Vua gamba vaa gwanda: Heche aisambaratisha ngome ya Kilango Same

Nimeipenda sana hii. Tunahitaji viongozi wachacharikaji kwa ajili ya kukijenga chama. Tukaze buti, hakuna kulala hadi kieleweke!
 
Kwahiyo hayo yana uhusiano gani na shughuli za kimaendeleo hapo Same?

mushi,
sisi huku Vuathu/Upareni huwa tunaimba "mtani muagha, mtani muagha, unenya uale, unenya uale"!! sasa tukiweka utani pembeni, wananchi wa upare tumekuwa na rekodi ya kuwabadilisha wabunge mara kwa mara na mara zote tumefanya hivyo baada ya kutoridhika na utendaji wao wa kazi na kusukuma gurudumu la maendeleo. hii ni tofauti na maeneo mengine ya tanzania ambapo huchagua wabunge walewale kwa mihula mingi.
kuhusu maendeleo, wananchi wa Upare wana ari ya maendeleo na hiyo inathibitishwa na jinsi wanavyofanya kazi kwa kujitolea(tunaita msaragambo) katika mazingira magumu sana. ndiyo maana kuna watu wakifika upare wakiona barabara tulizochimba wenyewe hawaamini wanadhani ametujenge msuya!! tulichokosa sisi ni wabunge madhubuti tangu aondoke mzee wetu chediel mgonja "kaghembe."

tumejaribu kupata mbunge makini ndani ya ccm, hatukufanikiwa. sasa tunakwenda kutafuta mbunge nje ya ccm baada ya kujiridhisha kwamba mfumo wa utawala wa ccm umeoza.
 
Ndio Wasira akasema CHADEMA itakuwa baada ya mwaka mmoja ujao kwa mwendo huu.. Kweli uzee ni dawa ila kwa Wasira uzee ni ugonjwa.
 
Hivi wewe pamoja na kuwa mtu mzima hujui uhusiano wa siasa na maendeleo? Hizi ni akili za wapi wakuu?
mtu mzima vipi na miye nimetahiriwa?wewe unajuwa hilo swali nimeliuliza kwenye context gani?usidandie treni kwa mbele
 
mushi,
sisi huku Vuathu/Upareni huwa tunaimba "mtani muagha, mtani muagha, unenya uale, unenya uale"!! sasa tukiweka utani pembeni, wananchi wa upare tumekuwa na rekodi ya kuwabadilisha wabunge mara kwa mara na mara zote tumefanya hivyo baada ya kutoridhika na utendaji wao wa kazi na kusukuma gurudumu la maendeleo. hii ni tofauti na maeneo mengine ya tanzania ambapo huchagua wabunge walewale kwa mihula mingi.
kuhusu maendeleo, wananchi wa Upare wana ari ya maendeleo na hiyo inathibitishwa na jinsi wanavyofanya kazi kwa kujitolea(tunaita msaragambo) katika mazingira magumu sana. ndiyo maana kuna watu wakifika upare wakiona barabara tulizochimba wenyewe hawaamini wanadhani ametujenge msuya!! tulichokosa sisi ni wabunge madhubuti tangu aondoke mzee wetu chediel mgonja "kaghembe."

tumejaribu kupata mbunge makini ndani ya ccm, hatukufanikiwa. sasa tunakwenda kutafuta mbunge nje ya ccm baada ya kujiridhisha kwamba mfumo wa utawala wa ccm umeoza.
@bangusule, kubadili viongozi wa chama kile kile mlidhani ni solution?Bado mlikuwa inside the box.Najuwa tatizo la maji ni sugu na sidhani kama limekwishashughulikiwa.Magamba is the same, and the problems we are facing as a nation are the same.However hizi picha zina encourage,wananchi wamechoshwa,its time to burry them (ccm) once and for all
 
Back
Top Bottom