Vurugu za UAMSHO Zanzibar: Polisi auawa kikatili...

Mnyika alisema tumefikishwa hapa na Serikali lege lege wakataka kumtoa macho pale bungeni, sasa wananchi wanajionea wenyewe kwa macho ulege lege wa Serikali, kama ni kweli Askari amechinjwa nasubiri kusikia matamko ya viongozi wa CCM, taratibu ardhi ya Tanzania itaanza kulowa damu........Hongereni CCM mbegu yenu ya udini imeanza kumea na muda si mrefu mtavuna, endeleeni kupalilia.
 
Hili la UAMSHO wa kulaumiwa ni Nyerere na Karume na muungano wao feki wa kwenye kijiwe cha kahawa!
 
Imani za kuiga zisitufikishe tulipo. Uislamu na Ukristo zote naita umani za kuiga kwa sababu kabla ya kuletewa, kulikuwa na imani za kwetu. Nani mwenye uthibitisho wa kisayansi kuwa imani ipi ni sahihi na ipi si sahihi? Wageni wametufikisha pabaya na wanachekelea ujinga wetu.

there you are comred. ni iman za kuiga na kibaya zaidi hatukuzipokea kwa nguvu kama tunavyotumia nguvu kuzifanya ziwepo. Sasa kama hatukuzipokea kwa nguvu, iweje tuzilinde kwa maguvu hayo?
 
Tumeona double standard ya Polisi juzi baada ya RPC Barlow kuuawa. Je watatuonesha kiwango kkingine ktk hli la mwenzao kuchinjwa?

Jana nimesoma kauli ya Kova eti "sasa wanataka kuwaonesha (?.....) kuwa nao sasa hawako juu ya sheria...." Nikatambua kuwa sheria zetu zimeweka matabaka mengi mno kiasi kwamba sio kila mhalifu ni mhalifu. Na pia raia wote hawako sawa mbele ya sheria za nchi. Nikaogopa kidogo kwamba kumbe Polisi hawawezi kumshughulikia mhalifu mpaka wapate nasaha, ridhaa, wapime upepo wa kidini ndipo wachukue hatua.

Nikajutia upuuzi ambao tumeupa kipaumbele sana katika kila nyanja ktk miaka ya karibuni. Nikajutia pia upumbavu tulioonesha pale tulipotupa tunu zetu za upendo, umoja, busara na ustahimilivu sijui kwa bei gani na kwa hasara ya nani.
 
Kwa nini nalazimishwa kuanza 'kuwaogopa' waislamu? This is not fair, not fair at all!
 
Eti ooh, serikali ya umoja wa kitaifa imeleta mtengamano zanzibar, wapi na wapi? Maalim ana ajenda ya siri na zanzibar wale wanaomshabikia kuna siku wataumbuka. Cuf na uamsho ni chanda na pete. Zanzibar tunasubiri ugaidi kuongezeka na si kupungua!
 
matunda ya ccm hayo walijua wanaikomaoa chadema tu..

Hawa jamaa nao bana, wangekuwa wababe na wanahasira na jeshi la polisi wangeonyesha juhudi zao za kuchoma makanisa kwa kuzihamishia kuchoma vituo vya polisi
 
Viongozi wetu ndivyo wanavyotaka hawapendi kujifunza toka kwa wenzetu kama Rwanda na Kenya. "Wiseman lean by othermans mistake but fools by their own", kama wanandoa wanadai wameshachokana wanadai talaka lkn wazazi wanawang'ang'aniza kuendelea na ndoa kwa kuogopa aibu kwa majirani unategemea nini kama sio mmoja wao kuwekewa sumu au kuchinjwa ? Kama ni 20% tu ndio walipenda vyama vingi lkn busara ikatosha kusoma alama za nyakati kwa nini busara hiyo isitumike sasa? Tuitishe kura ya maoni wananchi tuamue kwa amani kama tunataka au hatutaki muungano ili tumalizane kwa amani.
 
Kwanini hao UMASHO wasipewe fursa ya "kuendesha nchi"?( utadhani wana uwezo hata wa kufikiri jambo lenye manufaa kwa jamii na kulitekeleza, zaidi ya uharibifu tu)....bora bara wameliona hilo na kuanza kulchukulia hatua.
 
Serikali iko Oman inakula bata. Mpaka warudi watakuta Uamsho washafanya mambo makubwa sana.
Haya ndo maendeleo kwa kasi mpya na kwa ari mpya
 
waliofanya vurugu kwa kiasi kikubwa ni kikundi kimoja kinaitwa Ubaya Ubaya.....
 
N'jomba che nkapa angerudi hata kwa siku moja ili awatokomeze hawa wauwaji
 
Mkuu huko Zenj hii haihusiani na udini ni kuhusu Muungano tu!Hawa UAMSHO wao wanatumwa na wakubwao wao huko Oman kuhakikisha wanavunja muungano!

Mi niko tofauti na wewe kidogo, kwani naona ni zaidi ya huo muungano.Kwa sababu wakishavunja tu muungano wata declare zanzibar kama nchi ya kiislamu na makanisa machache yatakayokuwa yamebakia(si unajua kila vurugu hizi zikitokea wanabomoa makanisa) yatabomolewa!
 
Back
Top Bottom