Vua Gamba Vaa Gwanda, Ndani ya Ruaha Kilombero,,,!!!

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,564
7,973
Wadau,
Nilikuwa napitapita huku wilaya ya Kilombero ghafla nikakutana na mkutano wa Chadema katika mji mdogo wa Ruaha Kilombero.

Mkutano unahutubiwa na viongozi wa mkoa wakiongozwa na kamanda Mh. Suzan Kiwanga (mwenyekiti wa chadema mkoa wa morogoro).

Watu kadhaa wame cross kutoka ccm akiwemo Mzee mmoja ambaye ni muasisi wa ccm ruaha amevua gamba na kuvaa gwanda. Ameshangiliwa sana na wananchi inaonekana ni mtu maarufu sana hapa ruaha.

Kwa kweli watu ni wengi sana hapa bahati mbaya tu kitu changu cha mchina camera yake mbovu ningewatupia picha.
 
Kamanda asante kwa updates.Kesho utamiss Jangwani.

Kutokuwepo Jangwani litakuwa ni jambo la bahati mbaya sana.
Nimepanga kuondoka huku kesho alfajiri ili hadi kufikia saa 3 au 4 asubuhi niwe ndani ya jiji.
M4C ndani ya dar si ya kusimuliwa!
 
Kama kweli watu wa hapo wamejitokeza kwa kiwango hicho unachosema basi safari ya ukombozi inakaribia mwishoni. Watu wa hapo walikuwa nyuma sana.
 
Mdau mmoja wa chadema ametangaza kuwalipia kadi wanachama wa ccm wanaojiunga na chadema. Kuna watu kadri ya 15 au zaidi wamevua magamba.

Sasa ni zamu ya kuwakabidhi kadi za uanachama wananchi wengine wanaojiunga ambao walikuwa wanachama wa vyama vingine pamoja na wale ambao hawakuwa wanachama wa chama kingine chochote hapo kabla.
 
Kama kweli watu wa hapo wamejitokeza kwa kiwango hicho unachosema basi safari ya ukombozi inakaribia mwishoni. Watu wa hapo walikuwa nyuma sana.

Mzee wa Kilosa hawa jamaa zako wa ruaha wamejitokeza kwa wingi sana katika mkutano huu.
Nadhani viongozi wa kilombero wamefanya kazi nzuri sana ya kuwahamasisha wananchi wa eneo hili.
 
Waliojiunga na chadema toka ccm ni watu 25 na wengine watano kutoka ccm-b.

Wasiokuwa na vyama bado wanaendelea kuchukua kadi na mstari bado ni mrefu!
 
Mkuu pole na majukumu! Nakupongeza kwa kuendelea kutuhabarisha habari za huko! Hii m4c haita bakiza mtu! Ni kimbunga cha ukombozi kilichoikumba Tz. Nakuhakikishia mwaka 2015 hata wakiiba, hazitawatosha!
Tumeanza na Mungu, tutamaliza na Mungu. Wao wana nguvu, sisi tuna Mungu! Hakuna kulala hadi kieleweke. Nakuombea ufike salama Dsm kesho utupatie updates kama hizi! Pamoja daima.
 
Mura Mwita mbuya ohoyire

Mbuya tata Power.
Nimeambiwa huu ni mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa katika eneo hili la Ruaha ambao unafanyika jumapili 27/05/2012.

Kamanda Susan Kiwanga amewaomba wananchi washiriki kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya mawakala wa chadema na kiasi cha sh.126,100/- zimepatikana chap chap.
 
Last edited by a moderator:
Viva makamanda, mpaka mdudu FISADI wa huko CCM akasalimu amri kupisha maendeleo kwa wananchi bila wizi zaidi.
 
Mbuya tata Power.
Nimeambiwa huu ni mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa katika eneo hili la Ruaha ambao unafanyika jumapili 27/05/2012.

Kamanda Susan Kiwanga amewaomba wananchi washiriki kuchangia gharama za chakula kwa ajili ya mawakala wa chadema na kiasi cha sh.126,100/- zimepatikana chap chap.

Hicho kidogo walichotoa kina dhamani kuliko visenti vya Chenge! Hakika wametoa kwa moyo wao na Mungu atawabariki!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom