiye "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State" na vile vile yeye ndiye "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government".) Rais amuachie Waziri Mkuu uongozi wa "Ukuu wa Serikali" yaani "Head of Government" ili Waziri Mkuu awe na power kwenye Bunge na Serikali .
 
Mfumo huu ulitengenezwa kwa makusudi; kuzuia Waziri Mkuu kumpiku Rais. Fikiria kama Lowassa angekuwa ni Waziri Mkuu mwenye nguvu za kuwa "mkuu wa serikali" unafikiri watu wangejali sana Kikwete anafanya nini?
 
Umezungumza point ndio maana Mheshimiwa Mzee E.Lowassa aliona mbali wakati wa uongozi wake wa

UWaziri Mkuu alipojiuzulu, Mzee E.Lowassa alifanya jambo la Ushujaa kujiuzulu uongozi.Tunataka Viongozi washupavu ndani ya Serikali yetu wawe mfano kama wa Aliyekuwa Waziri

Mkuu Mh,E.lowassa. Kwa Mawazo yangu Waziri Mkuu na wenzake wale Mawaziri 8 wajiuzulu ili kuiweka heshima ya

Serikali pamoja na Chama tawala ili Wananchi wawe na imani na viongozi wao. Waziri Mkuu awe ni mfano bora juu ya mawaziri 8 wenzake yeye ajiuzulu pamoja na wenzake pia Wajiuzulu ili kujenga imani ya Serikali na chama tawala kwa wananchi unasemaje mwenzangu.?
 
MM, Kama ni hivyo si afadhali ungeshauri tubadilishe kabisa our system of Government- Yaani from Presidential System kwenda kwenye Parliamentary system. Lakini kusema kwamba tuendelee tu na huu mfumo wa sasa, ila MADARAKA yaende kwa PM sidhani kama ni possible.

Kwa mfano, unasema kwamba Waziri Mkuu achaguliwe na wabunge. Hapa ni sawa, lakini je ni vipi atakuwa na power kumshinda RAISI ANAECHAGULIA NA WANANCHI WA NCHI NZIMA? Binafsi nadhani tutakuwa tunakaribisha mtafaruki mwingine wa madaraka ndani ya nchi ya WACHUMIA TUMBO.
 
PM akijihuzuru automatically baraza la mawaziri linavunjika mkuu. Ndiyo maana watu wanamlenga yeye kwa kuwa atapelekea kuvunjwa kwa baraza. Wanakomaa nae kwa ajili hiyo.
 
Ndio kitu wanachotaka Wabunge ili Rais aweze kuunda Baraza jipya la Mawaziri. Kwa sababu Mawiziri waliopo hawawezi kufanya kazi waliyopewa na Rais .

kipanya_07-_03_-_2012_20120307_1624138827.jpg
 
Kaka/Dada mleta mada.

Umesahau kuwa kuna watu (Mtikila alishapeleka kesi mahakamani na akashinda kuhusu hili) wanapigania kuwepo na wagombea Urais wasiokuwa na vyama vya siasa? Ikiwa Waziri Mkuu atachaguliwa na chama kilichoshinda kura za Urais, Jee ikiwa URais atashinda mgombea asie na chama? Fikiri.

Mamlaka ya Kuongoza nchi hayawi kama utakavyo wewe.

Amma Serikali iongozwe na Waziri Mkuu amma iongozwe na Rais. Mfano mzuri ni India na USA, demokrasia mbili kubwa duniani zenye mfumo tofauti wa uongozi, moja inaongozwa na Rais moja inaongozwa na Waziri Mkuu.

Afrika hayo yote hayatufai kabisa. Uongozi urudi kuwa wa kitemi. Na watemi ndio wachaguwe Mtemi Mkuu ndio awe kiongozi wa nchi kwa muda fulani. Kamanda Mbowe atafurahia hili kwani litatupeleka kwenye sera zake za kuendesha nchi kwa kanda.
 
Mfumo huu ulitengenezwa kwa makusudi; kuzuia Waziri Mkuu kumpiku Rais. Fikiria kama Lowassa angekuwa ni Waziri Mkuu mwenye nguvu za kuwa "mkuu wa serikali" unafikiri watu wangejali sana Kikwete anafanya nini?

Mhhhhhhh, nawe kama PASCO?
 
MM, Kama ni hivyo si afadhali ungeshauri tubadilishe kabisa our system of Government- Yaani from Presidential System kwenda kwenye Parliamentary system. Lakini kusema kwamba tuendelee tu na huu mfumo wa sasa, ila MADARAKA yaende kwa PM sidhani kama ni possible.

Kwa mfano, unasema kwamba Waziri Mkuu achaguliwe na wabunge. Hapa ni sawa, lakini je ni vipi atakuwa na power kumshinda RAISI ANAECHAGULIA NA WANANCHI WA NCHI NZIMA? Binafsi nadhani tutakuwa tunakaribisha mtafaruki mwingine wa madaraka ndani ya nchi ya WACHUMIA TUMBO.
agreed. Tubadilishe Katiba (sheria), tubadilishe sera na kanuni kisha tutakuwa tumebadili mfuno wa serikali na uongozi
 
Sasa hivi vyeo hivi vimewekwa kwa Rais. Yeye ndiye "Mkuu wa nchi" yaani "Head of State" na vile vile yeye ndiye "Mkuu wa Serikali" yaani "Head of Government". Kama mkuu wa nchi ndiye amiri jeshi jeshi mkuu, na ndiyo alama ya umoja wa serikali na alama ya nchi. Lakini kama Mkuu wa Serikali yeye ndiye anayeunda baraza la mawaziri na kuliwajibisha na vile vile ndiye mkuu wa serikali hiyo.

Waziri Mkuu wa Tanzania siyo Mkuu wa Nchi wala siyo Mkuu wa Serikali. Anashiriki kwenye kuunda baraza la mawaziri kwa kushauriana na RAis tu lakini rais ndiye mwenye uamuzi wa mwisho wa kuundwa kwa baraza hiilo na baraza hilo haliwajibiki kwa Waziri Mkuu bali kwa rais. Waziri Mkuu ni kiongozi tu wa "shughuli za serikali" tena ni kiongozi wa shughuli hizo "Bungeni"! Nje ya bunge ni Rais ndiye mkuu wa shughuli hizo na anasaidiwa na rais na waziri mkuu.

Sasa tufanye vipi:

Rais abakie kuwa Mkuu wa Nchi na Amiri jeshi mkuu -na apatikane katika uchaguzi wa kawaida. Atakuwa na madaraka mengine mengi tu yakigawanywa kati yake na Waziri Mkuu. kwa mfano, Rais anateua wale wenye kushika nafasi za kitaifa tu katika Mahakama, Majeshi, na Taasisi nyeti wakati Waziri Mkuu anateua watendaji wa civil service nyingine n.k

Waziri Mkuu awe Mkuu wa Serikali - achaguliwe na wabunge baada ya kupendekezwa na chama chake kilichoshinda uchaguzi wa rais). Akishaguliwa ndiye anaunda baraza la mawaziri na anapeleka majina yake kwa rais kwa kukubaliwa "approval" na rais apewe muda fulani - not more than 7 days - kukubali baraza hilo. Akilikataa mbunge mwingine anapewa nafasi ya ukwa waziri mkuu na kuunda baraza jingine. Akikubaliwa basi Baraza linatangazwa chini ya Waziri Mkuu na baraza hilo litakuwa likisimamiwa na kuongozwa na Waziri Mkuu huku WM akiwa na uamuzi wote juu ya baraza hilo ikiwemo kumfukuza Waziri au kumbadilisha Waziri. Waziri Mkuu akijuzulu, baraza linajiuzulu lakini rais anabakia kwa muda wote wa kipindi chake; rais akiondolewa au akiondoka kwa sababu yoyote Waziri Mkuu anabakia wakati makamu wa Rais anakuwa rais na chama chake kupendekeza jina la Makamu - kama ilivyo sasa.

Kwa kufanya hivyo - Waziri Mkuu atajiwabika kwa baraza aliloliunda yeye na Rais atawajibishwa kwa nafasi yake. Waziri Mkuu ataweza kuulizwa maswali kuhusu mawaziri akiwa na madaraka ya kuwawajibisha mawaziri wake au yeye mwenyewe kuondolewa.

Food for thought!

thanks!
 
Mawazo mazuri sana! Ila nina tatizo pale uliposema waziri mkuu atokane na chama ambacho ametoka rais. Nadhani better practise ni waziri mkuu atokane na chama chenye wabunge wengi; au aliances ambayo itafanya kuwa na wabunge wengi.
 
Back
Top Bottom