Vyakula vya aina 5 vinavyosafisha Ini lako

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
VYAKULA 5 AMBAVYO VINASAFISHA INI LAKO.jpg

VYAKULA VYA AINA 5 VINAVYOSAFISHA INI LAKO

Vyakula vingi vinavyotumika kwa kizazi cha sasa ni vile vya kusindika, kukaanga ambavyo vinafanya ini liweze kufanya kazi nyingi na mara nyingine kuzidiwa.

Kama ini likizidiwa,basi litashindwa kutoa sumu na mafuta kwa ufanisi.
Kuna vyakula vingi vizuri ambavyo vitachochea uwezo wa asili wa kusafisha taka za sumu katika mwili wako.

Orodha hii ni muhimu na inajenga zaidi juu ya vyakula ambavyo vinaweza kusaidia kusafisha ini lako.
Ukitumia vyakula hivi utaweka ini lako katika afya nzuri na kukufanya uwe na afya bora,tumia vyakula hivi angalau mara moja kwa wiki

1.Vitunguu Somu
Kiasi kidogo tu cha kitunguu somu kina uwezo wa kuamsha enzymes za ini na kusaidia kutoa sumu katika mwili wako.Pia Vitunguu somu vina kiasi kikubwa cha allicin na selenium, vitu viwili muhimu kwa kulisafisha ini lako

2.Grapefruit
Ina wingi wa vitamini C na antioxidants,balungi uongeza mchakato wa usafishaji wa ini. Glasi moja tu ya juisi ya Grapefruit itakusaidia kuongeza uzalishaji wa enzymes za ini ambazo zitakusaidia
kutoa carcinogens na aina nyingine za sumu

3.Beets na Karoti
Ulaji wa beets na karoti utakusaidia kwa ujumla kuboresha shughuli zote za ini.

4.Mboga za majani
Ni moja ya mshirika mzuri wa utakaso wa ini, mboga za majani zina uwezo mkubwa wa kupunguza kemikali za madawa,utumiaji wa mboga za majani ina kinga kubwa kwa ini lako

5.Avocado
Ina madini ambayo yanasaidia mwili kuzalisha glutathione, ambayo ni muhimu kwa kusafisha sumu
hatari katika ini lako
 
Hakika leo umefanya jambo jema sana kuliko kila siku kutoa kasoro ya baadhi ya vyakula bila kutoa mbadala wake
 
Back
Top Bottom