Vurugu za kidini je ni akili kumfia Mungu asiyekufa na mwenye nguvu?

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
6,376
6,720
Kinachoendelea nchini Tanzania ambapo vurugu zimeishatokea kinaelezewa kama vurugu za kidini. Je ni kweli ni chuki za kidini au kukata tamaa kwa watu wetu? Nimejaribu kujihoji na kuhoji mantiki ya mtu ambaye ni kiumbe dhaifu kuliko vyote kuwa tayari kuua hata kuuawa eti kwa ajili ya ima dini au Mwenyezi Mungu. Nashindwa kuelewa kutokana na ukweli kuwa Mungu hafi ila binadamu anakufa. Je hapa wahusika hawasemi ukweli kuwa wanapambana kupata maisha bora kwa wote kwa kutumia mgongo wa dini? Kama tutamfia Mungu asiyekufa yeye Mungu atafanya kazi gani? Kwanini tufie dini zake wakati mwenyewe yupo anaangalia? Je sisi ni vichaa na mataahira au ni wajanja wenye hoja fichi? Wanangu nataka maoni yenu lau tujadili jinsi ya kulielekea hili. Maana tukilinyamazia litalimaliza taifa letu.
 
Mwanangu Maulid Daniel dini ninayo ingawa siyo kati ya hizi za kimamboleo. Dini kama mfumo wa maisha wa kiumbe si lazima uwe uislam au ukristo. Maana watu wamekuwapo kabla ya dini kuanzishwa, mfano sisi waafrika tulikuwa na mifumo yetu ya maisha kabla ya kuja kwa hizi abracadabra mwanangu. Hivyo mwanangu Maulid jibu swali badala ya uzushi wa kitoto.
 
mzee wangu nadhani hii ni kukata tamaa na maisha tu. wala hamna lolote. ugumu wa maisha ndio unaosababisha wa2 wafanye mambo ya kipuuzi kisa eti wanafia dini. na hao wahamasishaji wao kama vile wamejua. maana wamekuja kipindi ambacho maisha ni magumu. pia wengi wa wanaofanya huo upuuzi ni wale wasio na elimu. Nina rafiki zangu ambao nimesoma nao, nikiwaulizaga hili jambo, wananiambia kuwa wenyewe wanawaona wa ajabu sana hao ndugu zao. na pia wanasema hawawezi kuwaelimisha, kwa maana wakiwaelimisha wataenda kuwashtaki kwa walimu wao ambao asilimia kubwa hawana elimu yeyote zaid ya elimu ya madrasa.
 
Kinachoendelea nchini Tanzania ambapo vurugu zimeishatokea kinaelezewa kama vurugu za kidini. Je ni kweli ni chuki za kidini au kukata tamaa kwa watu wetu? Nimejaribu kujihoji na kuhoji mantiki ya mtu ambaye ni kiumbe dhaifu kuliko vyote kuwa tayari kuua hata kuuawa eti kwa ajili ya ima dini au Mwenyezi Mungu. Nashindwa kuelewa kutokana na ukweli kuwa Mungu hafi ila binadamu anakufa. Je hapa wahusika hawasemi ukweli kuwa wanapambana kupata maisha bora kwa wote kwa kutumia mgongo wa dini? Kama tutamfia Mungu asiyekufa yeye Mungu atafanya kazi gani? Kwanini tufie dini zake wakati mwenyewe yupo anaangalia? Je sisi ni vichaa na mataahira au ni wajanja wenye hoja fichi? Wanangu nataka maoni yenu lau tujadili jinsi ya kulielekea hili. Maana tukilinyamazia litalimaliza taifa letu.

Narudia kuchangia hoja kama hii kwa mara ya 1000 sasa. Narudia, siku zote ukiona mtu/binadamu ana base sana maisha yake kwenye dini basi hujuwe huyo hana la kufanya au la kajawa na unafiki. Huwezi ku base dini kuwa msingi wa maisha yako hata siku moja. Huko Misri leo hii (19/10/2012) waarab waliandamana kutaka mfumo mpya wa serikali yao na HAWATAKI serikali yao iendeshwe kiislam, tujiulize kwa nini? Mfumo wa dini ya kiislam umepitwa na wakati kwani wao wanataka nchi zao ziendeshwe kwa kanuni za Quran. Quran ni kitabu cha karne ya 6, hii ni karne ya 21. Kwa sasa tuna umeme, computer, TV, magari, bakery za kutengenezea mikate si zile za karne ya 6, na vitu kibao tu ambavyo vimekuja kutokana na maendeleo. Sasa tujiulize, hivi ni haki kweli kumkataza mwanamke asiendeshe gari? Kila mwanadamu ana haki ya kuishi anavyotaka na kuishi kwa kanuni za Quran ni sawa na usoshalisti....kumyima mtu haki yake. Binadamu yeyote anayekuwa hana la kufanya anajawa na fikra potofu kuwaza yasiyowezekana kama vile kuwa rais wakati ana elimu tu ya Quran, ama kuwa Mbunge umiliki gari na kuoa wanawake wengi wakati hata kuandika hujuwi na ndipo hapa unakuta uchawi unashamiri kwani waliosoma wakigombania ubunge dhidi yako, wewe unaenda kuwaroga wasishinde ushinde wewe ili upate kula. Sasa mtu kama huyu leo hii aje achaguliwe kuwa mbunge mnafikiri atatunga sheria gani. Ukija kwa hawa waandamanaji, utakuta wengi wao hawana elimu na wako katika lile kundi la wanafiki kwani illiteracy kujumulisha na ujinga unapata ya Mbagala na zanzibar.
 
Kinachoendelea nchini Tanzania ambapo vurugu zimeishatokea kinaelezewa kama vurugu za kidini. Je ni kweli ni chuki za kidini au kukata tamaa kwa watu wetu? Nimejaribu kujihoji na kuhoji mantiki ya mtu ambaye ni kiumbe dhaifu kuliko vyote kuwa tayari kuua hata kuuawa eti kwa ajili ya ima dini au Mwenyezi Mungu. Nashindwa kuelewa kutokana na ukweli kuwa Mungu hafi ila binadamu anakufa. Je hapa wahusika hawasemi ukweli kuwa wanapambana kupata maisha bora kwa wote kwa kutumia mgongo wa dini? Kama tutamfia Mungu asiyekufa yeye Mungu atafanya kazi gani? Kwanini tufie dini zake wakati mwenyewe yupo anaangalia? Je sisi ni vichaa na mataahira au ni wajanja wenye hoja fichi? Wanangu nataka maoni yenu lau tujadili jinsi ya kulielekea hili. Maana tukilinyamazia litalimaliza taifa letu.

Nadhani waislamu wameingiliwa. Inawezekana labda kuna kikundi kinachotumiwa na serikari ya Tanzania/Kenya au CIA (Afrika mashariki) kuwashawishi waislamu kuanzisha mijadala itayowapelekea kufanya fujo, na kwa sababu wao wanaongozwa na kulipiza visasi kwa kuua, basi ni rahisi kunasa kwenye mitego, na wakishanasa hiyo mitego yao ya fujo serikari itaingilia kati na hapo sasa ndipo unashuhudia itakuwa rahisi kuwakaribisha CIA au anti terrorist act. Mi ningewashauri waislamu wasinge choma makanisa, na waelimishane!
 
Back
Top Bottom