Vodacom na wizi wa mchana

ngonani

JF-Expert Member
Aug 27, 2012
1,366
596
Nilivutiwa na tangazo la Vodacom kuwa ongeza salio la 7500 kabla ya 31st August nao watakuongezea mara mbili, nikapiga hesabu yangu nikaona nikiweka hiyo na kupata ofa angalau itanisukuma kwa siku kadhaa nikiwa na salio la elfu 22,500.

Sasa cha ajabu nimeweka hela najibiwa nitaongezewa elfu 15 na nizitumie kwa siku mbili kupiga voda kwenda voda, huu si ndio wizi wa mchana, ilitakiwa kwenye ilo tangazo lao la ofa waseme kuwa hiyo nyongeza itatumika kwa siku mbil i tu na baada ya hapo haina kazi, pia wajulishe watu kuwa nyongeza hiyo ni voda kwenda voda tu, ningejua hivyo nisingepoteza hela yangu, ningeendelea na utaratibu wangu wa kununua dakika 100 kwa shilingi elfu mbili tu ambazo nazo ningetumia siku mbili hizo hizo.

Acheni wizi kwenye matangazo yenu.
 
Minya *602#
utachat bure siku nzima kwani lazima upige?
V. Kazi ni kwako.
Tigo ndiyo wezi.
 
Watanzania mnapenda vya bure!Mpaka leo mnaibiwa kwa karata 3,weka elfu upate elfu 2!
 
Hakuna Bure dunia hii Arifu.. wenyewe wameshapiga mahesabu na wanajua fika hutoweza maliza hizo pesa.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom