Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom,

Mwenzenu nimeenda kimasomo nje kidogo ya nchi, sijaitumia voda yangu toka tarehe 25/05/2014.

Nategemea kumaliza masomo mwisho wa mwezi wa kwanza 2015.

Je nitaikuta line yangu hai??
 
Jamani nisaidieni, M-PESA wezi, wananiibia kila mara. Tarehe 30 Nov.2014, wamenila, tarehe 3 Dec.12, wamenila tena. Nilipowapigia,kwamba sijapokea tokens wala fedha haijarudi. Wakaniambia fedha hurudishwa ndani ya siku saba. Leo siku ya 12 hakuna tokens hakuna hela.

M-pesa wezi....wezi hao...Kamata wezi hao! wezi....wezi....wezi hao! Mpesa wezi! Kamata hao!
 
Vodacom,

Mwenzenu nimeenda kimasomo nje kidogo ya nchi, sijaitumia voda yangu toka tarehe 25/05/2014.

Nategemea kumaliza masomo mwisho wa mwezi wa kwanza 2015.

Je nitaikuta line yangu hai??

Kwa experience yangu huikuti
 
Maeneo ya kwafundi baiskeli km 16 kutokajamanika ferry kigamboni network ya vodacom inasumbua sana. Tatizo ni la mda mrefu tusaidieni
 
Voda nyie sahv usanii umewazidi hamna kitu yaan network inazingua cm hazitoki ukituma txt km umeipeleka kwa miguu inachelewa kufika,ukiweka vocha hata kama una bundle unakuta mshaikata so kama mmeshindwa its better mkazima vimitambo vyenu mkafanya shughuli zingine jaman mnatukera
 
Ni muda sasa mtandao au kampuni ya vodacom imekuwa ikilalamikiwa na wateja wake kutokana na matatizo mbalimbali yaliyopo katika kampuni hiyo hasa pale ambapo salio la mtu lilipokuwa likikatwa na unapopiga simu huduma kwa wateja,muhudumu anakwambia kuwa salio lako limetumika kwa kuwa hukuzima data katika simu yako.
Hapo ndipo mwanzo wa wizi na hujuma za vodacom zilipoanza kwani iliwezekanaje simu iwe na kifurushi cha kutosha,MB za kutosha DAKIKA za kutosha na SMS za kutosha halafu mwisho wa siku uambiwe DATA ktk simu yako ndiyo iliyomaliza salio lako ?
Kwani matumizi ya data kuw on na matumizi ya vifurushi vya voda yanatofauti ?
Imefikia hatua sasa vodacom mshakuwa kero tena kubwa tu,unaweza kupiga simu huduma kwa wateja na muhudumu bila aibu anakwambia umpigie baada ya nusu saa au dakika kadhaa,hapo unaweza kujiuliza kuwa hiyo namba 100 ni line ya mtu binafsi au la ?.
Baada ya malalamiko yote hayo,sasa voda wamekuja na mtindo mpya kabisa ambao kibiashara na wizi na hujuma kwa wateja wao.
Nipo wilaya ya Arumeru,kata ya Akeri na tarafa ya Poli hapa mkoani Arusha.,eneo hili ni zaidi ya wiki sasa unapozungumza na mtu kupitia mtandao wa simu unakuwa hamsikilizani kabisa na mara nyingi tatizo hili linakuwa kubwa hasa nyakati za usiku.
Hapo tunajiuliza,tatizo hili hamlitambui na kama hamlitambui ni kwanini na kama mnalitambua ni kwanini hamjalitatua na kama lipo nje ya uwezo wenu ni kwanini mnaendelea kukata salio wakati mnatambua vizuri kuwa hakuna mawasiliano katika mtandao wenu ?
Ningependa kuwauliza vodacom,hivi mnachofanya mnaelewa kuwa ni wizi na hujuma kwa watanzania na muda si mrefu watanzania watawachoka na kuwafurumushia makwenu ?
Yapo makampuni mengi ya simu yanayotaka kuja kuwekeza Tanzania na pia Tanzania kuna makampuni ya kutoa huduma kwa wananchi.
Bado muda mfupi,wateja wenu tutapeleka malalamiko yetu serikalini na hapo ndipo itakapojulikana mbivu na mbichi.
TUMEWACHO.
 
Mm ni mtumiaji sana wa vodacom
Nmewapigia sana simu huduma kwa mteja
Nimetuma sana meseji kupitia ukurasa wenu wa facebook
Lakini kila siku mnasema porojo tuuuuu
 
Awa jamaa ni vilaza sana hakuna lolote wengi wao wanawaza kuiba tu wajinga sana. Muda mwingine mtu umenunu bandle ya cku nzima cha kushangaza masaa nane hadi tisa network upande wa internet inapotea masaa yote hayo hakuna internet wanakuja kurudisha usikuuu na masaa ya bandle lako kuisha muda wake yanabaki pale pale laiti kama vile tatizo halikua upande wao..mimi nasema hivi haya ni matatizo wanayoyatengeneza wenyewe ili kuiba pesa kwa kuwapunguzia muda wa matumizi wateja wao then wao wanachukua ile pesa ya muda ule ambao haukuweza kufanya matumizi ya simu yako ila kule wanaweka kama ulitumia
 
Mnakera pale unaposema kwa 6000 unapata siku saba unlimited speed kumbe ki ukweli ni siku saba of usage with unlimited speed up to 2gb download. Inabidi nifuatilie tcra kujua hapa mtumiaji inakuwaje
 
Back
Top Bottom