Vodacom Customer Care kariakoo Hovyo sana

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
Kama kuna sehemu mbaya sana kwa huduma basi ni kariakoo mtaa wa Kongo, vodacom wamebana sehemu kubwa ya huduma na kuifanya iwe m-pesa na kuacha sehemu ndogo ya kupokea wageni.

Yaani imekuwa kero sana watu wanajazana kupita kiasi, kibaya zaidi kuna msichana anayerudisha laini zilizopotea, huyu anahasira kweli watu wakimuuliza awaelekeze huwajibu vibaya karibia kuwatusi, yaani inahitaji imani sana kuhudumiwa, ukimuliza zaidi anakuambia nenda Ohio wakati huduma hii ya kuswap laini haitumii hata dakika tatu.

Kama basi hawawezi kuhudumia watu waandike kuwa huduma hii ya kuswap haipo kwani wanakera sana wanapowajibu wateja vibaya. Kisichana chenyewe kijibu hovyo kipo pale mlangoni kushoto.
 
Back
Top Bottom