Vurugu Tegeta, msafara wa JK waathirika pia (Dar)

Ni kweli niko maeneo hayo na mabomu yamelia kwa muda kama dakika kumi hivi na kwa sasa yametulia
 
Watu wasiojukikana walikuwa na nia gani wamezuia msafara wa Rais uliolukuwa unapita maeneo ya Namanga.

Watu hao walizuia kwa muda wa sakika kadha hivi kabla ya FFU kutinga maeneo hayo na kuwatimua na ndipo msafara ukapita mpaka sasa FFU wapo kwenye purukushani ya sombasomba maeneo hayo ya namanga.

Chanzo Nimepita hapo muda sio mrefu.

Ni aibu kwa raisi JK kuendelea kupata shida kwenye safari zake mikoani!
Mbeya msafara wake ulipigwa mawe,msafara mwingine ukapata ajali na sasa huu unazuiwa na wananchi!!
Ukifanyika utafiti wa rais gani anaongoza kwa kuchukiwa tangu uhuru JK anaweza kuongoza!
 
Nikweli kabisa,Ni eneo la Tageta-Namanga ni mbele kidogo baada ya kutoka njiapanda ya kwenda wazo kama unaenda bunju,kuna maeneo kuna petrol station,ndipo JK kaonja chungu ya watanzania.
 
Pengine ni kwa sababu usalama wa Watanzania mdogo hasa wagonjwa mahospitalini na wale wanaodai haki zao.
 
Hivi msafara wa rais mnauzuiaje? Hapa bado nahitaji technical explanations za namna ambavyo hili limefanyika.
 
Kuzuia barabara hakuna utaalam kaka,ni kujipanga tu kukata barabara.period
Mmmh, sijui maana kwa ule msafara wa Rais unavyokuwaga, sioni kabisa hiyo nafasi ya wananchi kuweza kusimama tu barabarani na kuzuia, otherwise waliambiwa kwamba Rais angepita maeneo hayo. Na sijui wakati wa kuzuia barabara walianzaje, ina maana walizuia na magari ya kawaida? Anyway sijui, but nafikiri ni jambo gumu sana, bora mngesema wameupopoa kwa mawe, lakini si kuzuia.
 
watu wasiojukikana walikuwa na nia gani wamezuia msafara wa rais uliolukuwa unapita maeneo ya namanga.

Watu hao walizuia kwa muda wa sakika kadha hivi kabla ya ffu kutinga maeneo hayo na kuwatimua na ndipo msafara ukapita mpaka sasa ffu wapo kwenye purukushani ya sombasomba maeneo hayo ya namanga.

Chanzo nimepita hapo muda sio mrefu.


...''liwalo na liwe''....
 
Back
Top Bottom