Vyama vyaanza kunyemelea Arumeru Mashariki

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Vyama vya upinzani vimejiandaa kukikabili Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha ambapo vimetuma wanachama na viongozi wao kwenda kufanya kufanya utafiti kuhusu hali ya kisiasa ilivyo kabla ya kutangaza kuweka wagombea wao.Uchaguzi katika jimbo hilo unafanyika kufuatia aliyekuwa mbunge wake, Jeremiah Sumari (CCM) kufariki dunia. Kampeni zitaanza Machi 9, mwaka huu na kufuatiwa na uchaguzi Aprili Mosi, mwaka huu.Naibu Katibu Mkuu wa CUF,Julias Mtatiro, alisema chama chake kimetuma watu kupeleleza jimboni humo na baada ya hapo itatolewa taarifa rasmi ya chama kuhusu msimamo.“Chama kitatoa tamko rasmi kuhusu msimamo wa chama na Jumapili wiki hii, lakini kwa sasa wapo watu tumewatuma wanafanya tathmini jimboni humo kuangalia hali ilivyo,” alisema Mtatiro.Mwenyekiti wa TLP, Agustino Mrema, alisema chama chake kitasimamisha mgombea katika jimbo hilo kwa sababu kina historia nzuri katika jimbo la Arumeru Mashariki. Alisema histori nzuri ya chama hicho inatokana na kufanikiwa kusuluhisha mgogoro mkubwa baada ya watu walichoma moto Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), nyumba na watu kadhaa kuuawa.Katibu wake Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza, alisema chama kimetuma watu ambao wamekwenda jimbo humo kuangalia hali ilivyo kabla ya kutoa uamuzi wa mwisho wa kuweka mgombea wao kuchuana na wagombea wa vyama vingine.Mkurugenzi wa Habari wa Chadema, John Mnyika, alisema chame chake kitatoa taarifa rasmi leo kuhusu ushiriki wake kuhusu uchaguzi huo.CHANZO: NIPASHE
 
Chama cha kijamii vp?..INAIDI KIENDE NACHO KIKAONESHE UWEZO WAKE WA KUNADI SERA.
 
Back
Top Bottom