Vua Gamba imeshindikana na imefungwa rasmi - Pius Msekwa

Maseto

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
944
545
Mzee Msekwa,makamu mwenyekiti CCM, ANATOA MAJIBU YA HATARI SANA KWA CHAMA Chetu ktk kipindi cha Jenerali on Monday.

Anasema kuwa imeshindikana kuwashughulikia wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi kwa kuwa haiwezekani kushughulikia makosa ya jinai kisiasa.

Hajasema kama kuna mkakati wowote wa kuwaondoa na ameahidi kutoshughulikia kwa sababu hawawezi kuagizwa na wapinzani wanaosema 'vua gamba, vaa gwanda'. Kwa maöni yangu, haya majibu ni mabaya zaidi kutolewa na kiongozi wa CCM.

Siamin kama akili yake iko sawa.
 
Msekwa hajadata bali ameonyesha utupu wake na chama chake. Nani atamshughulikia mwenzake ndani ya CCM yenye kuzama kwenye tope la ufisadi? Hakika usitegemee nyani na ngedere wafungane kwenye kesi ya wizi wa mahindi-wote wana kosa la kuiba mahindi. Nani amguse nani wasiumbuane? Msekwa ana so zake Ngorongoro sawa na Kikwete na EPA, Lowassa na Kikwete Richmond na mazabe mengine. Mnaotegemea kuwa CCM inaweza kupambana na ufisadi mnakuwa too optimistic for no reasons. CCM bila ufisadi ishakufa haina sera zaidi ya ufisadi.
 
Kuna mwananchi kauliza kwa nini ccm kuna ubadhirifu na kuna wazee kama kina msekwa wanashindwa kukemea na kama wameshindwa kwa nini wasijiuzulu?
Msekwa amejibu kuwa ccm haipo dar au dodoma pekee, kama ubadhirifu mbeya tatizo hilo linapaswa kushujulikiwa na viongozi wa mbeya.
Mzee msekwa alifika mbali zaidi na kuonyesha kuwa kashikwa na jazba na kutoa maneno makali kwa muuliza swali kwa kusema kuwa JE MUULIZA SWALI ANA AKILI TIMAMU KWELI???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ile dhana ya CCM ya kuwang'oa wakada wake wanojihusisha kwa ufisadi na rushwa imawashinda na hatimaye wamemwaga manyanga. Hayo yameelezwa na Makamu mkt TZ bara wa CCM Pius Msekwa pale alipokua akihojiwa na Generali Ulimwengu kwny kipindi cha Jeneral On Monday ndani ya Chanel 10.
Ameeleza sasa wamekuja na "singo mpya" KUJIPANGA UPYA.

Katika kipindi hicho ilionekana wazi Msekwa kushindwa kujibu maswali yalioelekezwa kwake hivyo kutoa majibu duni na yasiojitosheleza "pumba Pointi"

Bila shaka magamba wameona falsafa yao ya kuvua gamba imefeli kwny utekelezaji sababu ya kukosa nani mvishe mwenzie kengele. Kwa kweli nilitarajia ni danganya toto kama walivyozoea kuhadaa wa TZ.

Wadau napenda kuwakilisha
 
Mzee Msekwa,makamu mwenyekiti CCM, ANATOA MAJIBU YA HATARI SANA KWA CHAMA Chetu ktk kipindi cha Jenerali on Monday.

Anasema kuwa imeshindikana kuwashughulikia wanachama wanaotuhumiwa kwa ufisadi kwa kuwa haiwezekani kushughulikia makosa ya jinai kisiasa.

.

Hapo kwenye red: Msekwa anakiri kuwa ndani ya CCM kuna watu wenye makosa ya jinai lakini hawatachukuwa hatua yoyote? Kuna haja gani ya CCM kuendelea kushika dola kama hawana nia ya kusimamia sheria? Kauli ya ajabu sana hii!
 
Kwisha habari yao hawa ndo maana cuf wanajitaidi kuwasaidia hata kwa kuja kuvuna aibu zisizo na msingi huku arusha
 
Huyu msekwa ni mzee sana! lakini bado hataki kustaafu kweli hela ni noumer!
 
Hakika magamba ni kama mfa maji kamwe haachi kutapatapa. Albert Einstein alisema "problem cannot be solved by the same level of thinking that create it"

sisimu soul be rested in everlasting fire . Amen
 
pumba kama hizi nilitegemea zingemwagwa na shukuru kawambwa kwani ndie binadamu mjinga kabisa anaeishi sasa hivi, sasa kama msekwa nae reasoning yake imefikia hapa ishakuwa noma huko CCM.

kawamba kafanyaje tena mkuu?
Hebu tujuze, si tunasikia ni dokta tena kapewa wizara nyeti ya elimu?
 
pumba kama hizi nilitegemea zingemwagwa na shukuru kawambwa kwani ndie binadamu mjinga kabisa anaeishi sasa hivi, sasa kama msekwa nae reasoning yake imefikia hapa ishakuwa noma huko CCM.

kawamba kafanyaje tena mkuu?
Hebu tujuze, si tunasikia ni dokta tena kapewa wizara nyeti ya elimu?
 
ccm hakuna mwenye ujasiri wa kupambana na ufisadi kikwelikweli, ni usanii mtupu.
Yuko wapi ana kilango, aliekuwa kinara mpaka akapewa tuzo?
Wote kimyaa.
 
Mnamlaumu bure mzee wa watu, hii operation ili-fail tangu mwanzo, ilitakiwa iwe panga moja mbuyu chini. Unawapa watuhumiwa muda wa kujichunguza??? Wapi na wapi, ili siku walipoamua kuwang'oa wangehakikisha wakitoka kikaoni sio wanachama.
 
Anamlea yule boss wa necta

sio yeye tu, ktk mawaziri wote, wana jitahid kufanya kazi hawafiki hata saba, wengi ni mizigo isiyo bebeka.
Hawana nia thabit ya kuondoa changamoto zinazotukabili.
 
Vua Gamba haikuwa Falsafa ya CCM bali ilikuwa ni Falsafa ya Nnauye Jr . Sasa wameona Mwamba wa Kaskazini Laigwanani Mkuu Katingisha Monduli Wameamua Kunywea.

Vua Gamba ni Falsafa na Nape na Ilishindwa kufanikiwa kwa Sababu ilijengwa katika Misingi ya VISASI. Akina Sitta wakamtumia Dogo Nape sasa wanamwangalia tu
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom