Elections 2010 Vyama Vya Upinzani Iringa Mjini Vyaungana: V.O.A

Kumbe chadema inatisha hivi eeeh?!!!

Nilishasema kuwa mkakati wa CCM ni kutumia jeshi lake la akiba lililoko kwenye vyama vya upinzani na Usalama wa Taifa kuhakikisha wanapita kwa hila yoyote. Hizi ni dalili tosha kwamba sasa hali ni tete na ccm wamekosa msimamo na staha. Chama kinachojisikiliza na kuacha kusikiliza watu mwisho wake ni kuanguka kwa kishindo. Mnachokiona iringa ni dalili ya kitakachotokea ktk siku ya kuhesabu kura. Amini nakwambia safari hii CCM wataiba kura kidogo mno lakini watawapa mamluki wao hela za kuibia kura ionekane kwamba upinzai wameiba kura (kupunguza za chadema). Dawa ya chadema ni kuwa makini na kutofungua mlango kwa wakala yeyote wa chama chochote
 
tehe kama nawaona wanyalukolo wanapigwa na mtogwa(ulanzi) wa mia tano tuu wanakunywaaaaaaaaaaaaaaaaaa wakiamka na hangover wananyosha vidole viwili chademaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

hizi dharau sasa
 
Kama kuna mahali sisi m wanakosea ni katika eneo hili maana wao hupunguza kura zao. Ninao mfano halisi wa jimbo la Bukoba mjini.

Kuna habari za uhakika kuwa Hamis Sued Kagasheki alim-recruit jamaa aje kugombea kwa tiketi ya CUF ili kudhoofisha Chadema na kufanya mgawanyiko wa kura. Kwa wasiojua zamani Chadema haikuwa na nguvu sana bali CUF kwa kuwa watu wengi walikuwa wakimfuata kiongozi wao Wilfred Lwakatare wakati huo akiwa makamu katibu mkuu taifa CUF. Lakini huyu bwana alipoamua kujitoa CUF na kwenda Chadema aliondoka na kundi lote la watu. Kwa mahesabu ya Hamis alihisi anaweza kuweka mapandikizi kwa faida yake.

Lakini kwa uelewa wangu wa kisayansi nimegundua kuwa alifanya jambo jema maana kajipunguzia kura mwenyewe. Nasema hivi kwa kuwa najua wana Chadema ambao ni wengi sana katika jimbo la Bukoba hawawezi kwa namna yoyote kumpigia kura mwakilishi wa CUF. Na wana CUF ambao wapo na tena ni kikundi kidogo sana cha wana dini fulani, hawawezi kumpigia kura mwakilishi wa Chadema hata iweje. Lakini suppose kama kungelikuwa na wagombea wawili tu yaani wa sisi m na Chadema kwa vyovyote wale walio upande wa CUF wasingekuwa na jinsi na kwa vyovyote vile wangempigia kura wa sisi m ili kumkomoa wa Chadema. Na hapa ndipo hesabu zilipompiga chenga kagasheki. Namshukuru kwa kujipunguzia kura.

Wacha waungane hao mamluki waliojaa husuda tu ya mafanikio ya Chadema na kushindwa watashindwa maana hawana soko tena.
hustahili kuwa mwana CHADEMA kwa sababu huamini katika demokrasia, you are neither a great thinker even.... mara zote una -sound very violent na kwa kweli watu wa aina yenu, kuna umuhimu mkubwa wa kuwashuhulikia.
I like this forum kwa sababu inaonyesha wazi hisia za watu hata wasio na fikra pevu kama wewe.na kutokana na uwepo wa watu kama wewe ndani ya wafuasi wa chadema ndio maana CHADEMA kunaonekana harufu ya udini na ukabila.
wakati ukweli ni kwamba misingi ya uanzishwaji wa chadema imeegemea katika utaifa na ukombozi wa mtanzani na falsafa ya chadema inaonyesha hivyo...
Ila kosa lililofanywa na CCM linaelekea kurudiwa na CHADEMA kwa kuwa na wa2 wa aina ya mchukia fisadi
ndani ya chama.
Kama wanasiasa na washabiki wote wa siasa wangekuwa kama SLAA,ZITTO KABWE NA HAMMAD RASHID basi hii nchi ingekuwa paradiso
 
Kuwa mkweli kidogo na pia uelezee vipi huyo bwana alijitoa. Unaelekea utafikiri huyo bwana alijitoa wakati bado akiwa "makamu katibu mkuu taifa CUF" wakati ukweli ni kuwa alivuliwa hiyo nyadhifa kabla hajatimkia huko Chadema.

Kama washabiki wa CUF ni wale watu wa dini "flani", basi dini flani nyingine ndiyo watakuwa mashabiki wa Chadema? Au ukweli ni one sided tu? :becky: :becky: :becky:

Tungojee baada ya Oktoba 31 halafu hizi analysis zenu za "kisayansi" ndipo tutakapozichambua vizuri. :becky:
UKO RIGHT KAKA, jamaa sio tu kwamba sio great thinker but i think he doesn't think at all
 
Kumbe chadema inatisha hivi eeeh?!!!

Nilishasema kuwa mkakati wa CCM ni kutumia jeshi lake la akiba lililoko kwenye vyama vya upinzani na Usalama wa Taifa kuhakikisha wanapita kwa hila yoyote. Hizi ni dalili tosha kwamba sasa hali ni tete na ccm wamekosa msimamo na staha. Chama kinachojisikiliza na kuacha kusikiliza watu mwisho wake ni kuanguka kwa kishindo. Mnachokiona iringa ni dalili ya kitakachotokea ktk siku ya kuhesabu kura. Amini nakwambia safari hii CCM wataiba kura kidogo mno lakini watawapa mamluki wao hela za kuibia kura ionekane kwamba upinzai wameiba kura (kupunguza za chadema). Dawa ya chadema ni kuwa makini na kutofungua mlango kwa wakala yeyote wa chama chochote

Utajua kama inatisha ama inachekesha baada ya Oktoba 31. Usipotee tu humu. :becky:
 
Back
Top Bottom