Vuguvugu la Mabadiliko: CHADEMA kuwasha moto Monduli

SEBM

JF-Expert Member
Mar 7, 2012
495
325
Katika kuendelea kueneza elimu ya Uraia, kuimarisha Chama na kueneza dhana ya Vuguvugu la Mabadiliko(M4C), na kuzindua Ofisi ya Chama Kata, viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wikiendi hii watafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Mji Mdogo wa Mto wa Mbu ulipo jimboni Monduli.

Mkutano huo utakaoongozwa na Wabunge (Wah. Mch. Natse, Nassari na Gekul) na Viongozi wengine, unategemewa kuufanya mji huo na kata zake jirani za Esilalei, Makuyuni na Majengo kuwa ngome ya CHADEMA jimboni humo.

Wananchi wengi wamejaa hamasa ya kutaka kusikia ujumbe huu wa mabadiliko na nyumba nyingi za maeneo ya Korea, Kisutu, NHC(Shirika), Sabato, Jangwani, Magadini na Kigongoni zimeonekana kupambwa kwa bendera za CHADEMA.

Hata hivyo, kuna habari kwamba vijana kadhaa wanaoendesha Bodaboda ambao walijipanga kuupokea msafara wa viongozi wa Chama kutoka Kata ya Makuyuni(umbali wa Kilometa 35) wamezuiliwa kufanya hivyo.

Nitawapasheni kinachojiri LIVE kutoka mkutano huo na kuwawekeeni picha.

NGUVU YA UMMA
 
Boda boda hazijazuiwa na mapokezi yapo pale pale,tutaondoka Arusha saa nne asubuhi.Baada ya Monduli tunaelekea wilaya ya Ngorongoro
 
CHADEMA watamfanya Mr. White Head akapelekwa Apollo kwa pressure
 
Pamoja,Monduli mjini tuna jiandaa kufika mtoambu mapema sana naku endeleza arakati.vijana wa mstari wa mbele Monduli mjini.
 
Angalien sana Lowassa asiwape hela, mambo yake amezoea kutoa rushwa!
 
kazi nzuri......wakati wao wanazidi kuumbuana nani gamba,sisi tumwage sera zetu
 
PAMOJA SANA MAKAMANDA MI MWENYEWE HAPA A. town nafikiria kufika kwenye huo mkutano wa M4C
 
Huyo mzee anaweza akatemana na ccm na kuingia cdm any time. Yani sasa hivi ccm wakimzingua ndio ya mwisho. Oohoo!
 
Katika kuendelea kueneza elimu ya Uraia, kuimarisha Chama na kueneza dhana ya Vuguvugu la Mabadiliko(M4C), na kuzindua Ofisi ya Chama Kata, viongozi waandamizi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wikiendi hii watafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika Mji Mdogo wa Mto wa Mbu ulipo jimboni Monduli.

Mkutano huo utakaoongozwa na Wabunge (Wah. Mch. Natse, Nassari na Gekul) na Viongozi wengine, unategemewa kuufanya mji huo na kata zake jirani za Esilalei, Makuyuni na Majengo kuwa ngome ya CHADEMA jimboni humo.

Wananchi wengi wamejaa hamasa ya kutaka kusikia ujumbe huu wa mabadiliko na nyumba nyingi za maeneo ya Korea, Kisutu, NHC(Shirika), Sabato, Jangwani, Magadini na Kigongoni zimeonekana kupambwa kwa bendera za CHADEMA.

Hata hivyo, kuna habari kwamba vijana kadhaa wanaoendesha Bodaboda ambao walijipanga kuupokea msafara wa viongozi wa Chama kutoka Kata ya Makuyuni(umbali wa Kilometa 35) wamezuiliwa kufanya hivyo.

Nitawapasheni kinachojiri LIVE kutoka mkutano huo na kuwawekeeni picha.

NGUVU YA UMMA

​Hivi CHADEMA wanelewa maana ya elimu ya URAIA?
 
Boda boda hazijazuiwa na mapokezi yapo pale pale,tutaondoka Arusha saa nne asubuhi.Baada ya Monduli tunaelekea wilaya ya Ngorongoro

Mkuu Nanyaro Ephata tunaomba utupe ratiba ili tujue tunajipanga vp! Yaani lini mtakuwa Mto wa mbu na lini mtakuwa Ngorongoro!
 
Code:
Hata hivyo, kuna habari kwamba vijana kadhaa wanaoendesha Bodaboda ambao  walijipanga kuupokea msafara wa viongozi wa Chama kutoka Kata ya  Makuyuni(umbali wa Kilometa 35) wamezuiliwa kufanya hivyo.
Hakuna kinachoweza kubadili maamuzi vichwani mwa watu!
Utawakataza kuendesha boda2, watakuja kwa baiskeli au magari au miguu.
 
Back
Top Bottom