Vyama vya upinzani vyakubali uamuzi wa Mbowe

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
[FONT=ArialMT, sans-serif]Vyama vya TLP, CUF,NCCR-Mageuzi na UDP vimesema kuwa Kiongozi wa Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, amezingatia kanuni kwa kuunda “Baraza la Mawaziri Kivuli kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) peke yake.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Juzi Mbowe alilitangaza baraza hilo bungeni likiwa na wizara 26, akisema kuwa alifanya hivyo kwa ajili ya kutekeleza kwa vitendo azma yao ya kuwa na serikali ndogo.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuwa ameteua wasemaji wakuu wa wizara hizo kutoka Chadema peke yake kwa kuwa vyama vinavyounda kambi hiyo havijafikia maridhiano na kuahidi kuwa atavishirikisha baada ya kufikia maridhiano.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, akizungumza na NIPASHE jana kuhusiana na uamuzi wa Mbowe, alisema :[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Siwezi kuwalaumu, ni haki yao kikanuni kwa kuwa wametimiza kigezo cha kuwa na wabunge zaidi ya asilimia 12.5.“Nawaachia kama wataona umuhimu wa kunishirikisha nawakaribisha,” alisema Mrema na kuahidi kutoa ushirikiano kwa baraza hilo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, alisema kazi yake nzuri anayoifanya Vunjo, ikiwemo ya kupambana na maovu kama biashara ya gongo, Chadema kingetambua mchango huo na kumshirikisha.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema kuwa kutokana na uzoefu wa kuwa mchapakazi hadi kuteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi katika miaka ya tisini, alistahili kuteuliwa bila kujali kuwa chama chake kina mbunge mmoja.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Bariadi Mashariki, John Cheyo, alisema kuwa walichofanya Chadema ni sahihi kwa sababu kanuni zinawaruhusu kufanya hivyo.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Kanuni zinawaruhusu na tunawatakia kila la heri,” alisema Cheyo kwa kifupi alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusiana na uamuzi wa Mbowe.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alipoulizwa kama atakuwa tayari kushirikiana na wasemaji wakuu wa kambi hiyo kutoka Chadema, alisema kwa kifupi: “Hatutawanyima ushirikiano.”[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alipoulizwa kama atakubali kama Mbowe atamteua baadaye katika baraza hilo, alisema:”Why not (kwa nini nisikubali).”[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Gando, Suleiman Khalifa Suleiman (CUF), alisema kwa mujibu wa kanuni, Mbowe alikuwa sahihi na kwamba wasemaji aliowateua wana uwezo.[/FONT]
“[FONT=ArialMT, sans-serif]Nina imani watafanyakazi vizuri na ndio msingi wa Baraza Kivuli. Sisi tutajaribu kuwasaidia kuchangia michango kwa hoja zao,” alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Khalifa alisema kuwa ikiwa Mbowe ataona uwezekano wa kujumuisha wabunge wa vyama vingine huko mbele hakuna tatizo.[/FONT]

[FONT=ArialMT, sans-serif]Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alisema kuwa Mbowe alifanya uamuzi kwa mujibu wa kanuni.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Hata hivyo, alisema kuna mtazamo wa kibunge na kikanuni. “Kimtazamo wa kikanuni yuko sahihi kwa kuwa zinampa mamalaka hayo. Lakini kwa mtazamo wa uongozi, uamuzi huo una mushkeli kwa kuwa zinamfanya kuonekana kama kiongozi wa kambi ya Chadema zaidi kuliko kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni,” alisema Kafulila.[/FONT]
CHANZO: NIPASHE

"...kwa mtazamo wa uongozi, uamuzi huo una mushkeli kwa kuwa zinamfanya kuonekana kama kiongozi wa kambi ya Chadema zaidi kuliko kuwa Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni
 
Tangu mwanzo tatizo halikuwa juu ya mawaziri kivuli bali kamati zinazothibiti ulaji serikalini na kwenye mashirika ya umma. Wakubwa serikalini walikuwa wakihofia kwamba bila kuidhibiti CDM uenda kamati ya usimamizi wa fedha za serikali ikahangukia mtu ambaye itakuwa vigumu kumuweka mfukoni. Na hiyo ingelizua balaa.
 
Mbinafsi tu nami nilifahamu hawezi kuwashirikisha from day one..

Tunashukuru anavyofanya ili kila chama kijitegemee siyo kusubuiri chakula mezani period!.
 
Vikubali au visikubali ni Haki ya Chadema....
This people are turning a non issue into an issue...
 
Waanze kwa kushughulikia mil 90 wanazopeana kama kunyamazishana,CDM ni chama changu lakin watanichafulia khali ahewa kama hatasema lolote kuhusu huo mlungula.Si haki kutembelea gari ya thamani hiyo wakati nyumbani wanatumia taa za chinli na koroboi wananchi wao kutokana na mgao wa umeme.
 
Mtizamo kwa wananchi wengi na kwa kuzingatia misingi ya chadema ya kuboresha maisha ya watz ni bora wachukue hizo mil 90 na kwa ambao hawana magari basi sio vibay wakatafuta magari ya gharama za kawaida na yenye hadhi yao ni fedha zitakazo baki basi zikatumike katika majimbo yao kwa miradi mbalimbali ya kusaidia maendeleo ya wananchi wao.

Hivi vyama vingine hawana la kusema kwa sababu CDM wametumia haki yao ya kikatiba na kanuni za bunge.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom