Vote for Mount Kilimanjaro to become among new 7 wonders

Status
Not open for further replies.
Shindano litakalopelekea kutangazwa kwa maajabu saba ya dunia linaendelea na miongoni mwa maajabu hayo upo Mlima Kilimanjaro wa Tanzania. Hata hivyo kasi ya watanzania kuupigia kura mlima huo imekuwa ni ya kusua sua. Basi ewe mtanzania, tumia dakika chache za muda wako mtandaoni kupigia kura mlima wetu. Piga kura yako hapa New7Wonders of Nature. Mwisho wa shindano ni Novemba 11 mwaka huu
 
tutapiga ila kuna makundi mawili wengi hawajui kama kuna kitu kama hicho na kunawanaojua kunakuupigia kura lakini wapigeje?ninamaana kuwa ongezeni matangazo,nakutuelimisha itatufaidisha vp watanzania!
 
Nafikiri wahusika wanapaswa kuwa wabunifu zaidi hasa katika matangazo. Lile tangazo linalomuonyesha Mh. Mzee Ruksa akihamasisha lingeboreshwa zaidi. Halina mvuto hata kidogo. hivi watu wa utalii hamna picha/video nzuri zenye kuonyesha mlima? Maeneo mbalimbali ya mlima? Vijito vinavyotiririsha maji na dheluji inayongaa? Tumwone Mzee Ruksa mwanzoni na kisha sauti iwe kwenye background yenye milio ya maji yanavyotiririka na mandhari ya mlima. Kila siku nikiona hilo tangazo najikuta namfikiria Mzee Ruksa...ama kuwaza hivi anafanya nini siku hizi, bado ana nguvu, anasaidiaje chama chake kinavyoendelea kusambaratika...tangazo linaisha sikumbuki lilikuwa linanishawishi nipige kura!

Creativity!
 
Shindano litakalopelekea kutangazwa kwa maajabu saba ya dunia linaendelea na miongoni mwa maajabu hayo upo Mlima Kilimanjaro wa Tanzania. Hata hivyo kasi ya watanzania kuupigia kura mlima huo imekuwa ni ya kusua sua. Basi ewe mtanzania, tumia dakika chache za muda wako mtandaoni kupigia kura mlima wetu. Piga kura yako hapa New7Wonders of Nature. Mwisho wa shindano ni Novemba 11 mwaka huu

Utaratibu wa kura ukoje? Naona umeishia kupiga kampeni tu.
 
Nikiupigia kura utanisaidia nini mimi?miaka nenda rudi mlima upo pale watalii wanapanda lakini sijawahi ona msaada wake zaidi ya kuvimbisha mitumbo ya watu wengine!SIPIGI KURA
 
ili uwe ajabu ni lazima upigiwe kura? watanzania kuweni macho, msije mkawa mmetegwa kuumilikisha mlima wetu kwa wezi wa kimataifa na mkakosa nguvu ya kisheria kuurudisha kwenye miliki yetu tena, msije sema sikuwaonya kabla!
 
jamani tusisusie tupigi kura ili mlima kilimanjaro uingie kwenye maajabu 7 hatakama pesa nyingi inavimbisha matumbo ya mafisadi..dawa ya mafisadi imeshapatikana tunaendelea kuwanywesha...
 
Nafikiri wahusika wanapaswa kuwa wabunifu zaidi hasa katika matangazo. Lile tangazo linalomuonyesha Mh. Mzee Ruksa akihamasisha lingeboreshwa zaidi. Halina mvuto hata kidogo. hivi watu wa utalii hamna picha/video nzuri zenye kuonyesha mlima? Maeneo mbalimbali ya mlima? Vijito vinavyotiririsha maji na dheluji inayongaa? Tumwone Mzee Ruksa mwanzoni na kisha sauti iwe kwenye background yenye milio ya maji yanavyotiririka na mandhari ya mlima. Kila siku nikiona hilo tangazo najikuta namfikiria Mzee Ruksa...ama kuwaza hivi anafanya nini siku hizi, bado ana nguvu, anasaidiaje chama chake kinavyoendelea kusambaratika...tangazo linaisha sikumbuki lilikuwa linanishawishi nipige kura!

Creativity!

mzee mwinyi amewahi kupigwa kelbu kwa kuongea utumbo mbele ya kadamnasi, hafai kutumika kwa promo, kama mlima ni wa ajabu kura haziuongezei ajabu. chukueni hatua ya kizalendo.
 
ili uwe ajabu ni lazima upigiwe kura? watanzania kuweni macho, msije mkawa mmetegwa kuumilikisha mlima wetu kwa wezi wa kimataifa na mkakosa nguvu ya kisheria kuurudisha kwenye miliki yetu tena, msije sema sikuwaonya kabla!

hebu fafanua...
 
mzee mwinyi amewahi kupigwa kelbu kwa kuongea utumbo mbele ya kadamnasi, hafai kutumika kwa promo, kama mlima ni wa ajabu kura haziuongezei ajabu. chukueni hatua ya kizalendo.
duh! Mkuu kuhusu kelbu la Mwinyi umenichekesha sana.
 
chaajabu watu wa nje ya nchi ndiyo wanaoupigia kura sana kuliko watanzania hii ni ishara tosha ama hatujui uzuri wa kitu tulicho nacho au hatuoni faida yake...wanaoutangaza hawaju wapi pakujitangaza mimi nilitegemea wangetumia zaidi mitandao ya kijamii kuliko magazetini..
 
Nikiupigia kura utanisaidia nini mimi?miaka nenda rudi mlima upo pale watalii wanapanda lakini sijawahi ona msaada wake zaidi ya kuvimbisha mitumbo ya watu wengine!SIPIGI KURA
Huo ndiyo tunaita ubinafsi kama ulikuwa hujui tafsiri yake..... hivi kama kitu kina mvimbisha mtu tumbo si umsaidie kiendelee kumvimbisha tumbo? au unataka ufanye kitu kinachokuvimbisha tumbo na wewe?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom