Vurugu Tunduma 88 watiwa mbaroni

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,833
155,780
Vurugu Tunduma 88 watiwa mbaroni
*Ndugu wa marehemu wagoma
mwili wake kuchunguzwa




WATU 88 wanashikiliwa kwa tuhuma za kushambulia kituo cha Polisi baada ya kutokea mauaji ya mfanyabiashara mmoja wa mjini hapa, Bw. Frank Mwachemba. anayedaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi.


Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Bw. Advocate Nyombi alisema ulinzi umeimarishwa katika eneo hilo kutokana na vurugu hizo.


Aliwataka wananchi wa mji wa Tunduma kuacha kufanya fujo na kujichukulia sheria mikononi yanapotokea matatizo kama hayo badala yake wasubiri vyombo husika.



Alisema katika vurugu za jana kulikuwa na kundi la watu ambao waliokuwa wakirusha mawe eneo la Benki ya NMB. Katika tukio hilo kijana mmoja aitwaye Eliud Sikalumbe (19) mkazi wa Mpuyi, Mbozi alijeruhiwa kwa risasi mkononi na mkononi na polisi waliokuwa wakijihami.


Alisema kuwa kijana huyo amelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi.

Akizungumzia kuhusu askari aliyetuhumiwa kuua alisema Jeshi lake bado linafanya uchunguzi zaidi wa tukio hilo kwani linahitaji muda wa kutosha.

“Nipeni muda tukio hili bado linafanyiwa uchunguzi ukikamilika tu nitawapa taarifa kamili," alisema Kamanda Nyombi.

Aidha Kamanda Nyombi alisema wakati akiondoka Tunduma saa 5 asubuhi mwili wa marehemu ulikuwa unafanyiwa uchunguzi katika hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi na kwamba baada ya uchunguzi utakabidhiwa kwa ndugu zake kwa maziko.

Hata hivyo habari ambazo gazeti hili limezipata zinasema ndugu wa marehemu wamegoma mwili huo kufanyiwa uchunguzi baada ya kutokuwa na imani na madaktari na Polisi waliopelekwa kuufanyia uchunguzi hivyo kulazimika
kuahirisha shughuli hiyo.

Juzi wananchi hao waliandamana na kushambulia magari wakishinikiza Jeshi la Polisi kuwajibika baada ya mmoja wa askari PC Justin kudaiwa kumpiga risasi mfanyabiashara huyo, mita 50 kutoka nyumbani kwake kwa tuhuma za ujambazi.


SOURCE: MAJIRA
 
Maajabu ya Jeshi letu la Polisi, Double standards za hali ya juu sana ona hii,
kosa lililotangulia kufanyika ni mauaji na kosa zito ni mauaji aliyefanya/waliofanya kosa hilo hawajashikwa mpaka sasa kisa "jeshi lake bado linafanya uchunguzi zaidi wa tukio kwani linahitaji muda wa kutosha." Askari waliokuwa zamu wanajulikana, waliomfukuza marehemu wanajulikana, kwamba alipigwa risasi hakuna ubishi, kwamba askari walikuwa na silaha na si risasi zote zimerudi armoury inajulikana, kwamba marehemu alikufa kwa majereha ya risasi inajulukana sasa upelelezi gani unatakiwa au kinachofanywa ni kuficha upelelezi?

On the other hand kundi la watu limevamia kituo cha polisi baada ya mauaji (kosa sio kubwa kama mauaji na limetokea masaa baada ya mauaji), mabomu ya machozi yamerushwa ( therefore visibility poor) utambuzi hafifu etc, a pure case of mob justice lakini wameshikiliwa na polisi tayari a few minutes after offence. Looks weird sort of.

By the way wanajeshi waliompiga traffiki tume iliyoundwa kuchunguza imetoa taarifa maana its more than a month
 
Back
Top Bottom