Vyama vya upinzani: Unganeni kama mnataka kuing'oa CCM

m_kishuri

JF-Expert Member
Jan 27, 2010
1,484
372



Kwa mujibu wa the Wikipedia:
A political party is a political organization that typically seeks to attain and maintain political power within government, usually by participating in electoral campaigns, educational outreach or protest actions.

Kama vyama vya kisiasa vya Tanzania vinataka kushinda au kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni, basi inawabidi waungane. La sivyo uwezekano wa kuing'oa CCM madarakani ni mdogo. Mifano ipo mingi sana katika bara la Afrika na kwingineko, ambako vyama vikongwe vimeweza kuangushwa tu baada ya upinzani kuungana.

Wondwosen Teshome (2009) anaandika,
"So far in Africa, opposition parties are rarely successful in
ousting the incumbents in elections largely due to their
fragmentation and their failure to form opposition coalitions."

 
Last edited by a moderator:
CHADEMA & CUF........That will never happen in our planet TANZANIA!
 
Kwa vyama kama tlp, udp, upnp kusimaisha mrais si uzandiki? Bado cuf na chadema inaweza kuwezekana
 
Ubinafsi umetawala kwenye vyama vya upinzani, tusitegemee kuona muungano wowote
kutoka kwao kwa miaka hii ya karibuni. Labda kwa kizazi kijacho.
 
viungane kwa kutumia sheria ipi, mimi nafikiri ungesema vishirikiane, kuunganisha vyama haiwezekani hapa TZ, haiwezekani hasilani.
 
Ooohh, inaonekana hujui kwamba siasa = ulaji + ubinafsi, kama kungekuwa na nia ya dhati ya kulitumikia taifa kusingekuwa na kuzibiana, na hata vyama vya siasa visingekuwa na sababu ya kuwepo. CCM na watoto wake, wote wasingakuwepo.
 
Ubinafsi umetawala kwenye vyama vya upinzani, tusitegemee kuona muungano wowote
kutoka kwao kwa miaka hii ya karibuni. Labda kwa kizazi kijacho.
Kwa misingi hiyo wataendelea kuwa vyama vya upinzani daima bila kuleta mafanyikio yoyote kwa wananchi.
 
Ubinafsi umetawala kwenye vyama vya upinzani, tusitegemee kuona muungano wowote
kutoka kwao kwa miaka hii ya karibuni. Labda kwa kizazi kijacho.

Hii ni hasara kwa walala hoi endapo kila the so called (WANASIASA) wanafikia matumbo yao tu. :hungry:
 
Kwa misingi hiyo wataendelea kuwa vyama vya upinzani daima bila kuleta mafanyikio yoyote kwa wananchi.

Wana ccm nao kwa unafiki,

Umetoa ushauri na kisha unatoa hitimisho

Peleka unafiki wako huko Lumumba.... mafisadi bana hamjambo
 
Editha Majura

WAZIRI Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, ameshauri vyama vya siasa nchini viungane ili viwe na nguvu itakayoleta ushindani wa kisiasa wa kutosha kufikia wananchi wa kada zote. Warioba aliyazungumza hayo jana wakati akizungumzia uchaguzi uliomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita nchini.

Alisema uamuzi wa kuwa na mfumo wa vyama vingi haukulenga kuweka utitiri wa vyama bali vyama zaidi ya kimoja vyenye uwezo wa kuwafikia wananchi wengi zaidi.

"Viongozi wa vyama vya siasa waangalie uwezekano wa kuungana bila kujali ni chama tawala au pinzani cha msingi ni kupitia sera zao na kujadili namna wanavyoweza kuungana na kujenga vyama vichache lakini vyenye nguvu kisiasa na uwezo wa kuwafikia wananchi wengi," Warioba alieleza.

Hata hivyo, alisema hatua iliyofikiwa na vyama vya upinzani ya kupata viti vya ubunge kwenye majimbo mengi zaidi kwenye mikoa tofauti, ni ishara kwamba taifa linaelekea kwenye siasa ya kidemokrasia kwa sababu vitajiongezea uwezo kisiasa na kiuchumi.

"CCM ilijengwa katika misingi ya jamii kuanzia nyumba kumi kumi ,hilo limeanza kutekelezwa na vyama vya upinzani ambavyo mwaka huu vimepata wabunge mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Kagera, Arusha, Kilimanjaro, Dar es Salaam, Iringa, Mbeya.., inamaanisha vitajiongezea uwezo wa kifedha hali itakayoongeza ushindani wa kidemokrasia," alisema.

Madai kwamba wazee CCM walimtelekeza mgombea wao wa urais, Jakaya Kikwete, wakati wa kampeni Warioba aliyaelezea kuwa ni ya kisiasa kwa sababu wasingeweza kuongozana naye kila mahala bali walitekeleza majukumu yao kwa namna na nyakati sitahili huku vijana wakienda sambamba na mgombea huyo. Aliwaasa wanaopata uongozi kutambua kuwa ni dhamana ambayo kila mwenye sifa anastahili.

Alikemea tabia ya baadhi ya viongozi ambao wakipata madarakani wanadhani hakuna anayestahili zaidi yao na ikitokea mwingine kugombea wadhifa huo wanamuona kuwa amewaingilia. Waziri huyo mstaafu alipongeza hatua ya utulivu na amani iliyozingatiwa visiwani Zanzibar kipindi chote cha uchaguzi kwamba ni tukio la kihistoria kwa visiwa hivyo kuwa na uchaguzi wa aina hiyo huku matokeo yakitangazwa mbele ya vyama vyote vya kisiasa na kufuatiwa na hotuba zenye kuashiria umoja wa kitaifa.

