Vurugu: Polisi na wanachuo wa Tumaini Makumira

Wakati mwingine tunaweza tukawa tunawalaumu polisi bila sababu za msingi. Hivi mtu akigongwa na gari basi uamuzi ni kukusanyika na kupanga mawe barabarani? Halafu hii habari ina uhusiano gani na siasa?
 
Yaani kama sio Ugomvi kati ya Polisi na Machinga au Waandamaji wa Vyama,
Basi ni ugomvi kati ya Polisi na Wanavyuo, hii inamaanisha nini?
Mbona kila siku Polisi adui zenu ni haohao tu? Kwanini mnapenda kuyaonea makundi haya ambayo asilimia kubwa ni Vijana wenzenu?
Tumewakosea nini sisi Vijana enyi polisi?
Kwanini habari isiwe ugomvi kati ya Polisi na Waingiza Madawa ya Kulevya au Mafisadi??
 
Majambazi waliovaa sare za kaki na kupata mafunzo ya kuua,ndo tulionao Tanganyika...bora hata jeshi la kikoloni kuliko hili la walamba viatu kapuku kama mie,wanalala kwenye mabanda kama ya mbwa koko na bado wanatugeukia wananchi
 
Sasa mabomu ni kwasababu gani. Mi nasemaga hawa polisi wetu sio watanzania.
Kuna mwanajeshi m1 nilikuwa naongea naye leo akasema huwa wanatamani raia wafanye fujo ili waruhusiwe kuja kuwapiga. By the way hii avator yako huwa inaivunja mbavu.
 
Naripoti habari hii nikiwa katika eneo la tukio,hapa ni vuta nikuvute baina ya polisi na wanachuo wa chuo cha Tumaini Makumira,hii inatokana na mwanachuo EMMANUEL ULOMI kugongwa na kosta katika geti la chuo na .
 
Naripoti habari hii nikiwa katika eneo la tukio,hapa ni vuta nikuvute baina ya polisi na wanachuo wa chuo cha Tumaini Makumira,hii inatokana na mwanachuo EMMANUEL ULOMI kugongwa na kosta katika geti la chuo na .

na...amefariki??

wanavutana nini?? mabomu yapo au yamekwisha, lete taarifa huku tukisubiri mvutano wa kesho wakati wa Mhe. Lema atakapowasili Mahakamani kwa mara nyingine tena.
 
unanekana kuweweseka hujamalizia....huyo denti kapoteza maisha? hao polis wameingiaje hadi sasa wanapigana...wanafunzi wanataka matuta au vipi?
 
Poleni sana polisi wamengieaje tena hapo wakati costa ndio tatizo hebu tupe info vizuri.
 
Hii nchi siku hizi haina uogozi? Mbona kila mtu anaona bora ajichulie majukumu ya kujiogoza mwenyewe?
 
Uongozi wa chuo pamoja na serikali ya wanafunzi kwa muda mrefu sasa umekuwa ukiomba serikali kuwajengea matuta katika eneo la geti kwani magari yamekuwa yakipita kwa kasi kubwa sana bil mafanikio.ni kwa muda sasa tumekuwa tukishuhudiaa wenzetu wakigongwa na kupata ulemavu.mwaka jana aligongwa mwanafunzi anaye itwa Rajabu lakiniyeye alinusurika kufa,leo hii tumeshuhudia Emmanuel Ulomi akifariki baada ya kugongwa na kosta itokayo Arusha kwendda Moshi.Wanachuo wameamua kulala barabarani na kazi ipo.
 
Mmmh wiki hizi zitakuwa ngumu sana sana natabiri magumu zaidi
 
Washazama ndani ya chuo,wanasababisha tu

Mkuu! Tupe UPDATES ya hapo chuoni,maana hawa polisisisiem ni kwamba wameamua kuwa ni makada wa chama tawala na siyo wa kulinda raia na mali zao kwa uadilifu tena na naona wamekuwa wa mrengo mmoja na kwa hali hii hakika hatufiki. davestro! Tujuze Mkuu wangu!
 
It is not enough to say we must not wage war. It is necessary to love peace and sacrifice for it - MLK Jr
 
hii sehemu kwa kweli inahitaji matuta,gari zinapita speed mno na kwa hali hii watatuua wengi.
 
Huyo mwanafunzi ni wa chuo inaonesha .................

Faiza unakila haki ya kuheshimiwa na unapaswa kulipa heshima hiyo....je huyu ni mtu wa kwanza mtu mzima kugongwa barabarani? Je kila mtu mzima anaegongwa barbarani ni mlevi?

Tuache dharau na ushabiki inapokuja suala muhimu la maisha ya mtu...tutanie yote lakini sio uhai wa mtu



"Nothing in all the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity"....MLKJr
 
Back
Top Bottom