Vurugu Zanzibar, matokeo ya udini au Uchaguzi Mkuu 2010?

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,883
1,482

Deogratius Temba

PENGINE tunaweza kupingana, kukosoana na kutokukubaliana kuwa tatizo au sababu ya vurugu za Zanzibar zilizotokea wiki iliyopita ni udini au chuki za kiimani zilizoasisiwa na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi Mkuu mwaka 2010. Tuna kila sababu ya kuendelea kuwalaumu na kuwalaani wanasiasa waliotufikisha hapa.
Hali ya hewa imechafuka wao wamekaa pembeni! Hata kama Muungano utavunjika ni kwa uzembe wao. Haya ni matunda ya kutumia udini kujinufaisha kisiasa, walifanikiwa kuwagawa Watanzania kimakundi, ili wawatawale kirahisi.
Hii ilikuwa ni mbinu ya chama tawala kulikuza suala hili, wakilitumia kama mbinu ya kuua au kudhoofisha upinzani baada ya ukabila kushindwa.
Sababu nyingine ya CCM na viongozi wake kupandikiza mbegu ya udini ni kutaka kuvunja nguvu ya upinzani, baada ya kuona CHADEMA inakuja kwa kasi hasa baada ya CCM kujeruhiwa vibaya kwenye uchaguzi 2010.
Tutakumbuka kuwa agenda hii ilitumika sana kuwa CHADEMA ni chama cha Wakristo na hata tumeona kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga mambo yalivyofanyika baada ya CCM kufanikiwa kukipaka matope CUF kwamba ni chama cha Kiislamu. Kwa sera yao ya udini, sasa wameamua kuhamishia majeshi yao CHADEMA baada ya kufanikiwa kuisarambatisha CUF.
Udini unatumiwa na CCM kama kielelezo kwamba serikali inasemwa na kusimangwa sana kuhusu ufisadi kisa Rais ni Mwislamu, hata sasa hivi kuna watu wanazusha eti Mkulo (Mustafa) alihujumiwa kisa ni Mwislamu.
Kwa kuwa CCM wameshindwa kutimiza ahadi zao kama Maisha Bora kwa kila Mtanzania, wameamua kutumia udini kama sera ya kulinda uzembe,ufisadi na maovu yao! Kiongozi Mwislamu akishindwa kutekeleza wajibu wake akishughulikiwa wanasema ni kwa sababu ni Mwislamu.
Agenda ya Muungano imeingizwa kwenye suala hili la udini, kuwa umetawaliwa na mfumo wa Kikristo, na Tanzania Bara imejaa Wakristo, na wanaichafua Zanzibar, kwa hiyo ukiua Muungano Ukristo utakosa nguvu Zanzibar.
Haya ni matunda ya kukua kwa mbegu ya udini iliyopandwa na watawala wetu mwaka 2010. Niliandika katika gazeti hili katika safu hii Januari 29, mwaka huu, niliona mbali na kutabiri hili kutokea Zanzibar kwa sababu nilishaona jinsi CCM na viongozi wake wakuu walivyoutumia mtaji wa udini.
Serikali inafikiri kuwa kuwagawa Wakristo na Waislamu, ikapandikiza chuki itafanikiwa kuwatawala daima! Amani ni muhimu!
Nchi za Afrika ya Magharibi zina Waislamu tena wenye imani kali kuliko Tanzania, Afrika ya Kaskazini na hata Bara la Asia kumekuwa na machafuko na vuguvugu la kudai mabadiliko kwa muda mrefu, lakini hata siku moja hawajawahi kuchomeana makanisa au nyumba za ibada.
Wananchi wa huko hawakubali kugawanywa kwa itikadi za kidini kama hapa kwetu, wanaungana, wanajenga hoja wanaamua kudai mabadiliko na kuuwajibisha uongozi.
Kila Mtanzania anajiuliza Zanzibar hawataki Muungano au hawataki Makanisa? Je, tatizo la Muungano ni Ukristo? Je, Ukristo ukiondoka tatizo la Muungano litamalizika?
Viongozi wetu wanachochea, wanachekelea na wanafikiri wameshinda.Watanzania waachwe wajadili,waelimishane, wakemeane kama Watanzania bila kujaili dini na kama hawautaki Muungano waseme waziwazi.
Tunatonana wiki ijayo.

