Pale Namanga kuna sheli ya BigBon iko barabarani kwa nyuma yake amepakana na nyumba za wanakijiji, sasa yeye anadai kanunua hilo eneo lote na anamiliki hati wanakijiji wamesema hawamtambui wala hawajawahi kuuza kwa mtu eneo hilo, kesi ilikwenda baraza la ardhi kwa mbinu na hila akafanikiwa kushinda kwani baraza hilo halina haki kisheria ya kusikiliza kesi hiyo.Mambo mengine mleta Mada kachanganya habari. Mosi kulikuwa na Uvunjaji wa nyumba hapo Namanga- Tegeta kwa hiyo kulikuwa na Mabaunsa waliokuwa wakifanya fujo ndipo Polisi wakaingilia kati. Kupita kwa Rais hakuna uhusiano na tukio hilo
Nikweli kabisa,Ni eneo la Tageta-Namanga ni mbele kidogo baada ya kutoka njiapanda ya kwenda wazo kama unaenda bunju,kuna maeneo kuna petrol station,ndipo JK kaonja chungu ya watanzania.
Anaelekea msitu wa PANDE
Mbeya waliupopoa na si kuuzuia. Halafu baada ya king'ora huwa yanafuata magari kadhaa ya polisi pamoja na yale ya wanausalama kabla ya gari la rais. Zaidi ya yote ili hilo liwezekane ni lazima watu wajue kwamba Rais atapita hapo mahali na wajipange kwa ajili ya kuuteka huo msafara. But is not easy man.mbona laisi tu!,umesahau mbeya?Watu hufanya taiming ikisha pita kile king'ola watu wanaingia barabarani na ndicho walichofanya leo.
Eeeh mabwepandemh..mkuu unamaaana kuangalia kule alikopigiwa dokta au? kazi ipo
Wee lijamaa kumbe hamnazo kabisa! Mbona unauliza swali lilelile nililouliza mimi? Mimi nimeuliza ni nani aliwaambia kama rais atapita hapo? Na wewe unauliza wangeanzaje bila kujiorganize? Hofu yangu ilikuwa ni namna gani wamejiorganize kiasi cha kuweza kujipanga kufanya hayo, na wangewezaje kufanya hayo bila vyombo vya usalama kujua? Sometimes tupunguze ukurupukaji.Kilahunja, hapa alichouliza ni kuwa msafara utazuiwa vipi? nilichojibu ni namna ambavyo unaweza kuzuiwa... ni lazima kuwa hao waliotaka kuzuia walikuwa wame ji organize, yaani kwa akili yako Kilahunja inaweza tokea tu from nowhere watu wakazuia msafara bila kuamua kwa pamoja kufanya hivyo? acha udwanzi bana!!
Hivi msafara wa rais mnauzuiaje? Hapa bado nahitaji technical explanations za namna ambavyo hili limefanyika.
Mmmh, sijui maana kwa ule msafara wa Rais unavyokuwaga, sioni kabisa hiyo nafasi ya wananchi kuweza kusimama tu barabarani na kuzuia, otherwise waliambiwa kwamba Rais angepita maeneo hayo. Na sijui wakati wa kuzuia barabara walianzaje, ina maana walizuia na magari ya kawaida? Anyway sijui, but nafikiri ni jambo gumu sana, bora mngesema wameupopoa kwa mawe, lakini si kuzuia.
Msangi hakuwepo kwenye msafara?