Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vodacom na vocha ya tshs. 450/= mtaani wauzaji vocha wanatunyanyasa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkiliman, Aug 8, 2012.

  1. Mkiliman

    Mkiliman JF-Expert Member

    #1
    Aug 8, 2012
    Joined: Jun 8, 2011
    Messages: 942
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 35
    Habari wanajamvi?

    Naomba kufahamu juu ya Vocha Mpya ya Vodacom yenye thamani ya Tshs. 450/=.
    Nimepata mkasa wa kubishana na kufikia hatua kuonekana mkorofi dhidi ya wauzaji wadogo wa Vocha, kisa ni kwamba hizo Vocha za Tshs. 450/= zimeandikwa bei hiyo lakini wao wanauza kwa Tshs. 500/=.

    Nilipata shida kuamini kwenye duka la kwanza lakini takribani 3 days nimeona huo mchezo unaendelea huku kwetu TABATA, nilikwenda dukani na kuambiwa kuwa hiyo ndiyo bei mpya ya Vocha ya Voda na wanakonunua (whole sale shops za voda au wafanyabiashara wakubwa wa Vocha) wanawaambia kuwa let your customers pay Tshs. 500/= and give them voucher ya Tshs. 450/=.

    Wadau hamjakutana na hii kadhia au nini maana ya hii bei, Tshs. 50/= kwa kila mteja kuacha dukani....ni pesa nyingi sana....na i find it to be illegal appropriation of money!!

    Tusaidiane kufahamu wizi huu wa either VODACOM au WAFANYABIASHARA.


    Thanks for having this platform to air my views.
     
  2. SYENDEKE

    SYENDEKE Senior Member

    #2
    Aug 8, 2012
    Joined: Jul 18, 2011
    Messages: 163
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Ndugu yangu bora umeleta hii threat huu ni wizi kwenye mitandao ya simu lazima tuwapeleke tcra huwezi kuniandikia price tag 450 halafu unaniambia nilipe 500 na ile hamsini inakwenda wapi kama sio ni njia ya kukwepa kodi jana nimegoma kununua hiyo vocha nimeamua kununua vocha ya 1000 sasa hawa watu wa voda wajitokezi halaka iwezekanavyo hawawezi kutufanya sisi watoto
     
  3. B

    Bangoo JF-Expert Member

    #3
    Aug 8, 2012
    Joined: Nov 3, 2011
    Messages: 5,597
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Ni kweli hata sisi wauzaji twapata tabu sana
     
  4. HASSAN SHEN

    HASSAN SHEN JF-Expert Member

    #4
    Aug 8, 2012
    Joined: Mar 26, 2009
    Messages: 428
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Voda ni wezi p****af zao mi mwenyewe leo asubuhi nimegombana na muuza duka,kwanza wametengeneza zile vocha za nini? Jiti tatu wamepeleka wapi? Zile 500 za kwenye karatasi kwa nn hawazitaki. Mwisho hii nchi ni jahazi lisilokua na nahodha linakwenda tu kufuata uelekeo wa upepo.
     
  5. mchemsho

    mchemsho JF-Expert Member

    #5
    Aug 8, 2012
    Joined: Jun 8, 2011
    Messages: 3,058
    Likes Received: 61
    Trophy Points: 145
    TCRA zZZiiii, usingzi wa pono, hata haijulikani wanaregulate nini, bora wenzao polisi tunajua wanaregulate Chadema
     
  6. charminglady

    charminglady JF-Expert Member

    #6
    Aug 8, 2012
    Joined: Apr 16, 2012
    Messages: 17,497
    Likes Received: 547
    Trophy Points: 280
    Naandika kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo. Nunua muda wa maongezi via m-pesa na utapata nyongeza 25%. Me nshasahau vocha za voda kitambo sana. Uzuri m-pesa hata buku unapata. . . . Achana na hyo mikaratasi. Nahisi pia wana-discourage vocha makaratasi. .
     
  7. S

    Sometimes JF-Expert Member

    #7
    Aug 8, 2012
    Joined: Dec 28, 2010
    Messages: 4,574
    Likes Received: 353
    Trophy Points: 180
    Kwangu mimi ni tofauti kabisa. Kila nikinunua muda wa maongezi kwa m-pesa hiyo 25% ninaiona kwenye maandishi lakini salio halisi linakuwa ni lile nililoingiza!
     
  8. P

    Prince Hope JF-Expert Member

    #8
    Aug 8, 2012
    Joined: Jul 21, 2012
    Messages: 2,170
    Likes Received: 39
    Trophy Points: 145
    Waiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiizi! Nyambafu!
     
