vurugu mdahalo wa katiba ubungo leo

kuna kundi lilikuja kuzomea watu halafu kituoni ubungo kuna jamaa amenusurika kupigwa kisa alichangia mdahalo wa katiba ila kuna walizuia jamaa kupigwa
 
Inasikitisha kuona kuwa Watanzania wanakosa uvumilivu wa hata kusikiliza maoni ya watu wengine ambayo yanatofauitiana na wao. kama wewe hutaki kusikiliza wengine, kwa nini wengine wakusikilize wewe?
 
mzee chipaka ndo alichafua hewa mlepamojana yule kijana aliyesema ametokea pemba
 
Serikali lazima ifahamu kwamba CDM ni chama cha upinzani na kinatakiwa kupewa ulinzi wa hali na mali na vyombo vya usalama na sio kuzalilishwa ambako tunashuhudia. Fisadi papa na genge lako mtalipa haya, oneni yaliyomkumba swaiba wenu aliyewahonga magari ya kifahari aliambulia kujificha kwenye mtaro wa maji machafu nyinyi mtakimbilia wapi?
 
Yule ni Mwenyekiti wa Tadea nakumbuka hata jana alikuwepo kwenye mdahalo uliofanyika Peacock hotel na leo tena kahamia ubungo kuleta pumba zake akaanza kung'ang'ania na mic ndo wadau wakataka kuzaa naye...logic ni kwamba unatakiwa kusoma 'mood' na move ya hadhira popote pale ulipo...akaanza kunya pumba,isome hadhira mapema vinginevyo usishangae watu wanakuacha peke yako kwenye vikao...mzee amejishushia heshima yake hata mvi zake zikawa kama manyoya ya kanga
 
kweli yule dogo wa Pemba, amekosa ustaarabu wa kuongea katika majukwaa. imagine ingekuwa kenya upo kwa wajaluo na wewe ni mkikuyu halafu useme huwapendi? kweli watz bara wamemshangaa halafu wakamwacha, akajiona *****..
 
Yule ni Mwenyekiti wa Tadea nakumbuka hata jana alikuwepo kwenye mdahalo uliofanyika Peacock hotel na leo tena kahamia ubungo kuleta pumba zake akaanza kung'ang'ania na mic ndo wadau wakataka kuzaa naye...logic ni kwamba unatakiwa kusoma 'mood' na move ya hadhira popote pale ulipo...akaanza kunya pumba,isome hadhira mapema vinginevyo usishangae watu wanakuacha peke yako kwenye vikao...mzee amejishushia heshima yake hata mvi zake zikawa kama manyoya ya kanga
 
Tuwe makini na hii midahalo kwani inaonyesha wazi kuwa inapendelea upande mmoja, hata waandaaji nao wanaonesha wazi kuwa nini wanataka wananchi waamini matakwa yao, kwa nn mnakataa kusikiliza mawazo ya wanaotetea upande wa serikari? C ni mawazotuu au Mnadhani ccm hakuna wanaoiunga mkono'? Au katiba iliyopo hakuna wanaoiunga? , Hawa wakina Kibamba hawatendi haki kbs Kwanza yeye anapohimiza wananchi waingie barabarani kupinga muswaada kusomwa mara ya pili kwani anauhusiana nini na majukumu ya bunge? Kweli msipokuwa makini katiba ijayo itakuwa na mapungufu makubwa kuliko hata iliyopo sasa na itadumu kwa muda mfupi sana,, maana naona ushabiki wa vyama ndo umetawala kuliko kuangalia matatizo yaliyopo. angalieni sana Tanzania ni yetu sote. Na nina imani Wenye mamlaka watazingatia maoni ya wengi lakini Ushabiki achane kila mtu ana haki ya kutoa mawazo yake mahala popote na mujibu wa sheria.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
kale kajamaa kanatafuta umaarufu hata ukiangalia malumbano ya hoja lazima ukaoe.......kajamaaa ka pemba
 
Back
Top Bottom