Vua gamba vaa gwanda kutingisha kusini

Tatizo la kusini hawawaamini wachaga wa kaskazini!

Hayo ni maoni yako. Umetumia uhuru wako. Yanaweza kuheshimika, lakini si lazima yakubaliwe. Je unazo taarifa kuwa wapo Watanzania wa Kusini ambao wamevuka kiwango cha kufikiria kikanda, walipanga kuandamana kuja Makao Makuu ya CHADEMA kuhoji kulikoni chama hakipeleki nguvu huko kujenga ngome nyingine wakati wanazo taarifa kuwa maamuzi yalishafikiwa siku nyingi sana? Mtabaki kusema hivyo CHADEMA inasonga mbele. Haya...
 
Tunawapongeza viongozi wetu kwa mkakati huo wa ukombozi kanda ya kusini, siku nyingi wengi wetu tulikuwa na kiu ya kuona kanda hiyo inashambuliwa kwa nguvu na mbinu zote thabiti.
 
Nassari na Lusinde nani mtoto sio riziki?.
Ilaunaonekana unamipasho kama ya yule bwenge wa CCM.
Unatokea bendi ya hadija kopa? au Ni kijana kutoka Mombasa? Let me know you as soon as you can reply

sawa kiongozii...!
Heshima yako lakin
 
hii pia iwe ajenda mana zitto alipokuwa tanga ilisema kwamba wakienda mikoa ya kusini watawelimisha wakulima jinsi wanavyozumiwa kwa bei ndogo ya korosho.
 
Tatizo la kusini hawawaamini wachaga wa kaskazini!

Hawana haja ya kuwaamini wachagga wa kaskazini. Wanachotakiwa kufanya ni kuiamini Chadema na nguvu yao katika kuleta mabadiliko ya kweli nchini. Waikatae ccm kwa vitendo na kusimamia kwa dhati maendeleo yao.
 
Nendeni mkashambulie makamanda Kuanzia rufiji,kilwa,lindi mjini,lindi vijijini,nachingwea ,liwale,ruangwa,masasi,newala,tandahimba,mtwara vijijini,mtwara mjini,nanyumbu na tunduru. Watu wapo tayari kwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda. Kazi njema makamanda
 
Wananchi wa kusini wamenyanyaswa sana na ccm kiasi cha kubaki nyuma kimaendeleo na kudhania umaskini na kulala kwenye TEMBE ni haki yao. Hongere CDM kwa kuwakumbuka wana kusini, ndoa ya ccm na cuf ilimaliza kabisa matumaini yao. Ila haitakuwa kazi rahisi inabidi mjipange kwelikweli kwa vile ujinga, umaskini na maradhi ndio mtaji wa magamba na kusini vime prevail
 
Sasa tunamalizia kuleta Uhuru wa kweli Tanganyika, tukishaiteka Lindi na Mtwara baasi CCM kwaherini
 
Mwitikio ni mzuri.SUGU YUPO RUVUMA LEO ALIENDA MADABA KESHO ATAKUA MBINGA NA JUMAPILI ATAMALIZIA HATA MUJINI.
 
Pamoja sana wakuu ,niko Tanga but nimeshatuma ujumbe kwa washkaji na jamaa zangu Ndanda na Nyangao kuwa freedom is coming wawe tayari kuvua magamba hadi mazeli nimeshamtel yaani
 
Back
Top Bottom