Vodacom huu sasa ni utapeli...

NOT FOUND

Senior Member
Mar 14, 2011
158
59
Hizi messages zao zinanikera sana:

wastahili sifa! Tulijaribu kuwasiliana na wewe na hukujibu! Muda ni sasa: Tuma jina lako kwenda 15544 na waweza shinda leo tsh 3m taslimu na vodacom! 550tsh/sms
___

una neema! Usichukulie ujumbe huu ki mzaha: Tuma jina lako haraka kwenda 15544 na waweza shinda tsh 3,000,000 taslimu ya vodacom usiku huu! 550tsh/sms

___

075624**** imechaguliwa, ni namba yako? Basi, waweza shinda tsh 3,000,000 taslimu leo na vodacom! Tuma jina lako kwenda 15544 sasa! Hatukutanii! 550tsh/sms
___

umebahatika! Katika mchujo, namba 075624**** yaweza kushinda usiku huu tsh 3,000,000 taslimu na vodacom! Tuma jina lako kwenda 15544 haraka! 550tsh/sms
___
hongera! 075624**** imeshinda namba ya siri: Sc01! Tuma tu jina lako kwenda 15544 haraka na mara 1 uingie droo ya tsh 3,000,000 usiku huu na vodacom! 550tsh/sms

na nyingine nyiiiingi ambazo ni wizi mtupu
 
Tunakoelekea sasa ni kuwapeleka mahakamani na kudai mamilioni kwa kutusumbua kwa biashara zao. Nchi zingine ili uingizwe kwenye meseji kama hizo ni lazima ujaze fomu na kusaini. They can't take us for granted. Ninaposoma meseji hizo kwanza napoteza muda wangu, pili simu yangu inatumika kusoma meseji zao, tatu chaji inatumika na wakati mwingine unaposubiri ujumbe wa maana inaweza kukutoa roho bure. Those capitalists should be serious otherwise wataishia mahakamani.
 
Wameiga kushusha bei faida inakua ndogo wanaamua kutumia njia ya kitapeli au RA kawadanganya njia ya wiz?
 
Definitely..Vodacom wanapoteza credibility kabisa..even me nimepata hayo ma sms yao ni kero..
 
zipo nyingi na hata yale magari zuga tu. Sijaona hata moja dar, mwanza, moshi au arusha. Wamekusanya bilioni mia na sasa wanataka bilioni 210 watunishe mtaji. Nasikia washindi wote ni wafanyakazi wao au mawakala....RA/ER mtatueleza pesa/zatu
 
Kuna haja ya kupeleka malalamiko TCRA maana zinaleta usumbufu na kwa namna fulani zinalaghai wateja hasa ambao hawataelewa maana iliyojificha ya ujumbe huo.
 
upuuzi na ujinga mtupu,yani serious huwaga naboreka saaaana.
:A S 465:
 
jamani kama kuna jambo linaronikera ni hzi msg kwani wana haki gani kulazimishakutuma zinapoteza mda
 
Tunakoelekea sasa ni kuwapeleka mahakamani na kudai mamilioni kwa kutusumbua kwa biashara zao. Nchi zingine ili uingizwe kwenye meseji kama hizo ni lazima ujaze fomu na kusaini. They can't take us for granted. Ninaposoma meseji hizo kwanza napoteza muda wangu, pili simu yangu inatumika kusoma meseji zao, tatu chaji inatumika na wakati mwingine unaposubiri ujumbe wa maana inaweza kukutoa roho bure. Those capitalists should be serious otherwise wataishia mahakamani.

There is Push and Pull Messages, na zote hizi ni lazima ujisajili na uridhie kupokea takataka zote, Wao wanachukuliaga poa wananchi,
I think the best option ni kutumia Radios an TV, na sio kutuvuruga kwenye sim zetu,

Fulukupisi!
 
Huu ni wizi wa mchana wanalaghai wananchi. Inakuwaje wanamtumia kila mteja sms hizo kwamba namba yake imechaguliwa, mara walijaribu kuwasiliana naye hakupatikana. Kitu kibaya zaidi wanatuma sms zenye kutia matumaini huku wakijua hali ya maisha ya watanzania wengi ni ngumu hivyo watashawishika kujibu sms hizo wakiwa na matumaini ya kupata hizo mil 3 ili wajikwamue kimaisha kumbe ni danganya toto.

Mimi nimetumiwa sms hzo mara nyingi na huwa nazipotezea na jana wamemtumia mzazi wangu nikamwambia hao ni matapeli tu hawana lolote. Mimi naziita pesa zinazokusanywa na vodacom kupitia shindano hili kuwa ni pesa haramu kwa sababu zinapatikana kwa njia ya udanganyifu na ulaghai. Shame upon you VODACOM acheni utapeli vinginevyo tutachukua hatua.
 
zipo nyingi na hata yale magari zuga tu. Sijaona hata moja dar, mwanza, moshi au arusha. Wamekusanya bilioni mia na sasa wanataka bilioni 210 watunishe mtaji. Nasikia washindi wote ni wafanyakazi wao au mawakala....RA/ER mtatueleza pesa/zatu
whaaaat?
 
Mbaya zaidi nasikia kila msg ukijibu tuu wanakukata kama 550 ivi,ivi hamna namna ya kublock izo msg zisiendelee kutufikia
Wana bahati ni line ya ofisi otherwise ningeshahama kitambo
 
mimi nilijaribu kujibu hizo sms ili nione mwisho wake. Nilituma sms kibao, na kuliwa mshiko wa nguvu. sikufika mwisho. na bado zinakuja tu.

My verdict: STYLISH DAY LIGHT ROBBERY! ... Karata 3 ! BEWARE
 
nadhani hawakutafakari vema kabla hawajitigolize. but hiki ni
kivuli cha namna tutakavyo buruzwa na wakenya na waganda
tutakapoanza rasmi soko la pamoja la EAC na vikorombwezo
vyake
 
Nisingekuwa najua marketing ningekuwa naingia mkenge sana kwa hizi msg
Mkuu huhitaji kujua marketing kujua kwamba huu ni wizi....eti tuma jina lako tu utaingizwa kwenye droo...kwani wamelitafuta kwenye database yao halipo!?
 
mimi nilijaribu kujibu hizo sms ili nione mwisho wake. Nilituma sms kibao, na kuliwa mshiko wa nguvu. sikufika mwisho. na bado zinakuja tu.

My verdict: STYLISH DAY LIGHT ROBBERY! ... Karata 3 ! BEWARE
Pole sana tena ukiwajibu ndiyo utakuwa unatumiwa mpaka ukome.....
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom