Vyama vya upinzani Tanzania vijisahihishe kwanza vyenyewe

Mashibes

Member
Aug 28, 2016
24
18
Ni wakati muafaka sasa vyama vyetu vya siasa vinavyojiita ni vya upinzani vijipime kama vinatosha kua vyama vya upinzani ama ni upinzani uchwara?

Vyama hivi ambavyo ndani yake haviishi migogoro na misukosuko,ambayo inaashiria ukandamizwaji na uminywaji wa demokrasia ndani yake leo vinatuaminisha utawala uliopo ni wa kidikteta..

Nani hakumbuki sakata la Zitto alivyodhubutu kutangaza kugombea urais kupitia chama chake cha Chadema,na baadae anatafutiwa zengwe na kufukuzwa chamani,leo hata yeye mwenyewe ameusahau Udikteta aliofanyiwa enzi zile na anaunga mkono harakati za Chadema kutuaminisha Magufuli ni Dikteta.

Nani hakumbuki kilichomkuta Dr. Slaa, au nani hakumbuki upinzani wa Dr. Slaa, ulikua ni upinzani imara wenye masilahi mapana kwa taifa letu,lakini Dr. Slaa alivopinga kuja kwa Lowassa chamani akaambiwa ni bora yeye aondoke ili Lowassa apate nafasi.

Chama kinaendeshwa na maamzi ya mtu mmoja mbona sisi wanachama hatukushirishwa kwenye mchakato wa kumpokea Lowassa ama kumkataa, na sisi ni wanachama? Si kweli kwamba kila mwanachama wa chadema alifurahishwa na kitendo hicho, chama kinaongozwa kama familia yenye mfumo dume.

Nani pia hakumbuki jinsi mchakato wa kumpata katibu mkuu wa sasa wa chama chetu?,mchakato uligubikww na mizengwe kibao,ilimradi tu mwenyekiti anaamua nani akae kwenye nafasi hiyo, na kwa nn mwenyekiti kang'ang'ania madaraka? Chama hakina utamaduni wa kuachiana uongozi?..hayo yote na mengine yanaonesha wazi upinzani wa Chadema ni Upinzani Uchwara, M/kiti anakanyaga katiba ya chama hivi leo akiingia ikulu atashindwa kukanyaga katiba ya nchi?

Nani hakumbuki kua hichi chama ndo chama kilichoanzisha vuguvugu la ufisadi pale bungeni miaka kadhaa iliyopita na waziwazi wakatuaminisha kua Lowassa ni mtuhumiwa namba moja wa Ufisadi,leo wanakuja na ngojera za kutuaminisha Lowassa ni mtukufu kwa kua wamekalia hizo nyaraka za ushahidi...hivi hapa napo panahitaji usomi kiasi gani kujua hawa ni wapinzani uchwara? Maana sio Slaa,sio Tundu Lissu, sio Peter Msigwa, sio Mnyika,na wala si Mbowe wote walimtuhumu Lowassa.

Kwa majirani zetu na penyewe kumenuka,Lipumba alijiuzuru tena kwa mbwembwe, kwa kuitisha press leo anatangaza yeye ndo mwenyekiti halali wa chama,kwani hivi vyama havina katiba? Sasa kama nyie wenyewe ni madikteta kwenye vyama vyenu, huo mnaotuaminisha ni udikteta uchwara mtaweza kupambana nao?

Ifike pahala watanzania tuamue kutokuwaunga mkono nyie upinzani uchwara, kama miaka kadhaa mlituaminisha kua Tanzania inahitaji rais mwenye maamuzi,rais asie chekacheka mwenye kusimama hadharani na kukemea ufisadi na ubadhairifu wa mali za umma, Mungu si kiziwi kasikia maombi yenu katupa kiongozi ambaye leo tuna sababu lukuki za kujivunia,kiongozi ambaye hajamaliza hata mwaka lakini tayari tumeshaona dira na mwelekeo wa wapi tunaenda.

Cha ajabu kila anachokifanya kizuri kwa watanzania nyie kwenu ni kuponda tu, hivi ni kweli hamuoni,Majipu yaliyotumbuliwa,hamuoni elimu bure?,hamuoni pesa zilizookolewa kupitia watumishi hewa?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kudhibiti ukusanyaji kodi?,hamuoni pesa zilizookolewa kwa kufutwa kwa maazimisho ya siku kuu za uhuru na muungano?,hamuoni ni sh ngapi zimeokolewa kwa kuzuia safari za nje?,hamuoni hata jitihada za serikali kubadili mfumo wa elimu ambao ulikia umechakaa?,hamuoni hata madawati? Mnachoona ni Udikteta uchwara..

Hivi ukuta utatumia sh ngapi? Kwa nini hiyo bajeti msiielekeze kutatua kero za wananchi kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na serikali? Kama kweli mna uchungu na sisi(watanzani) leo hii huu ukuta unamfaishaje mkulima,mama ntilie?mwanafunzi?wazee?,na watanzania wa kawaida hata wafanyabiashara,....lakini huo mnaouita udikteta uchwara ukimuuliza mtanzania wa kawaida atakuambia amepata elimu bure,shirika la ndege limefufuliwa,bomba la mafuta kutoka Uganda linajengwa ambalo litareta ajira na kukuza uchumi,reli itajengwa ndani ya miaka mitatu,elimu bure nk..
 
Neno Democracy linahubiriwa kwa nguvu nyingi na baadhi ya vyama vya siasa nchini Tanzania mpaka kutishia usalama wa taifa kwa matamko mbali mbali ya VIONGOZI, hasa wa CHADEMA.

lakini ukivichunguza vyama hivyo ndani ya uendeshaji wake havifuati democracy hata kidogo.
Navishauri kabla ya kutoka hadharani na kudai democracy vijiendeshe ki democracy.

Mifano ni mingi Sina haja ya kuitaja jinsi vinavyoendeshwa kwa maslahi ya wachache na wanachama Kua ni stamp rubber tu.
"Charity begins at home "
 
Ipo Hivii...., Ukitaka kujua set up ya vyama vya upinzani hapa afrika rejea vyema vya UKOMBOZI miaka ya kuanzia 1950's na 1960's, hakuna tofaut yoyote! kwahyo tuambie kwanza kwann Baba Wa Taifa amedumu km rais wa TANU na mwenyekt wa ccm kwa almost miaka 40?? Watu munaongea tuu, mziki wa upinzani afrika sio kila mtu anaweza kuucheza, jasiri anayejitokeza kupambana na vyama dola acheni tu aliendeleze mpaka siku uwanja ukikaa sawa!! ww unaejiita et mwanamageuzi, nikuulize tu ushawahi kukaa lockup japo lisaaa?? hovyo kabisa wewe
 
Wenye ulta uzi kutoka hama kuu wanataka wale ambao ni jasiri na wana uwezo kifedha kama Mbowe na Lowassa waondoke ili CHADEMA ife. Ndiyo nia yao. Leo wanampenda sana Slaa. Kila siku slaa slaa slaa. Hata kama angekuwepo Slaa bila backup ya Mbowe asingefanya cho chote pamoja na akili yake yote. Ndiyo maana wanaomba Mbowe aondoke na abaki Slaa mwenye akili lakini hana bao kifedha. Wamewafanya kina mrema wawe kama ombaomba sasa wanataka Slaa arudi naye awe ombaomba kule chama kuu. Ndiyo raha yao. Mwanzo wa kila chama ni mtu jasiri na siyo mabadilishano tu. Zitto ni karibu sawa na slaa lakini pia shida yake ingekuwa hiyo tu pesa ya kuendesha chama. Wajumbe wa CHADEMA wanajua hili kwani siyo kama wengine wengi. Hivyo mtulie.
 
Iwe upinzani, iwe ccm bado hatuna mpangokazi wa kitaifa ambao ungewaongoza wanasiasa kufanya kampeni za mikakati ya kutekeleza mpangokazi.
 
Katiba na misingi ya Democrasia tunataka ifuatwe na serikali na viongozi wetu. Hili halina majadiliano.
 
Mleta mada umejichanganya Sana wewe hujui kuwa mtuhimiwa huwa hana hatia mpaka Mahakama imtie hatiani?

Pili Lowasa ndiye mgombea aliyepata kura nyingi zaidi za halali milioni6 kuliko mgombea mwingine yeyote. Hapa nimezungumzia kura halali tuu.
Sasa ulitaka Lowasa akubalike vipi zaidi ya uhalisia huo uliotangazwa na tume huru ya serikali yako?

Huduma za kijamii zilikuwa zikitolewa hata wakati wa ukoloni tena wazee wanadai elimu ya Mkoloni ilikuwa bora kuliko hii ya sasa.

Lakini wazee wetu waliona thamani ya Uhuru ni bora kuliko Elimu, barabara, hospitali au hata vyakula.

Wakajitoa Muhanga kupigania Uhuru kwa kumwaga Damu zao hata wewe umekaa hapo unafurahia matunda ya Uhuru ukiandika Ujumbe Kama huu.
 
Ccm wote wanamlilia Dr.Slaa sijuwi kwanin
Slaaa alikua anasimamoa anachokiongea....
angekuwepo Ukuta usingeahirishwa,Slaa alikua kiongozi mwenue kufanya utafiti wa kutosha kabla hajasimama kiongea...mikakati ya slaa ilifanikiwa kuliko ya sasa,angalia operation sangara,angalia pia M4C kabla Mbowe hajabadili gia angani.,,Hatatokea kama Slaa ndani ya Chadema..
 
Mleta mada umejichanganya Sana wewe hujui kuwa mtuhimiwa huwa hana hatia mpaka Mahakama imtie hatiani?

Pili Lowasa ndiye mgombea aliyepata kura nyingi zaidi za halali milioni6 kuliko mgombea mwingine yeyote. Hapa nimezungumzia kura halali tuu.
Sasa ulitaka Lowasa akubalike vipi zaidi ya uhalisia huo uliotangazwa na tume huru ya serikali yako?

Huduma za kijamii zilikuwa zikitolewa hata wakati wa ukoloni tena wazee wanadai elimu ya Mkoloni ilikuwa bora kuliko hii ya sasa.

Lakini wazee wetu waliona thamani ya Uhuru ni bora kuliko Elimu, barabara, hospitali au hata vyakula.

Wakajitoa Muhanga kupigania Uhuru kwa kumwaga Damu zao hata wewe umekaa hapo unafurahia matunda ya Uhuru ukiandika Ujumbe Kama huu.
Ndicho mlichobakiza kujitetea eti tuprove kama kweli Lowassa alikia Fisadi,
una macho lkn huoni,
una masikio lakini husikii,
naona mpaka ww ndo umekua Lubuva sasa unamatokeo ya uchaguzi, mbona kama Lowassa aliongoza mbona hajawa raisi? Na uweza kuprove kama Lowassa alishinda? Afu huo ni uchochezi inamaana hutambui ushindi wa Ccm? Mbona mimi nilimpigia Lowassa na nkakubali kushindwa?
 
Baada ya kufika sentensi sijui ya sita kuwa nani asiyejua kuwa upinzani wa Dr Slaa ulikuwa upinzani wa kweli na madhubuti nimeacha kusoma na kukupuuza.
Nyie ndani ya chama chenu si ndio mlikuwa mnambeza Slaa kuwa mwongo, mnafiki na Dr uchwara? Iweje leo hii eti baada ya kuondoka kwa hiari yake kawa madhubuti? Huu ni unafiki na propaganda za kitoto.
Halafu mambo ya vyama sio ya kitaifa. Kama chama kinaendeshwa kidikteta ni lazima kuwa huko? Unaondoka kwenda kwingine lakini nchi ya WATANZANIA WOTE hakutakiwi kuwe na udikteta wala uvunjaji katiba wa aina yeyote maana hatuna pengine pa kukimbilia. Ndio maana kuna Ukuta hapo 1/10 kama hakuna muafaka
 
Baada ya kufika sentensi sijui ya sita kuwa nani asiyejua kuwa upinzani wa Dr Slaa ulikuwa upinzani wa kweli na madhubuti nimeacha kusoma na kukupuuza.
Nyie ndani ya chama chenu si ndio mlikuwa mnambeza Slaa kuwa mwongo, mnafiki na Dr uchwara? Iweje leo hii eti baada ya kuondoka kwa hiari yake kawa madhubuti? Huu ni unafiki na propaganda za kitoto.
Halafu mambo ya vyama sio ya kitaifa. Kama chama kinaendeshwa kidikteta ni lazima kuwa huko? Unaondoka kwenda kwingine lakini nchi ya WATANZANIA WOTE hakutakiwi kuwe na udikteta wala uvunjaji katiba wa aina yeyote maana hatuna pengine pa kukimbilia. Ndio maana kuna Ukuta hapo 1/10 kama hakuna muafaka
Rudi ukamalizie kusoma na kwa taarifa yako huo Ukuta hautakuwepo,
 
Wadau naomba kujuzwa Ukiwa kiongozi wajuu ukahama chama je huwezi ukawa mwanachama wakawaida??
Pili kwanini vyama vya upinzani mnawakaribisha wakati wameharibu kwao??Wapo wakuwapokea lakini si kila maarufu aje na umaarufu katika chama chenye umaarufu!Kwanini wasiende Damian Dovuttwa?kama kweli hawafati vyama vyenye umaarufu??
Na hawa wanaowapokea hawajiamini!
 
Neno Democracy linahubiriwa kwa nguvu nyingi na baadhi ya vyama vya siasa nchini Tanzania mpaka kutishia usalama wa taifa kwa matamko mbali mbali ya VIONGOZI, hasa wa CHADEMA.

lakini ukivichunguza vyama hivyo ndani ya uendeshaji wake havifuati democracy hata kidogo.
Navishauri kabla ya kutoka hadharani na kudai democracy vijiendeshe ki democracy.

Mifano ni mingi Sina haja ya kuitaja jinsi vinavyoendeshwa kwa maslahi ya wachache na wanachama Kua ni stamp rubber tu.
"Charity begins at home "
1473157584047.jpg
 
Mnachotaka ni kuona vyama vya upinzani vikiwa katika migogori.Kinacho wauma sana ccm ni kuona watu wao hawapati nafasi ndani ya vyama pinzani kwa masilahi yao.Kw a taarifa yenu hawekwi bora kiongozi ili mpate urahisi ,hapa kazi tu
 
Mitizamo ya kisiasa ni mipana sana, naona hata kuijadili sana ni kupotezeana wakati tu, zaidi nahofia chuki kupanda na hatimaye yakatokea tusiyopenda kuyaona yakitokea.

Maana ikiwa ndani ya siasa kuna miungu watu, wakitawala kila kitu na kila idara, na kutaka kushangiliwa kila mahala, hatari yake ni kubwa zaidi. Maana watu hao wanaoshangilia ikitokea wakafumbuliwa macho siku moja.

Kwa umri wangu mdogo huu, nimeshuhudia siasa za kila aina (kushuhudia si lazima uwepo, kuna namna nyingi za kushuhudia). Nimekua nikimuona marehemu Ghadafi, akipendwa kila kona ya nchi yake na baadhi ya nchi za kiafrika, kheeeee kilichotokea ni walex2 waliokuwa wakimshangilia wanamuua.

Kabila (baba) marehemu, wakati anaipigania congo drc, alipokewa kwa nderemo haswa, na raia wakasema sasa amani itakuwepo, kheee kilichotokea ni mzee Kabila (baba) kuuliwa na mmoja wa walinzi wake mwenyewe (tuliaminishwa hivyo). Sasa fikiria, mlinzi wako anakuua, unajua chanzo kinaweza kuwa kidogo tu, mfano labda narudia labda aliamuru majeshi yaue raia wa eneo analotoka huyo mlinzi wake ama aliamuru polisi kuwapulizia mabomu ya machozi na kuwapiga raia wa eneo lake na kumpa kilema cha maisha labda mama yake ama baba yake aliyempenda sana. Ni mfano kwa uelewa.

Mlishuhudia kilichotokea nchi za Africa ya kati, ni vita vya kidini, na Nigeria baadhi ya majimbo (mikoa). Vita vya kikabila na kiukoo (huku sasa tunaita ukanda, na ndivyo huanza hivyo), mnajua zilivyowatafuna Rwanda na Burundi, na sasa vinaitafuna Sudani kusini na somalia huko, udini ndani yake umo.

Utasema sisi Tanzania ni nchi kubwa hatutakuwa na vita vya kikabila, enhee vya kidini utamuachia nani, na vya kikabila huwa vinaanza kama sasa, kuna siasa za ukanda, zikikomaa hizi ni balaa kwa Taifa.

Tuwe wamoja, tudumishe ushirikiano wetu, tujadiliane hoja, tutaniane kwa busara, tufanye kazi kwa bidii, viongozi waongoze kwa uweledi, kisheria na hofu ya Mungu, ubabe ubabe hautakiwi, maana hautakuwa kiongozi / mtawala milele.

Ahsante!
 
Back
Top Bottom