  9. asigwa

    asigwa JF-Expert Member

    #9
    Aug 8, 2012
    Joined: Sep 21, 2011
    Messages: 11,546
    Likes Received: 6,066
    Trophy Points: 280
    TCRA wako bize wanafaudu upepo wa ghorofa jipya........

    wakija utawasikia bado wanafanya tathmini ya kina kujua athari ya vocha mpya kwa wafanya biashara wadogo....
     
  10. Aggrey86

    Aggrey86 JF-Expert Member

    #10
    Aug 8, 2012
    Joined: Jun 26, 2011
    Messages: 856
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35
    Mkuu hilo tatizo limenikuta mimi jana jioni mitaa ya tabata mawenzi pia huku,niliingia maduka kama matatu hivi wananiambia vocha ya voda ya mia tano haipo eti vocha ni mia 450, Lakini wanauza mia tano nikabishana nao sana kiukweli huu ni wizi jamani sasa kila siku ukiacha hizo hamsini hamsini ni sh.ngapi?
     
  11. R

    Rebel volcano JF-Expert Member

    #11
    Aug 8, 2012
    Joined: Jun 1, 2012
    Messages: 404
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    hizo chenchi za 50/= 50/= 50/= ndio issue na hakuna benki wanazozitoa hata ukienda na laki moja upewe 50/= utakuta bila bila.
    sasa akuuzie 450/= na chenchi ya kukurudishia hana si bora akupigize mia tano tu!!!
     
  12. Iyokopokomayoko

    Iyokopokomayoko JF-Expert Member

    #12
    Aug 8, 2012
    Joined: Sep 15, 2011
    Messages: 1,816
    Likes Received: 19
    Trophy Points: 0
    Hata airtel wezi sana upande wa bundle, leo asubuhi kila nikitaka kujiunga na kifurushi cha siku yaani 500 imegoma zaidi ya mara 10, niki-surf bila kuunga bundle inakubali, wamefanya hivyo mpaka walivyomaliza 2000 yangu!, unajuwa kuna wakati mi nashindwa kuelewa ni namna gani watu wakawa wanaibia tu wananchi na hakuna wa kukemea!!!!!!!!!!
     
  13. R

    Rebel volcano JF-Expert Member

    #13
    Aug 8, 2012
    Joined: Jun 1, 2012
    Messages: 404
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    muhimu hapo si kulaumiwa wafanyabiashara waliopokea vocha hizo toka kwenye shirika,swala la msingi kwa nini voda watoe vocha ya 450/= badala ya 500/=,na tigo nao wakitoa ya 470/= au zain watoe ya 380/= nani hapo alaumike mfanyabiashara au mwenye kampuni ya simu kwa kutoa vocha ambazo inaeleweka itakuwa kero kwa wauzaji na wanunuaji!!!
     
  14. Iyokopokomayoko

    Iyokopokomayoko JF-Expert Member

    #14
    Aug 8, 2012
    Joined: Sep 15, 2011
    Messages: 1,816
    Likes Received: 19
    Trophy Points: 0
    Mi kuna vocha ya voda pia nimenunua tangu asubuhi ya 500 sijaikwanguwa ipo mezani hapa, baada ya kusoma thread hii naangalia kweli imeandikwa 450! wizi huu, sasa sipati picha huko kijijini itakuwa inauzwa 700!
     
  15. Pota

    Pota JF-Expert Member

    #15
    Aug 9, 2012
    Joined: Apr 8, 2011
    Messages: 1,762
    Likes Received: 55
    Trophy Points: 145
    kama mawazo ya grrit thinka ndo haya...kazi kweyikweyi...issue sh 50, bali ni haki na uhalali wa kilichoandkwa na unacholipa...neva b ize going that much...
     
  16. N

    Nguto JF-Expert Member

    #16
    Aug 9, 2012
    Joined: Apr 11, 2011
    Messages: 1,938
    Likes Received: 144
    Trophy Points: 160
    HII HABARI NIMEISIKIA SIKUAMINI KUWA UKINUNUA VOCHA YA SHS 500 UNAPEWA 450. kAMA NI MIMI SINUNUI HIYO VOCHA KWANI HUU NI WIZI WA MCHANA KWEUPE!!!
     
  17. mtotowamjini

    mtotowamjini JF-Expert Member

    #17
    Aug 9, 2012
    Joined: Apr 23, 2012
    Messages: 4,540
    Likes Received: 3
    Trophy Points: 0
    Na mimi nilitaka kusema hivi hivi kua hizo vocha za 450 zinaumiza wauza duka maana shs 50 atazitoa wapi? Voda wanaleta shida tu kwa wauza vocha ni bora wafanye 400/- angalau change ya 100 ni rahisi kuipata
     
  18. Msalagambwe

    Msalagambwe JF-Expert Member

    #18
    Aug 9, 2012
    Joined: Jul 11, 2012
    Messages: 599
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    Ni Tanzania tu ambako.
    Salio la $100 (150,000) halitoshi,
    kulipia simu ya mkononi,
    kuongea mwezi mzima.

    Kampuni za Simu Tanzania,
    Zinatoza Roaming Rate kwa kila mtu,
    Kana kwamba Watanzania wamejisajiri katika kampuni,
    za simu nje ya nchi ili watumie zimu zao nchini Tanzania,
    kwa gharama kubwa iitwayo Roaming.

    Rate za simu za Tanzania,
    Hata Ibilisi kuzimu hatozi hivyo,
    Rate za internet Tanzania hata,
    ibilisi anatuhurumia tunavyominywa,
    Cha ajabu wenyewe tumeridhika,
    wala hatushituki.

    Wamenyonya damu karibu iishe,
    wamenyonya misuli na bone marrow,
    sasa wameanza kuchomoa mifupa yenyewe,
    sisi tunachekelea tena tunaona sawa tu?

    Ukiweka hata Nusu Millioni Tshs 500,000.00 ($334.00)
    kama salio katika simu yako,
    bado huwezo ongea na simu yako ,
    mwezi mzima.
    Hivi hatutambui kwamba tunaibiwa,
    au tunajua sasa tufanye nini!?

    Kukubali bei za kifisadi,
    ni dalili moja ya kuwa na.
    mawazo ya kifisadi,
    Wananchi tunaamini kuna,
    siku nasi tutaukata kwa,
    kuendelea kuibiwa na kila mtu.

    Hapa USA kampuni aghari sana unalipa $145.00,
    kwa mwezi kwa
    Simu
    SMS
    Internet

    Kima cha chini katika kampuni za simu ni $12.00 kwa saa,($1920 kwa mwezi)
    huyo ni karana asiye na cheti chochote na bado inalipa ile mbaya kwa kampuni.

    Kuna Uhuni na uharamia mwingine,
    Cellphone za Tanzania hazina Mail box ya kuacha message,
    Wanasave mabillioni kwa mwaka kwani,
    hawalazimiki kulipia saver.

    Kuna yeyote alionae hili au ni mimi tu? Je ni halali hiyo?
    Tunasubiri Zitto au Mnyika waanzishe hili soo bungeni?
    Sisi kama wateja tunafikiria nini?

    Haya sasa vocha ya Tshs 450.00 tunauziwa 500?
    KWa ulofa bado tunakubali!!!
    Sisi tungekuwa juisi ingekuwa juisi ya BAMIA.

    Sisi wa Tz ni
    Kichwa cha mwendawazimu,
    Shamba la bibi,
    Choo cha City,
    mama huruma,
    shimo la maji taka,
    Tuna uvumilivu wa sbuni.
     
  19. o

    oyaoya JF-Expert Member

    #19
    Aug 9, 2012
    Joined: Mar 4, 2012
    Messages: 276
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Ni njaa ya wauzaji wenyewe kutaka Super Normal Profit, bei ya jumla ya hizo vocha ni kati ya 380 na 400 kwa vocha.
    Bei stahili ya rejareja ni 450 otherwise muuzaji ndo anaekuibia. Ila kwa kuwa Tshs 50 ni hadimu kidogo bora hawa VODA waondoe huu mkanganyiko, wazirudishe jero jero!
    Kuna mbabe mmoja kamkung'uta muuzaji makonde eneo la Feri asubuhi hii kwa kutorudishiwa Tshs 50 yake
     
  20. Msalagambwe

    Msalagambwe JF-Expert Member

    #20
    Aug 10, 2012
    Joined: Jul 11, 2012
    Messages: 599
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    Nchi zenye Wenyenchi,
    Hii habari ingekuwa gumzo,
    la kuwabana Kampuni ya simu,
    Kwetu waandishi wa habari,
    wanasubiri habari zinazowafurahisha,
    Waheshimiwa.

    Watu wakipigana kwa sababu ya,
    Utata wa product fulani,
    maana yake Marketing Director,
    wa kampuni husika,
    Yuko matatani.

    Hapa kwetu ni kichekesho,
    na chanzo cha kuona kila mtu,
    mjinga.
    Tutaamka lini?


     
Loading...