watz mmezidi kuiba hamuaminiki
Ndilo tatizo letu watanzania. Mali ya wizi tunaiita mafanikio!!! Nilikuwa na hamu ya kujadili lakini sijadili tena.
Wewe unafurahisha kweli, unajua sheria ya kuajiri foreigner kama kuna mtanzania mwenye sifa hiyo hutakiwi kufanya hivyo. Unasema watz wezi lini wamekuwariported police na kupelekwa mahakamani. Wizi uko kote hata hao wanaiba mstafute sababu dhaifu kujustify kuvunja sheria za tzAcha kuropoka vitu usivyovijua. NImesoma barua yenyewe hapo juu hawa foreigners hawazidi 15. Wafanyakazi wa Vodacom na NSN ni wangapi? Barua inaishia kutaja foreginers tu bila kutaja ni percent ngapi ya staff wote!
Hakuna mtambo unaotengenezwa hapa Tanzania. Hivyo huwezi kukwepa foreigners ambao ndiyo waliobuni mitambo hiyo.
Labda inawezekana hujui kwamba fundi wa Tanzania kazi yake ni kuiangalia mitambo ikiharibika anaishia kukimbizana huku na kule kuangalia kimeharibika nini na kama ni kikubwa kuzidi ujuzi wake anamtaarifu aliyekitengeneza. Sasa, utakwepaje kuwa na foreigner.
Kama unataka watanzania wawe expatriates waambie ndugu zako huko NSN na Vodacom watengeneze mitambo yao uone kama kuna mgeni atanusa pua yake hapa nchini.
Hivyo, tatizo ni hao vijana wako wa Tanzania. Tatizo ni elimu yako Tanzania haitoi ubunifu hata wa kutengeneza toothpick.
Utalaumu nini katika hali hii.
teh teh teh....hata wewe na mimi tukisema no, haina maana wataondolewa Tanzania. By the way, hilo ni duka lake kweli. Ana hiari ya kufanya anachotaka. Namna pekee ya kumbana ni kuwa na sheria zinazofuatiliwa na zinapewa meno ya kufanya kazi.
Watanzania tuliopata nafasi ya kupita Vodacom tuueleze umma ukweli. Hivi tulitaka tusaidiwe na serikali kwa vitu gani ambavyo hata sisi tungeviweza.
Nimeingia Vodacom mwaka 2005 nikaondoka mwaka 2010. Watanzania msishangae kusikia kwamba Vodacom ni kampuni kubwa ina wafanyakazi wengi lakini hakuna chama cha wafanyakazi yaani COTWU au chochote.
Nasikia kabla ya mimi kuajiriwa kilikuwepo halafu staff wote wakajitoa kukabaki hakuna mwanachama. Hivyo kwa miaka nenda rudi eti hakuna chama cha wafanyakazi. Mimi nilivyosikia hivi sikuwa hata na hamu ya kufikiri kuwepo na chama maana ukikitaja tu unaonekana kama kituko, si na menejiment bali kituko kwa staff wenzako.
Sasa hata kuwa na tawi la chama cha wafanyakazi mlitaka serikali itusaidie kuwa nalo? Ndiyo maana hiyo barua huoni popote kama imepelekwa kopi kwenye chama chochote cha wafanyakazi.
Tumeula wa chuya, tuelezane ukweli tusifiche udhaifu wetu uliotufikisha hapa. It's too late.
Dawa yake ni wao wenyewe kuunda umoja humohumo kupambana na wazungu wawekezaji. Na hilo liliwezekana kwa kuwaondoa SIEMENS na wakashika nafasi hizo.
Tatizo ni kwamba wazawa wanapopewa nafasi basi wale wanaokamata nafasi za juu wanaakandamiza wazawa wenzao kuliko hata wazungu.
Unajua wazungu wanaogopa kukandamiza kwa sababu wanajua hawako nchini mwao. Ukiwatishia sheria kidogo tu wanagwaya.
Hivyo wazungu wanawatumia wazawa waliowapandisha tu-vyeo tudogo tu. Mzawa akipandishwa cheo na ndani ya miaka miwili akaweza kujenga nyumba Mbezi Beach basi humwelezi kitu, yeye ndiye anakuwa wa kwanza kumkandamiza mzawa mwenzake.
Wote waliopita Vodacom au kampuni hizi za wazungu wanalijua hili fika na ndiyo wengi kwenye post hii wanaoujua ukweli kwamba post hii ikiachwa kama ilivyo basi itaonekana kama vile ina lengo zuri kuwatetea watanzania lakini kumbe imeficha kitu ambacho kama hukupitia kwenye makampuni haya utakuwa umepigwa changa la macho.
Mimi nionavyo ni kwamba watanzania tujifunze kwamba bila umoja unaodumu hakuna tutakachokiweza. Mkiwa na umoja kazini wa kupambania haki zenu bila kugeukana hakuna mwajiri au mwekezaji atakayewaweza wala kuwaonea.
Lakini mwenzenu akipewa ka-cheo halafu akaweza kununua gari na nyumba ya kifahari, basi huyo ndiye anakuwa wa kwanza kuwakomesha na neno haki ya wafanyakazi linnakuwa msamiati mzito kwake.
Wazungu wa Vodacom walilijua hili, wakaunda vyeo vingi sana ndani ya Vodacom. Waliunda vyeo vinaotwa HOD yaani Head of Division na kilipoonekana kinachuja wakaunda cheo kingine kiitwacho EHOD yaani Executive Head of Division.
Kulikuwa na msururu wa vyeo kiasi kwamba parking kwa ajili ya wenye vyeo hivyo ilikuwa haitoshi! Vyote vile vya nini? Ili wawafanye kazi ya kuwakandamiza wazawa wenzao. Na wamefanikiwa sana kwa kazi hii.
Hivyo, kinachotokea Vodacom na NSN ni fundisho tamu kwa watanzania, tena acha kitokee hivyohivyo bila chenga. Mshahara wa dhambi ni mauti na malipo mengine ni hapahapa duniani.
kwani agreement inasemaje?kuna baadhi ya senior positions zinatakiwa kupewa wazawa na zingine wapewe foreigners just like other institutions,ila naona almost senior position zote wamechukua hao makaburu na wahindi!!kweli hapo kuna tatizo may be hawatuamini watanzania,like what happened NBC LTD!