Chanzo Tanzania Daima

Hakuna shaka (Deogratius Temba) kuwa umeona mabali.

Kipindi cha nyuma hivi kama mwezi niliandika kuwa kuiondowa ccm madarakani sio kitu cha rahisi bila ya vyama vya upinzani kungana, hususan vyama vikubwa vya upinzani yani Chadema na Cuf , Ccm ni chama kikongwe na kimetawala kipindi kirefu na kina binu nyingi tu.

Sasa kusema kuashia Dola hivi hivi sio kitu cha rahisi, zamani ilikuwa aduwi mkubwa wa ccm ni cuf na walitumia mbinu nyingi tu cm zikiwemo za kuwagawa wananchi kwa kutumia sumu ya kuwa cuf nichama cha Warabu, chama cha Udini na walipo chindwa mbinu zote wakawagawa watu kwa upemba na Unguja.

Yote hayo ilikuwa ni mbinu chafu za ccm kukizoficha chama cha cuf na mwicho wakaamua kunda Serekali ya umoja wa kitaifa na kugawana wizara.

Sasa hivi sasa ccm wanaona hali ilivyo 2015 na Chadema anavyokuja moto wa juu, kimeona tumwage sumu ya udini ili kukipiga fulstop Chadema, ndio ukaona wanasambaza sumu kuwa chadema ni chama cha kanisa kikiongozwa na viongozi wake wakuu Dr Slaa na Mbowe.

Hili kwa upande wa Pwani na Zanzibar limepokewa vizuri sana na hii ni isabu ya ccm kuona kuwa ikiwa Waislamu hawato ipigia chadema basi wataipigia cuf ambayo sio tichio kwa ccm hivi sasa.

Isabu zinasema hivi ikiwa waislamu watajitokeza wengi na kuipigia Cuf basi kura za Chadema hazito wafanya wanyakuwe Dola kutowa Rais na Cuf itapata wabunge wengi tu Zanzibar na wanaweza kupewa mikowa miwili mitatu nyenye waislamu wengi Bara mikowa ya Pwani na maeneo mengine.

Sasa na Chadema atazidishiwa wabunge tu,Nafasi ya urais na kuongoza Dola inabakia kwa ccm, baada ya ccm kuchakachua na kuwagonganocha vishwa chadema na Cuf kwa udini ulio msababisha Chadema kukubalika kwake.

Hii ndio tetesi na mikakati ya ccm katika turufu yao na karata yao wanayoisheza hivi sasa, ndio ukaona fataki iliopigwa Zanzibar taget yao ccm ni kuwataget Chadema kwa kwa udin na kuamsha hisia za udini.

Na hili nazani Chadema wamechakuwa alart ndio ukaona wako kimya kwa matokeo ya Zanzibar hawakupurushuka tu kuja juu na kuwalaumu Waislam wa kikundi cha Jumuia ya Muamsho.

Mimi naweza kusema kuwa inawezekana juu yakuwa Uamsho kampeni zao zinakuwa kali juu ya kuto kukubali Muungano huu , lakini kuchomwa Makanisa ikawa nimbinu za ccm ili kuwagonganisha vichwa watu kwa kutumia udini kama kujikocha ccm katika utawala wao.

Kuna kila dalili za chaka hususani vikogo wa Zanzibar wanaona Chadema ikichukuwa Hata wao hawako salama Zanzibar, hii nikuwa ccm itapoteza mvuto hata kwa Zanzibar, ndio likatarishwa sakata hili la Zanzibar siku ilikuwa inadaiwewa ili watu wapitishe agenda yao.

Ccm wana kundo maalum huko Zanzibar na hilo linajulikana kundi la hujuma Janjawii, nivijana wa ccm wenye kufanya hujuma mbalimbali likisimamiwa na vigogo wa ccm, hundi hilo halijifichi hutowa maelezo ya hujuma hazarani kwa vile lina mkono wa vigogo wa ccm.

