Vyandarua vya bure!

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Kuna tetesi kuwa vyandarua vya bure vinavyotolewa kwa akina mama kule kliniki huwa havitoshi kwenye vitanda,familia nyingi za kibongo huwa wanalala na mtoto hivyo chandarua hakiwatoshi.
Je wahusika wanalitambua hili?
WanaJF wenye uelewa wa mambo ya kinga za malaria mnasemaje?

NAWASILISHA...
 
hali hii imepelekea mpaka wamama wanachukua net hizo na kuwatunzia vifaranga kwa malengo ya kuwazuia mwewe wasichukue vifaranga kwakuwa vifaranga hupewa chakula wakiwa ndani ya neti. Hii ni kweli na ya uhakika!
 
Unajua haya amabo mengine tuliwa bila kujijua. wameshafanyaga research kujua ni watanzania ngapi wanavitanda?
na ni vya aina/ukubwa gani?
na wanolalia mikeka ni wangapi?
kua nakitanda peke yake haitoshi inapaswa kujua idadi ya watu wanaolala kwa pamoja. maana essence ya bednet iskuguse ukiwa umelala. kama ni mizungu wanne mmjazana neti haina maana.
ukiangalia sana hii stori ya neti ni kiini macho
 
Tabora watumia vyandarua hivi kwa kufugia vifarang vya kuku.sababu walizotoa ni pamoja na vyandarua hivi havitoshi vitandani.wahusika walifanyie kazi suala hili.
 
Back
Top Bottom