Vua Gamba imeshindikana na imefungwa rasmi - Pius Msekwa

mi napita tu maana majibu yote yako kwenye uchaguzi unaoendelea. Viongozi watoa rushwa hawana nafasi katika uchaguzi huu yaliyofanyika ni neema kwa wajumbe asiyejenga hata kigenge atakuwa ****.ehh nagu na sumaye mwe!!!
 
tatizo la kuvua gamba lilionekana mwanzo tu, walipewa miezi 3 wawe wamejitoa wenyewe. sasa hata ningekuwa mimi nisingetoka, miezi yote hiyo ningejua hapa ni fix kwa wananchi, wala nisingejigusa. labda wangesema siku 7, labda wangeshtuka , halafu hawa watu si wanakaaga vikao vyao vya giza (usiku) kupanga mikakati? kwa hiyo si wanaambiana tu,kwamba tunawatokea wananchi hivi, kaukeni tuwatoe wananchi njiani kwa staili hii.
hakukuwa na seriousness yoyote kwenye huo mkakati wanyamaze tu.
 
lowassa alisema kama issue ya richmond JK nae kahusika so kama ni kuvua gamba maana yake waanzie na ikulu kwanza ndo maana wanashindwa kuwaondoa maana gamba kuu liko white house pale.
 
Uzee dawa Asante sana Mzee Msekwa kwa kuwa muungwana!Binadamu Utu na pale unapodhibitika kuwa na mapungufu Kukiri ni moja ya njia kufikia Majawabu!
 
Tehe he he he heeeeeee.... Waliwaza nini wao kutoa tungo tegemezi "Vua gamba......" CDM tukaikamilisha, Vua gamba, vaa gwanda...
 
lowassa alisema kama issue ya richmond JK nae kahusika so kama ni kuvua gamba maana yake waanzie na ikulu kwanza ndo maana wanashindwa kuwaondoa maana gamba kuu liko white house pale.

Hapo kwenye bold ndo shida ilipo. Kuvua gamba ni sawa na kundoa gamba la kobe, lazima kobe afe, kwa hiyo ni ngumu sana.
 
Mzee Msekwa kaongea ukweli kweupe, habari ya kuvuana magamba haiwezekani CCM. Nani amvike paka kengele?
 
CCM ina survive kwa fedha chafu kutoka kwenye deal chafu za the same guys...CCM inatumia milions and milions kwenye kila kitu inachofanya. Unafikiri hiyomijihela inatoka wapi?

Wezi wanaichangia CCM, wezi hao wamo ndaniya CCM na niviongozi wa ccm.

Mbwa kala mbwa.
 
Sijaona sababu kubwa ya kumshambulia Pius Msekwa, kwa kiwango alichojibu na kueleza wazi kuwa ndani ya viongozi walioteuliwa hivi punde wamo wenye makosa ya jinai lakini Chama kimewakumbatia.

Kwa mtazamo wangu kadiri ya Msekwa hapa amejitahidi sana kueleza ukweli kimantiki, na yaelekea hajakubaliana na kinachoendelea kuwakumbatia waliwanyooshea kidole kuwavua magamba na kuishia kuwakumbatia.

Pius Msekwa amejitahidi kuweka wazi kile kinacholalamikiwa na wananchi wengi, vyama vya upinzani na wapenda mabadiliko, unataka amwage yote kwa hasira ashikishwe adabu? Hapa hapa kajitahidi sana kuonyesha uozo uliopo ndani ya CCM.

Msekwa kaamua kuueleza umma wa watanzania nchi imevamiwa wao katika uchache wao hawataweza japo na wao mwanzoni walionja mchuzi ila sasa wanaona wenzao wameamua kuchukua kila kitu na kujivika ufalme....Ametoa go ahead kwa wananchi kujaribu bahati yao wao wamenyoosha mikono.....Lakini wengine tunasema no re-treat no surrender ufisadi lazima upige goti na kukiri kwa ulimi kuwa Mungu anaishi! I for one will never bow to ufisadi come rain or sunshine!
 
