Vyandarua vyenye dawa

idea

Senior Member
Apr 3, 2009
123
16
Nasikia dawa inayowekwa kwenye vyandarua ni DDT. Je hii dawa haiwezi kutumika kuua mbu wote wanaoeneza Malaria? Kuna agenda yoyote ya siri ya kushindwa kutokomeza Malaria? Tafadhali tujadili hili!
 
Nasikia dawa inayowekwa kwenye vyandarua ni DDT. Je hii dawa haiwezi kutumika kuua mbu wote wanaoeneza Malaria? Kuna agenda yoyote ya siri ya kushindwa kutokomeza Malaria? Tafadhali tujadili hili!


Agenda ya siri ipo, na ni wewe mimi na mitanzania mingine yooote yenye vichwa ngumu!! Hebu zunguka nyuma ya nyumba yako, kuna madimbwi mangapi ya maji? Vichaka je...? Je uliwahi kufanya jitihada zozote kuharibu mazalia ya mbu? Au ndo kina wale tunakaa tunalalamika oooh serikali imeshindwa kutokomeza malaria... jiulize umefanya nini katika vita hii? Kama ni elimu imeshatolewa vya kutosha nadhani ni watanzania wachache sana wasiojua malaria inaambukizwa vp, na jinsi ya kujikinga, lakini hakuna anayejali kuchukua initiatives!!! Wacha ituue an izidi kuwatajirisha wenye kutunga sera!! (by the way, unajua kuwa malaria ndo inaingiza mishiko kwenye hospitali za private??) Teeeh teeeh teeh!! Mitanzania ndivyo tulivyo!!
 
Nasikia dawa inayowekwa kwenye vyandarua ni DDT. Je hii dawa haiwezi kutumika kuua mbu wote wanaoeneza Malaria? Kuna agenda yoyote ya siri ya kushindwa kutokomeza Malaria? Tafadhali tujadili hili!

DDT haitumiki kwenye vyandarua, hakuna agenda ya siri ni hela na uamuzi tu, Zanzibar wamefanya spraying ya nyumba karibia malaria imetokomea.
 
How can someone dare to say Mitanzania? Inaonekana wewe umekata tamaa jamani! But what I know is possible to eradicate Malaria. Juhudi za kuspray nyumba Zanzibar ni za serikali au ni watu binafsi? Pamoja na kwamba ubepari ndio unaotawala dunia kwa sasa, tusiwe wajinga kiasi cha kuachia tu watu wachache watajirike na kutuua hakina sisi na wewe. Angalia ni dawa ngapi fake za malaria ziko mitaani? Pole wewe mwenye kiosk chako mtaani eti ni hospitali. Hii juhudi ya kutokomeza malaria naanzisha mimi kuanzia leo.
 
Tunashindwa kutokomeza malaria kwa kukosa right strategies na right means. Tunawategemea wazungu waje na misaada na strategies zao. Kama uchumi wetu unategemea kilimo, halafu bajeti ya kilimo ni issue bila misaada, itakuwa hela ya elimu kuzuia malaria. Nilibahatika kuwemo kwenye msafara wa Roll Back Malaria toka Cape Town mpaka Cairo Misri, ulikuwa ni ulaji tuu wa pesa ambazo zingetosha kutokomeza Malaria nchini za Afrika Mashariki.

Zanzibar wanakaribia kutokana na udogo wake na kuzungukwa na bahari ambayo siyo mazalia ya mbu na tabia nchi ukijumlisha na iliyojaa permiable rocks ni aghlabu sana kukuta madibwa kwenye maeneo ya udongo wa kichanga.

Pamoja na vita yote dhidi ya matumizi ya DDT, kwa vile inasumu, ila ni kiboko!. Madawa mengi ya kuuwa wadudu yanasumu, waulize Wasukuma kuhusu dawa ya pamba ya Thiodan, ni kizunguzungu, DDT afadhali.

Madawa mengi ya malaria yana maisha mafupi kabla wadudu hawajayazoea na kugeuka sugu, hivyo pamoja na kukosekana kwa kiwango cha dose stahiki ya Muarobaini (Cinchona Tree), ndiyo hutumika viwandani kutengeneza Quinine, hivyo ni kiboko ya malaria.

Na kuhusu vyandarua vya dawa, nashauri uvifue kabla ya kutumia, kuna wakati watoto wenye sensetive skin wanawashwa na kupata vipele fulani kwenye ngozi zao kutokana na sumu ya vyandarua, na pia usishangae watoto kupata vikohozi vya ajabu mara tuu baada ya kufunga chandarua kipya chenye dawa ya miaka mitano!.
 
Je mimi na wewe can we design strategies to eradicate malaria? I am ready to devote myself and do this for the sake our country. Hii shughuli inahitaji support kuanzia ngazi ya familia hadi kimataifa. Kutokana na kwamba una uzoefu kuhusu hili jambo ningependa tuanzishe hii movement. I am sure tutafanikiwa.
 
Back
Top Bottom