Ingawa uongozi wa umoja wa kitaifa visiwani humo unatarajiwa kukabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ya tofauti za sera za vyama husika na matatizo ya muungano, Warioba alisema kwa mshikamano uliyoonekana wakati wa uchaguzi ni dhahiri kwamba changamoto hizo zitadhibitiwa.

"Tofauti ya sera za vyama hivyo, siyo kubwa sana naamini zitawekwa sawa. Matatizo ya muungano awali yalikuwa kati ya Bara na Visiwani lakini baadaye yakachukua sura ya kisiasa na kuwa ya CCM na CUF jambo ambalo baada ya vyama hivyo kuonyesha mshikamano, matatizo hayo yatakwisha kwa sababu kiini cha muungano ni kikubwa kuliko cha matatizo hayo," alisema Warioba.



SOURCE: Warioba ashauri vyama vya upinzani viungane
 
Wananchi wengi wanapenda mageuzi…!!, wananchi wengi wameshachoka…!! Kinachozuia Mageuzi ni mbinu chache tu.

Baadhi ya mbinu zinazotumiwa sasa tumezisikia:-

  • Kununua shahada (lakini hili kama kuna fomu za kujaza kama umepoteza shahada) basi mtu anaweza kuuza shahada yake na bado siku ya siku akapiga kura, kwa kusema kwamba shahada yangu imepotea.
  • Mbinu nyingine ni propaganda ambazo wamebatiza kila Chama kuanzia Dini, fujo mpaka Ukabila. Utaona dawa ya hii propaganda ni kwamba wapinzani wote wakiungana hii itakuwa diluted. Na wakiungana na kusimama kama Chama kimoja kwenye Uchaguzi 2015, CCM watakuwa hawana pa kukimbilia na propaganda za sasa hazitafanya kazi.
Kila Chama kina vichwa na wanamageuzi wa kutosha ifike wakati wote waone kwamba kutengana na kuendelea kugawana kura na kupata ruzuku za hapa na pale haitoshi, inabidi kuweka nchi mbele na kuiangusha CCM na kutaifisha mali zetu, (viwanja vya mipira majengo n.k., na kufuta makada wao wanaofuja pesa zetu ambao ni wakuu wa wilaya n.k.); Just imagine wote wasimamishe mgombe Urais mmoja na wengine kina Lipumba Mtikila et al wote wakasimama kwa kugombea Ubunge...

Kama bado wapinzani watataka kutengana basi watatengana baadae baada ya kumuondoa CCM yaani uchaguzi wa 2025 (baada ya kufanya shughuli pevu ya miaka 10)
 
hakuna hata haja ya kuungana, chadema inakubalika, wengine ni wanafiki wakubwa watatutia aibu tu huko mbele.
 
Vyama vya upinzani vikitaka kuungana viungane lakini chama makini kama CDM wasishiriki kwani karibu vyama vyote vya upinzani ni wanafiki. Hawapo kwa maslahi ya nchi na kuna mifano mingi. CUF tayari wana ndoa na CCM ni sehemu ya serikali Z'bar; sijui kama inawezekana mwanamke mmoja kufunga ndoa na waume wawili. Vyama cha NCCR na vingine vyenye wabunge wana kambi yao ndogo ya upinzani na walikataa kuunga mkono CDM bungeni hata kwa masuala ya msingi yenye maslahi kwa wananchi kama vile kufuta 'sitting allowance'. Tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, CCM imekuwa na vyama pandikizi na pia kutumia mamluki ndani ya vyama pinzani vyenye nguvu. Vyama vya upinzani vinaweza vikaungana vyote kwa nia nzuri tu, lakini ikitokea KWA MFANO uchaguzi mkuu wa 2015 vikaamua kususia uchaguzi mpaka katiba mpya ipatikane, CCM inaweza ikatumia mbinu kikasajiliwa chama kipya kwa haraka haraka ali mradi kikubali kuingia kwenye uchaguzi. Uchaguzi unaweza kufanyika kwa sababu masharti ya kufanyika uchaguzi katika mfumo wa vyama vingi yamekidhi haja. Hii iliwahi kutokea Zanzibar ambapo chama cha PPT cha Dr. Che-Mponda kilianzishwa na kusajiliwa kwa muda mfupi, CUF kilipotishia kususia uchaguzi kutokana na rafu za CCM. Chama hicho kwa sasa kipo kwenye usingizi wa milele kwa sababu malengo ya kusajiliwa kwake yalitimia. CDM ni chama makini wanayafahamu hayo, janja nyani kula mahindi bichi.
 
Upinzani ni wakati wa kuungana n kuwa na chama kimoja au viwili imara. Wekeni plan hasa kwa vijana, uchumi wa mtaji na elimu ya kisasa ya technology. Zitto, Mboe, Mbatia, Seif ukiungana na kuweka katiba imara ya chama bila kujali ubinafisi na ego mtasaidia nchi. Hii ni demokrasia kukua hata US, Kenya, Canada n.k walikuwa na vyama vingi lakini vinapungua na muda unavyoenda.
 
Back
Top Bottom