Vua Gamba Vaa Gwanda, Ndani ya Ukonga Jumamosi hii 19/05/2012

Nilikuwa nataka kuja kwenye huo mkutano nimeishia pale Moshi bar nimerudi barabara mbovu sana...jimbo la Matola
ritz labda nikusahihishe, hilo jimbo la Ukonga linaongozwa na mbunge wa CCM Mwanamke mmoja anaitwa sijui Eugine Mwaiposa, pili hiyo kata kunakofanyika huo mkutano Diwani wake ni Jery Silaa na ambaye ndio meya wa Ilala, sasa nashukuru kwa kutupa taarifa kwamba kumbe kata anayoishi meya wetu hata barabara ni mgogoro, kwahiyo Mimi kama Matola mkazi wa jimbo la Segerea sitegemei maendeleo yoyote kutoka kwa viongozi hawa wa CCM.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu usichanganye.Mkutano wa leo upo hapa Ukonga mazizini na mkutano wa Jumamosi ni wa kitaifa Jangwani.Nipo mkutanoni nitawapa updates kadiri inavyowezekana.

Nnakushukuru kwa ufafanuzi kaka
 
Wadau mniwie radhi kwa kutowapa updates, nilikuwa na majukumu ya kusimamie protocal ya mkutano.

UKONGA YATAKA SHIBUDA ATIMULIWE!
Katika hali ambayo haikutarajiwa viongozi pamoja na wanachama wote wa Chadema waliohudhuria mkutano wa leo wametoa msimamo wa kutaka John Shibuda atimuliwe ndani ya chama mara moja.

Wamemuomba Mh. Suzan Kiwanga afikishe salamu hizo kwa uongozi wa Taifa na hatua ichukuliwe bila kumuonea aibu.
 
Katibu wa jimbo Juma Mwipopo: Halmashauri ya manispaa ya ilala inachukua ushuru kiasi cha sh.4,000 kwa kila ng'ombe anayechinjwa, hivyo wanakusanya sh.48milioni kila mwezi lakini machinjio ni machafu na barabara ya kuingia machinjioni haipitiki.
 
Mwita Waitara: Katiba mpya si agenda ya ccm kwahiyo wameiteka agenda ya Chadema na kutaka kuwalaghai na kuwazuia wananchi kujadili na kutoa maoni yao bila vikwazo. Wananchi wawe huru kujadili juu ya nchi yao bila masharti.
Jumamosi ijayo 26/05/2012 kutakuwa na mkutano mkubwa Jangwani na viongozi wa taifa watatoa tamko la muelekeo na msimamo wa chama katika katiba mpya.
 
Susan Kiwanga: serikali ya ccm kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi raisi ni mafisadi.
 
Sasa jukwaani yupo suzan kiwanga mbunge viti maalumu,anamwaga sera,anahimiza mwamko wa wana dar kwenye mabadiliko
 
Susan Kiwanga: serikali ya ccm kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi raisi ni mafisadi.

Kiwanga: kwa mujibu wa ripoti ya CAG raisi kikwete anavunja sheria na kukiuka kanuni za ajira kwa kuwateua wanajeshi kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, wanalipwa mishahara na malipo yote stahiki ya kisiasa lakini wakati huo huo wanalipwa stahiki zao katika ajira zao za kijeshi.
 
Amepanda Henche,anamtambulisha kijana aliyepambana na Lusinde kule moro anaitwa Lamerk, na umeme umeleta tatizo kidogo
 
Ukonga kuna mwamko sana,tatizo la umeme limetatuliwa henche anaendelea na hoja ya ugumu wa maisha
 
Sijui lakini, hawa ambao daily tunawalalamikia kuwa wameongoza nchi miaka hamsini bila mafanikio, leo eti anakaribishwa kwa mikono na miguu chamani, whats wrong with u pipo, akiwa cdm ndo atabadilika? I dont get it kwa kweli, hao waliokuwa cdm wakaenda ccm kwa madai kuwa cdm hakuna jipya wamefanya nini la maana huko? Its absurd kwa kweli kujisifia kupokea magamba, kwa nini isitafutwe ngozi inayouzika
 
Henche ni hodari sana wa kujenga hoja,anawaambia vijana wa dar wamelala sana,anarudia uteuzi wa wakuu wa wilaya wilaya ulivyofanywa kishkaji,ugumu wa maisha
 
Wadau mniwie radhi kwa kutowapa updates, nilikuwa na majukumu ya kusimamie protocal ya mkutano.

UKONGA YATAKA SHIBUDA ATIMULIWE!
Katika hali ambayo haikutarajiwa viongozi pamoja na wanachama wote wa Chadema waliohudhuria mkutano wa leo wametoa msimamo wa kutaka John Shibuda atimuliwe ndani ya chama mara moja.

Wamemuomba Mh. Suzan Kiwanga afikishe salamu hizo kwa uongozi wa Taifa na hatua ichukuliwe bila kumuonea aibu.
Suala la kutimuliwa shibuda haliko simpo kama wengi wanavyoweza kuamini. Tujifunze kutokana na yaliyojiri kwa akina Hamad Rashid na Kafulila.
Shibuda ametikisa kiberiti na chadema inaonekana wameingia kwenye mtego wake bila kujijua.
Kuendelea kumjadili ndiko anakokutaka yeye kwani anapata wasaa wa kureact, kitu ambacho ndio plan yake.

Kipindi kile alichofanya ushenzi wake halafu chadema wakakaa kimya, aliishia wapi..? Bila shaka alijiona mjinga, lakini sasa naona mmejiingiza kwenye tract yake.
Bavicha wamefanya kosa kubwa sana, huenda likaikosti chadema.
 
Susan Kiwanga: serikali ya ccm kuanzia mwenyekiti wa mtaa hadi raisi ni mafisadi.

Kiwanga: kwa mujibu wa ripoti ya CAG raisi kikwete anavunja sheria na kukiuka kanuni za ajira kwa kuwateua wanajeshi kuwa wakuu wa mikoa na wilaya, wanalipwa mishahara na malipo yote stahiki ya kisiasa lakini wakati huo huo wanalipwa stahiki zao katika ajira zao za kijeshi.
Kwa sababu huu mkutano unafanyika Dar natarajia updates ziendane na mafoto.
 
Wakuu, tunawaomba mtupiamo na picha zilete hamasa! Mh. Mwita Maranya niambie kama Mkandarasi yumo!?
 
Mwita Waitara: Katiba mpya si agenda ya ccm kwahiyo wameiteka agenda ya Chadema na kutaka kuwalaghai na kuwazuia wananchi kujadili na kutoa maoni yao bila vikwazo. Wananchi wawe huru kujadili juu ya nchi yao bila masharti.
Jumamosi ijayo 26/05/2012 kutakuwa na mkutano mkubwa Jangwani na viongozi wa taifa watatoa tamko la muelekeo na msimamo wa chama katika katiba mpya.
Huu mkutano ni muhimu sana kwa wakazi wa Dar na watanzania kwa ujumla.
Muda utakuwa saa ngapi?
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom