Kibo10
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 11,277
- 8,840
1. Uji wa pilipili
2. Magimbi
3. Viazi vitamu
4. Tambi nyembamba
Vitu hivi vinapikwa kwa ustadi wa hali ya juu na mama ntilie mpaka hotel za kati, Nimejiuliza vina mahusiano gani na mwezi huu, Maana baada ya mwezi wa Ramadhani vinayeyuka mtaani.
Au ni Quran imeagiza kula milo hiyo kipindi cha mwezi mtukufu?
2. Magimbi
3. Viazi vitamu
4. Tambi nyembamba
Vitu hivi vinapikwa kwa ustadi wa hali ya juu na mama ntilie mpaka hotel za kati, Nimejiuliza vina mahusiano gani na mwezi huu, Maana baada ya mwezi wa Ramadhani vinayeyuka mtaani.
Au ni Quran imeagiza kula milo hiyo kipindi cha mwezi mtukufu?
Uji wa Pilipili Manga au Chai ya Viungo Spiced Tea,hutumika saana kipindi hiki.
Na ukweli ni kwamba baada ya kufturu (Kuftari) mwili unahitaji ku gain nguvu kwa muda mfupi na virutubisho vingi sana.
Na asikudanganye mtu,we kunywa Uji wa Pilipili Manga au wenye viungo vingine uone ndani ya dakika kumi hali itakuwaje.
Mie hupendelea zaidi Uji wa Mtama au Ulezi wa viuongo,ukiunywa huo basi hata kama ni siku za kawaida mkuu utaniambia habari yake.
Chai ya viungo vilivyokamilika hutumika pia kama tiba,yaani wakati mwili hauna kitu unakuwa active saana ku absorb virutubisho muhim.
Na ndio maana utakuta kwamba wale wanao Swali Swala ya Taraweh(Suala Ndefu),hunywa Uji tu au Chai ya viungo na chapati au andazi moja au mbili kisha kujiona kuwa na nguvu saana,ili kuweza kuwa mwepesi katika Swala ya Taraweh.Ili baada ya swala wakati wa daku ndio aweze kula vizuri maana mwili utakuwa umefunguka vizuri kupokea mlo mkubwa.
Ila wale wanaofakamia kula saana,basi swala hii kwao huwa ni uvivu saana kuiweza.
Vyakula vya ziada kama
Tambi
Viazi
Njugu Mawe
Maharage
Dengu
Chooko au choroko
Kunde
Maboga
Vipopoo(hasa huku kwetu Zanzibar)
NK
Sio kwamba vinatumika saana,ila sema tu mfumo wa manunuzi na Maisha ndio unapelekea iwe hivyo. Na pia watu wengi wavivu kuvipika miezi ya kawaida.
Ndio maana unakuta miezi ya kawaida ni waliii, ugaliiii, ukipata bahati ndizii. Sasa ni vyakula vilivyo common saana.ndio maana mwezi huu watu hupenda kubadilisha
Ila kama akitokea mtu mjanja kwa nyie mliopo Dar akapika aina ya vyakula mchanganyiko kama hivi kwenye mgahawa wake, amini usiamini atapiga hela ndefu kweli.
Ila sie tumefanya mazoea ya milo iliyo common
Kwa wale Mliopo Zanzibar kuna Mgahawa unaitwa Lukmaan, pale unakuta vyakula aina mbali mbali sana kwa kadri ya uwezo wao. Na jamaa ukienda pale watu kibao hadi pa kukaa unapakosa. Na wazungu telee
So, kama upo Dar na umeona vyakula hivyo vinapendwa basi chukua Fursa mungu amekufungulia kwamba. Baada ya Ramadhani anzisha biashara ya namna hiyo kwa vyakula hivyo, na utatoka tu.
Hoja kubwa ni kwamba watu wanapenda kupika vyakula vyepesi kupika, wali, maharage, ugali.
Sasa vile vyakula vinavyomchukulia mtu muda anaona havina issue. Na Hii ipo mpaka Majumbani kwetu na ndio imetubadilisha mfumo wa kula.
We muulize mtu lini Amekula Njugu mawe au Msusa wa Karanga, utakuta mtu anakuambia sijala miaka kumi au nilipoenda mkoa fulani.