Hili ni pigo kwa Nape!

Ruttashobolwa mimi naitwa mtakyamilwa-siku mbili tatu zilizopita nimetokea kaisho na vijiji vingine karibu na town hiyo. Upuuzi unaofanywa na viongozi hawa wa sism si pigo kwa Nape bali wanajua wanalolifanya-kiukweli ili ni janga la kitaifa. Niliojiana mawili matatu na wenyeji wa maeneo hayo kuhusu uchaguzi wa sism uliokuwa ukiendelea nikagundua safari ya kulikomboa taifa ili silelema. Mbali na kashifa zote zinazowaandama sism na kujivua kwa mangamba yao bado watu wanavaa kijani, wanachaguana kwa rushwa na hawaelewi chochote. kazi bado tunayo.
 
Amechoka huyu, yupo kwenye bobi ya Ngorongoro kama mkiti fikiria anendaga kila shoo
ukifikiri anatusaidiaje kuleta watalii au kuuza mlima. Mzee waposho.
 
Udhaifu huo haupo Msekwa peke yake tu, kwani hata Vasco pia ni dhaifu

Naomba mnitajie mmoja ambaye si dhaifu. Umuite mbele ya hadhara utaona wote wanajichekesha chekesha kama January na Nape walipokuwa wanahojiwa na Jenerali Ulimwengu. Hakuna hata mmoja timamu kwani wote wamekulia na kulelewa ktk mazingira yanayofanana (kubebwa bebwa tu) hakuna aliyewahi kuumiza kichwa kwa kufikiri.
 
Wanajamvi naamini wengi wetu tunakumbuka ni hivi juzi kati makamu mwenyekiti wa ccm bara ndg. Pius msekwa aliutangazia uma wa watanzania kuwa dhana ya kujivua gamba, waliyoiasisi (ccm) kwa lengo la kujaribu kurejesha imani ya wananchi kwa chama chao (ccm) haitekelezeki.

Kwa maana hiyo ya kutokutekelezeka, lengo la kujaribu kurejasha imani ya wananchi kwa chama hicho kikongwe zaidi nchini, zimeachwa zishindwe, hivyo wamewadhihirishia wapiga kura wa Tanzania kuwa chama chao (ccm) hakina mvuto na kimepoteza uungwaji mkono kwa kiwango cha kutisha kwani kimejipambanua kuwa kinahujumu uchumi wa nchi.

Ni kwa nini basi chama hiki kinatumia hila kughilibu akili za watanzania ama kwa kuwatumia cuf ama ccm wenyewe wanapojaribu kukusanya wananchi kuhudhuria mikutano yao ama ya cuf ili kuongopa kuwa wanaungwa mkono sana, Mbinu hii imekilazimu chama kuwashawishi wahudhuriaji mikutano kwa mbinu chafu ikiwemo matumizi ya mlungula tofauti na chadema kinavyoungwa mkono kwa dhati ya moyo wa watanzania wengi.

Nisikuchoshe,Kwa kuwa Pius Msekwa ameshasema kinagaubaga kuwa hakuna kuwafukuza mafisadi chamani!!!!! Yaani chama ni cha kifisadi, kwa ukweli unaofanana na huo je ni lini mwenyekiti wa ccm taifa atakiri na kuwatangazia watanzania kuwa "HAKUNA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA"

Naomba kuwasilisha.
 
wanajamvi naamini wengi wetu tunakumbuka ni hivi juzi kati makamu mwenyekiti wa ccm bara ndg. Pius msekwa aliutangazia uma wa watanzania kuwa dhana ya kujivua gamba, waliyoiasisi (ccm) kwa lengo la kujaribu kurejesha imani ya wananchi kwa chama chao (ccm) haitekelezeki.

Kwa maana hiyo ya kutokutekelezeka, lengo la kujaribu kurejasha imani ya wananchi kwa chama hicho kikongwe zaidi nchini, zimeachwa zishindwe, hivyo wamewadhihirishia wapiga kura wa tanzania kuwa chama chao (ccm) hakina mvuto na kimepoteza uungwaji mkono kwa kiwango cha kutisha kwani kimejipambanua kuwa kinahujumu uchumi wa nchi.

Ni kwa nini basi chama hiki kinatumia hila kughilibu akili za watanzania ama kwa kuwatumia cuf ama ccm wenyewe wanapojaribu kukusanya wananchi kuhudhuria mikutano yao ama ya cuf ili kuongopa kuwa wanaungwa mkono sana, mbinu hii imekilazimu chama kuwashawishi wahudhuriaji mikutano kwa mbinu chafu ikiwemo matumizi ya mlungula tofauti na chadema kinavyoungwa mkono kwa dhati ya moyo wa watanzania wengi.

Nisikuchoshe,kwa kuwa pius msekwa ameshasema kinagaubaga kuwa hakuna kuwafukuza mafisadi chamani!!!!! Yaani chama ni cha kifisadi, kwa ukweli unaofanana na huo je ni lini mwenyekiti wa ccm taifa atakiri na kuwatangazia watanzania kuwa "hakuna maisha bora kwa kila mtanzania"

naomba kuwasilisha.

duplicate news - sorry!!!
 
thibitisha!!


  • [h=6]View First Unread[/h]
  • [h=6]LinkBack[/h]
  • [h=6]Topic Tools[/h]
  • [h=6]Search Topic[/h]
  • [h=6]Rate This Topic[/h]


  • user-offline.png
    Maseto

    Yesterday 14:10
    #1
    MemberArray


    Join Date : 3rd April 2012
    Posts : 84
    Rep Power : 553
    Likes Received33
    Likes Given1


    [h=2]
    icon1.png
    Msekwa katika Jenerali on Monday (Channel 10)[/h]
    Mzee Msekwa,makamu mwenyekiti CCM, ANATOA MAJIBU YA HATARI SANA KWA CHAMA Chetu ktk kipindi cha Jenerali on Monday.

    Anasema kuwa imeshindikana kuwashughulikia wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi kwa kuwa haiwezekani kushughulikia makosa ya jinai kisiasa.

    Hajasema kama kuna mkakati wowote wa kuwaondoa na ameahidi kutoshughulikia kwa sababu hawawezi kuagizwa na wapinzani wanaosema 'vua gamba, vaa gwanda'. Kwa maöni yangu, haya majibu ni mabaya zaidi kutolewa na kiongozi wa CCM.

    Siamin kama akili yake iko sawa.


 

  • [h=6]View First Unread[/h]
  • [h=6]LinkBack[/h]
  • [h=6]Topic Tools[/h]
  • [h=6]Search Topic[/h]
  • [h=6]Rate This Topic[/h]


  • user-offline.png
    Maseto

    Yesterday 14:10
    #1
    MemberArray


    Join Date : 3rd April 2012
    Posts : 84
    Rep Power : 553
    Likes Received33
    Likes Given1


    [h=2]
    icon1.png
    Msekwa katika Jenerali on Monday (Channel 10)[/h]
    Mzee Msekwa,makamu mwenyekiti CCM, ANATOA MAJIBU YA HATARI SANA KWA CHAMA Chetu ktk kipindi cha Jenerali on Monday.

    Anasema kuwa imeshindikana kuwashughulikia wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi kwa kuwa haiwezekani kushughulikia makosa ya jinai kisiasa.

    Hajasema kama kuna mkakati wowote wa kuwaondoa na ameahidi kutoshughulikia kwa sababu hawawezi kuagizwa na wapinzani wanaosema 'vua gamba, vaa gwanda'. Kwa maöni yangu, haya majibu ni mabaya zaidi kutolewa na kiongozi wa CCM.

    Siamin kama akili yake iko sawa.



sijaona mahala panapendekeza jk naye aseme kuwa maisha bora kwa kila mtanzania hayawezekani.
 
Back
Top Bottom