George Maige Nhigula Jr.
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 470
- 149
Ndugu Wana JF,
Nadhani sote tuna kumbu kumbu njema mda si mrefu mwaka jana wakati wa kampeni za uchaguzi, Mgombea wa CCM JAKAYA MRISHO KIKWETE aliwatangazia watanzania kuwa vyama vya siasa vya upinzani vinafaa kupuuzwa na kuto aminiwa na wananchi kwani ni vya msimu, yaani ni vyama vya uchaguzi tu!
Nadhani wengi wetu tulipinga sana kauli hiyo ya mgombea wa CCM JK na iliyokuwa ikipigiwa tarumbeta na makada wengi kwenye social media mbali mbali kama JF, FB, TWITER etc.
Lakini baada ya uchaguzi kumalizika CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO kimeendelea kufanya shughuli zake za kisiasa kama kawaida kwa hari na vuguvugu jipya la ukombozi kwa kudai katiba mpya na kupambana na ufisadi unaendelea kulitafuna Taifa letu, Lakini tumeshuhudia jinsi serikari ya CCM chini ya JK ikifanya kila mbinu kuhujuma CHADEMA isiweze kufanya siasa na kuendelea kujiimarisha kama chama kikuu cha upinzani bungeni.
Kitendo cha serikari kupiga marufuku mikutano kadhaa ya wabunge wa chadema nchi nzima na kuzuia maandamano ya amani ARUSHA ni dhahiri kabisa ni jitihada za kutaka tamko la JK wakati wa kampeni kutimia yaani vyama vya siasa vya upinzani ni vya msimu.
Tumemsikia mkuu wa kitengo cha propaganda TAMBWE HIZA akisema kuwa uchaguzi umekwisha chadema hawapaswi kufanya siasa, Je hii ina maana gani?
Ni ukweli usiopingika kuwa CHADEMA kimechukua nafasi yake kama chama kikuu cha upinzani Tanzania kwa ufanisi mkubwa na kimekuwa mstari wa mbele kupigania haki za wananchi na kuwaumbua watawala kiasi kwamba hali ya CCM ni taabani kutokana na kibano cha chadema. Hivyo mimi binafsi napenda kumwambia Raisi Jakaya Kikwete kuwa inawezekana kuna vyama vya upinzani ni vya msimu yaani wakati wa uchaguzi lakini sio chadema, kwani kibano wanachokupa nadhani unakuwa na wakati mgumu sana,
Sasa ni mda wako JK to show leadership kwani CHADEMA ni mwendo mdundo mpaka 2015