Ndio ukaona baada ya Jumuia ya Muamsho kufanya Mandamano ndio uperation ya vigogo ikawa secced, Polisi wakashiriki kikamilifu kuwafumbia macho na hujuma hizo na Muamsho ikawa ndio wametolewa kafara na watu kupotezwa lengo.

Habu fikirini Muamsho wamefanya Mandamano na wakamaliza salama bila kuingiliwa na Jeshi la Polisi wakachawanyika na kwenda majumbani kila mtu, usiku wake wakamkamata kiongozi moja wa Muamsho tena ni kiongozi wa chini tu mdogo kabisa.

Hata kama watu wa mskiti anao salisha walikwenda kituoni kumulizia mazingira alokamatiwa lakini Polisi walianza kurusha mabomu pale kituo cha Madema na kuchawanywa mitani na wengine kwenye magari ,sasa hao vijana waliokuwa wakiyachambulia Makanisa na Mabaa na magari ya sehemu nyingine , jee Polisi walochawanywa mitaani walikuwa hawawaoni?.

Kwa maneno ya Maskofu wa Makanisa wanasema vijana walochoma moto Makanisa walikuwa wakitembea kwa vikundi na walikuwa na silaha za jadi yani mapanga mawe na visu na hawapunguwi mia mbili katika kuwaona Padri wa Kanisa la Kariako Zanzibar anasema?.

Sasa chakujiuliza nikuwa Polisi walikuwa wapi wakati huo hata wasifike hapo? wakati Makao makuu ya Polisi Zanzima iko Hapo hapo hata hatua mbili hazifiki kutoka Hapo lilipochomwa kanisa na makao makuu ya Unguja mzima yapo hapo na Nyuma zote takriban hapo ni Zapolisi.

Na hata Mh Waziri wa Mambo ya Ndani Mjimbi alikuja kuweka mkutano hapo hapo Ziwani eneo hilo hilo la kariakoo, hii inatia wasi wasi na chaka kuwa waliofanya hivyo wamepata mkono wa Baraka kutoka kwa vigogo na suala la uamsho silaku puza nilakulichunguza kwa kina na kuwafikicha wahusika Mahakamani ni wazo zuri ili kujuwa nyuma ya pazia kuna nini?.

Mara nyingi viongozi wa ccm Zanzibar wanapopanda kwenye majukwaa husema tutatumia silaha zetu za jadi tulio pindulia nchi hii bado tunazo na tunazienzi, Sasa waliokwenda kumvamia Padri ni silaha hizo hizo za Jadi na waliokwenda ni watu wasiopungua mia 200, hii inatia wasi wasi kuwa kuna mkono na baraka za viongozi.

Kwa usiku ule walivyoenezwa askari na takribani watu kutembea ilikuwa ni kwa hofu,mji ulikuwa umejinamia kimya vipi watu waweze kutoka kanisa hadi kanisa kuchoma moto, bilashaka polisi walikuwa wanajuwa na walipata baraka kwa wakuu wao .

Mimi nahisi hata Chadema Baada ya ile kamati yakufichua Ufisadi wa kuticha kwa kutafunwa pesa za Umma basi na swala hili walifuatilie watajuwa jee linamkono wa kisiasa au dini? hii itaweza kufichua mengi yaloko katika nyuma ya pazia.

sisi tunaweza kusema Muamsho kumbe tageti zimepigwa mbali muamsho ikawa ni kutolewa tu kafara agenda ikawa nyengine.

Katika kipindi hicho chote cha nyuma Cuf ilipikiwa mbinu chafu kila sampul na ccm , kwanza kulingizwa sumu ya ccm kusema cuf ni chama cha warabu,walipoona wafuasi hawakuitikia wito huo na kupokea sumu hio, wakaja na nyingine yakusema nichama cha wapemba, mambo hayo yalizima yote pale cuf kilipo ungana na ccm na kunda Serekali ya Pamoja ndio yote hayo yakazima na watu wakagawana wizara.
 
Back
Top Bottom