Vurugu korogwe.!

yawezekana poliCCM wako bize kuandaa movies, ni wasanii wazuri sana siku izi wa kubadili uongo kuwa ukweli wakiongozwa na Sterling kova, maana wamejiondoa katika masuala walosomea ya kupambana na uarifu na sasa wanaangaika namna ya kuisafisha Ikulu, TISS dhidi uarifu na uaramia wanaowafayia watanzania

Tunahitaji kutumia FORENSIC SCIENCE... Nchi Nzima

The best way ya kuwakamata hawa wezi wa sasa ni Forensic Science - badala ya kula pesa; ni kuapgrade POLICE
 
idumu chit chat....
maana kule tunapost mada iliyo kamili sio huku sihasa wanapost mada imevaa bukta....


hili jukwaa nalipenda, lanipa raha! kila mtu hupost chake, kwa muda wake. ni sawa na kule kwetu chi chat! kwi kwi kwi!
 
kwa hiyo wamemuua msamaria mwema aliyeenda kuripoti?
pamoja na kuwa polisi hawa-act mara tu tukio linaporipotiwa lakini haina maana kuwa bodaboda wachukue sheria mkononi...(na hili limekuwa ni tatizo kubwa ya hawa boda boda, kuchukua sheria mkononi....)

na mamlaka husika inajua tatizo hili imetulia tu sijui inaona raha au inafurahia.....

kwa ufupi...polisi na bodaboda ni janga la taifa....





Nikweli kabisa, zaidi ya masaa mawili na nusu hali ya Korogwe haikuwa nzuri kabisa.

Ndani ya wiki moja kuna matukio ya wandesha boda boda kuuawa na kunyanganywa pikpiki. Hadi jana alishakufa mmoja na watatu ni majeruhi. Matukio yote hayo polisi hawakuwahi kuchukua hatua yoyote, hata ule upelelezi wa awali tu. Achilia mbali matukio km haya yameshatokea nyuma na hakuna kilichofanyika.

Sasa waendesha boda boda wakpata taarifa kuwa kuna msamaria mwema aliyetaka kuuziwa pikipiki ya wizi ameenda kuripoti polisi, so wakaanza kufuatilia kimya kimya. Walipopata taarifa kuwa yuko polisi., wakafuata huko, wakakuta ndo anahojiwa kuwataja wenzie, alipowataja tu, wakmvamia wakamchukua kwa nguvu mikononi mwa polisi, wakapiga hadi kuua, then wakmfunga nyuma ya pikipiki wakaburuza mji mzima.

Then wakaanza kuwasaka wengine, wakampata wa pili, wakafanya vivyo hivyo. Then wakawapeleka kwenye uwanja wa Chuo cha ualimu korogwe wakawachoma moto hadharani.

Polisi walijaribu kutuliza na kupiga risasa kutawanya watu haikuwezekana. Karibu mtaa yote ya Kor kulijaa watu na waendesha pikipiki wakifanya msako wa watuhumiwa. Kwa hiyo hali haikuwa nzuri kabisa. Kuna raia wasio na hatia waliojeruhiwa na wako hospitali ya wilaya.

Hadi naandika hapa mtuhumiwa wa3 amekamatwa but amenusurika kuingia mikononi mwa hawa boda boda wenye hasira. Tena ni mwanadada.

I see acheni, usiombe kushuhudia mambo haya. Japo walifanyiwa haya ni wezi lakini!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Na hii ni kutokana na uzembe wa jeshi letu la polisi kutokuwa makini na kazi zao, na kutofuatilia haki za wanyonge.
 
huko korogwe kimenuka kweli
mtu moja wa bodaboda alichinjwa kama kuku,sasa waendesha bodaboda wakawa either wanawafahamu au wanawahisi waliofanya tukio,wakawakamata hao watu mchana peupe na kuwapiga visu baada ya kuwaua wakaanza kuwavuta na pikipiki hapo mjini wakiwa uchi wa mnyama na kwenda kuwachoma moto.gari za polisi toka tanga tanga zimeenda hapo korogwe.

kama unamtu unamfahamu hapo korogwe wewe mvutie tu waya
 
Dhambi ni lazima ikemewe,
Dhambi ikiachwa humgusa kila mtu,
Ubaya wa dhambi,
ni tabia yake ya kupatiliza,
huwaingiza waliokuwemo,
na wasio kuwemo.

Dhambi ya mtu mmoja,
ina uwezo wa kuangamiza taifa zima,
chuki ya mtu mmoja,
ina uwezo wa kuangamiza taifa zima,
Hasira ya mtu mmo in uwezo wa,
kuleta chuki taifa zima.

Ona dhabi ya rushwa,
inavyotufanya kwa nguvu kila siku,
tunadharirishwa katika nchi yetu.

Ona dhambi ya uongo ituangamizavyo,
uongo ni mtaji wa utajiri,
uongo ni dira ya taifa,
uongo una abudiwa na viongozi wetu?

ona dhambi ya wizi itutuavyo umasikini,
kuiba ni ujanja,
kuiba ni kuchngamka,
maaskofu wanaiba,
masheikh wanaiba,
rais anaiba,
mawaziri wanaiba,
Wengi wanatamani kuiba ili waukate.

ona dhambi ya uchoyo,
Magari 20 ya nini,
wakati barbara zenyewe hakuna?
mtu ana vimada 100,
lakini bado anatongoza wake za watu?
Unaiba pesa,
huwekezi popote,
unazificha Ulaya,
sasa uliiba za nini??
utazitumia lini?
Unamkataba na Mungu?

Dhambi,
inavyotafuna maendeleo yetu.

Ni lazima tukemee dhambi,
tena tukemee,
kwa nguvu na akili zetu zote,
au tuwe tayari kumwaga damu,
za wakosefu na wema pia.

Dhambi mkataba wake unasainiwa kwa damu.
 
Mwanzo wa kuwa taifa lisilo na utawala kama Somalia na DRC. Serikali na vyombo vyake inapokwenda likizo wananchi wanakuwa hawana la kufanya bali kujijali wenyewe namna wanavyoweza. Matokeo sote tunayajua. CCM na serikali yake walipotufikisha ni pabaya mnooooooooooo!!!!!!

Ni kweli kabisa Ruge Opinion, tunakoelekea ni kubaya sana sana.
Na serikali isipobadilisha mfumo wwake wa utawala, tutauana sanaa
 
kwa hiyo wamemuua msamaria mwema aliyeenda kuripoti?
pamoja na kuwa polisi hawa-act mara tu tukio linaporipotiwa lakini haina maana kuwa bodaboda wachukue sheria mkononi...(na hili limekuwa ni tatizo kubwa ya hawa boda boda, kuchukua sheria mkononi....)

na mamlaka husika inajua tatizo hili imetulia tu sijui inaona raha au inafurahia.....

kwa ufupi...polisi na bodaboda ni janga la taifa....

Hapana aliyeuawa si msamalia mwema, ni mtuhumiwa baada ya msamalia mwema kwenda kuripoti na kuwezesha kuatikana mtuhumiwa.

Ni kwel kabisa pamoja na kwamba hawa ni waarifu but kifo kilivyowakuta kwa kweli ni humiliation ya hali yajuu. Maana waliburuzwa kama walivyozaliwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom