Vurugu za Mbeya part II

Polisi wanapitia phase ngumu sana katika kazi yao. Napata mashaka kama wanaujuzi na uzoefu wa kushughulikia hizi purukushani tunazoziona leo.
Na kwa wale wanaoona sifa kuendelea kutumia dola kutimiza malengo yetu ya kisiasa, yanayoendelea leo ni ushuhuda tosha kwamba times change! Mnatakiwa kufikiria upya kabla ya tatizo kuwa kubwa na kuwazidi uwezo wa kukabiliana nalo.
 
Sugu for Mbeya namkubali sana sugu,Bujibuji weka taarifa rasmi maandamo ya nini? Tukinukishe jaman kama Tunisia kuwaondoa magamba madarakni,Hongereni wana mbeya kwa kuamua polisi wajifunze wasitegemee risasi ndo zitatuliza fujo,hamtoweza kuwapiga wakazi kama waliofulika kwenye uwanja wa NMC,mtaua watu wachache tu lakini ndo hiyo hiyo itakua mwisho wenu
 
Sawa kabisa!!

Tumshaurini Rais wetu Nini CHAKUFANYA!! Hali ndio kama hvyo!!

1. Vijana wasikilizwe sio kukimbizana nao mtaani!! ... Hii inakomaza tatizo!!

2.

3.

4.
 
waheshimiwa mnaotumia magari ya stk,su stj wasikilizeni vijana risasi mabomu hayatawatuliza.hapa ni jukumu lenu kukaa chini na kusema nini kifanyike kunusuru taifa
 
waheshimiwa mnaotumia magari ya stk,su stj wasikilizeni vijana risasi mabomu hayatawatuliza.hapa ni jukumu lenu kukaa chini na kusema nini kifanyike kunusuru taifa

Kwa wale wote tunayoipenda nchi yetu huu ni wakati wa kuomba sana juu ya hatima ya amani na utulivu. Japo masuala ya machinga kupambana na vyombo vya dola yamekuwepo toka tulipojiingiza katika mfumo wa soko huria, hiki kilichotokea mbeya ni kielelezo cha hatari ya suala la umasikini na ukosefu wa ajira kulipuliwa na wanasiasa. Ki msingi ni jambo la kusikitisha na linalohitaji umakini na busara kubwa katika kuliendea. Pia linahitaji uzalendo na ukomavu mkubwa wa kisiasa.

Hatua za haraka za busara zinapaswa kutumika kuepusha moto kuliko kusubiri kuuzima. Na hili tunaopenda nchi yetu na kujipenda wenyewe tunapaswa kulipa kupaumbele bila kujali maslahi na tofauti zetu za kisiasa. Nionanvyo mimi, wapo waliyomo ndani ya CCM na vyama vya upinzani ambao wangependa moto uwake bila kuwa na uhakika wa kuuzima ili mradi kiwi yao ya kisiasa ifanikiwe. Hali kadhalika ndani ya CCM na vyama vya upinzani wapo wazalendo ambao wako tayari kushilikiana kuzuia moto. Mwisho wa siku moto ukiwaka utaunguza nyumba tuliyomo na wwote tutakuwa wa kukosa.
 
Back
Top Bottom