Viwanja vya NMC Arusha: Dr. Slaa akamatwa, Polisi yajaribu kuwaondoa kwa nguvu CHADEMA

Tuna viongozi mazuzu, wanadhani wao sio binadamu. Wao ni biaadamu wa kawaida kama Gadafi. Na cheo ni dhamana. Wachunge sana sana.
 
Watu hawajaangalia tu kama risasi zingekuwa zinanyamazisha watu Gaddafi angeendelea kuwepo na waandamani ya Yemen na Syria wangeacha.. wanalazimisha wananchi kuvuka mstari wa aidha kuchagua maisha au kifo.. hekima ndicho kitu pekee ambacho bado tunakihitaji zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Polisi na hao Viongozi Waandamizi hilo hawalitambui:
Binadamu mwenye akili timamu uwezi kumbadilisha kutenda unachotaka wewe bila ridhaa yake na hasa akisha gundua kuwa kuna zengwe linafanyika
 
Hawa CCM wamechokwa na watu na huku Arusha ndiyo hawakubariki kabisa wanajaribu kulazimisha tu,hao polisi wanaowatumia na mafisadi kuzuia nguvu ya uma hawatafanikiwa.

VIVA CHDEMA, FREEDOM IS COMING
 
Nadhani madai ya regime change yanaanza kupata mashiko.

Kadri unyama unavyozidi ndivyo kadri wanamapinduzi wanapokosa sababu za kurudisha majeshi nyuma...Wananchi wanapouwawa,inaongeza ari ya wenzao kupambana zaidi ili kuhakiisha kuwa damu yao haikumwagika bure.

Kama kuna wananchi wanauwawa kwa unyama wa polisi,basi kuacha damu hiyo ipite bure ni kuwa macoward.

Nadhani unyanyasaji wa kutumia dola ndiyo motivation kwa wanamapinduzi.

Historia imedhihirisha hilo.

Acha kujidanganya wewe hakuna chochote...eti historia imedhihirisha.
 
Nimeona landrover PT 1178 Pickup na nyingine yenye namba ya kibinafsi ingali ni ya police ikiwa imepakia pikipiki aina ya Toyo na kuelekea central police. Na kila kitu kimechomwa moto na hata baadhi ya matendi yote yamepakiwa na naona hili litakuwa shazi lingine mpya kwa upande wa siasa.

inamaana police wamewatawanya watu uwanjani?
 
Jamani, hivi kweli hakuna njia mbadala ya kulishughulikia hili jambo?. Kama Lema yuko ndani kwanini tusiache sheria ifuate mkondo wake?, huo mkutano hapo NMC utasaidia vipi katika kutatua tatizo hili?. Kweli imeshindikana kukaa mezani na kulizungumza suala hili kistaarabu?.

Inawezekana kabisa kuna mambo hayaendi ipasavyo lakini pia jinsi ya kudai haki isitumike fujo, busara na hekima itumike badala yake.

mkuu sheria haiwez kuamua hili lema aliamua kukaandan baada ya kuona kila kukicha anaonewa?
Zamana ilikuwa wazi wameenda kumtoa kwa kukata remove ordel hakim kagoma kusain anadai akae ndan mpaka tarehe 14.
Je sheria ndiyo inasema hivyo ?
Wa2 wamechoshwa na uonevu wa polisi wanao 2miwa na ccm.
Wananch hawajaleta fujo bali wamekesha kwa kutaka haki itendeke juu ya mbunge wao polisi ndiyo wamewavamia na kupiga mabom na risas za moto.
 
Habari nilizopata mida hii kutoka kwa swahiba wangu aliye katika uongozi wa juu ni kwamba serikali imewekwa katika mtihani mkubwa kuhusiana na mgeni Prince Charles, kutokana na yanatokea Arusha. Kuna baadhi ya wakuu wanaona yule hakimu hakutumia busara kwani angemtoa jana Lema, CDM wakafanya mkutano wao jana na leo, na kesho tarehe 9 Arusha ingekuwa shwari kwa ajili ya ziara ya Prince Charles eneo hilo.

Wanaona sasa hali hii inaweza ikaharibu kabisa ratiba.

Nakubaliana nawe, hakimu hakutumia busara katika hili kwa kuona mazingira yaliytokuwapo. Mahakama zetu hizi! Daima hudai kuwa ziwe huru, na huku zinakubali kutumiwa tu. Katika kongamanao la Majaji wastaafu Ijumaa iliyopita jaji mstaafu Thomas Mihayo alisema hata ile kesi ya Mtikila ya kutaka wagombea binafsi, Mahakama ya Rufaa ilipata msukumo kutoka nje kutoa hukumu ile waliyotoa.

Na katika miaka ya hivi karibuni Mahakama Kuu ilipata msukumo kutoka serikali ili ikae usiku wa manane kusikiliza shauri la mgomo wa walimu uliokuwa uanze siku ya pili yake na ikatoa uamuzi wa kusema mgomo haukuwa halali.

Mahakama zetu zinakuwa shit kweli kweli.
 
Habari nilizopata mida hii kutoka kwa swahiba wangu aliye katika uongozi wa juu ni kwamba serikali imewekwa katika mtihani mkubwa kuhusiana na mgeni Prince Charles, kutokana na yanatokea Arusha. Kuna baadhi ya wakuu wanaona yule hakimu hakutumia busara kwani angemtoa jana Lema, CDM wakafanya mkutano wao jana na leo, na kesho tarehe 9 Arusha ingekuwa shwari kwa ajili ya ziara ya Prince Charles eneo hilo.

Wanaona sasa hali hii inaweza ikaharibu kabisa ratiba.

Ndio maana ni wazi kuwa Misiningi ya UPENDO, HESHIMA Na MATUMAINI mtaani havitapatikana. Jibu ni moja Waraka wa Lema 2011 (UTU NA UBINADAMU) na Waraka wa Azimio La Arusha 1967 (UTU NA UBINADAMU) ... Vingekuwa akilili kwa huyo Hakimu .. Angejua UTU kama Busara, UTU kama Heshima , UTU kama Upendo, UTU kama MATUMAINI na hii Ingeplekea HESHIMA UTU NA UZALENDO WA TAIFA!!

Na kwa UTU Na UBINDAMU huo wa KITANZANIA ...Ungemfanya huyo Mgeni ..ATUHESHIMU na kutodhubutu kutupangia aina za NDOA kabla ya kutupa MISAADA!

Kukimbizana na vijana mtaani kwa risasi na mabomu ...What a SHAME!!
 
Nguvu ya umma na wabunge 23?

Duh! Magamba kweli! Wabunge ndiyo UMMA? Chama cha Hosni Mubaraka huko Misri (NDP) kilikuwa na Wabunge wengi sana Bungeni karibu asilimia 80 ya Wabunge wote -- lakini ona nguvu ya UMMA ilivyomtokomeza.

Siku nyingine jaribu haidhuru kutumia kichwa chako cha nazi katika kufikiri badala ya makalio yako!
 
Mbowe na dr Slaa na Tindu Lussu wamekamatwa kituoni,ila watu wamegoma kufanya kazi leo na hakuna usafiri na watu wameanza kujikusanya tena uwanjani,Mungu tubariki CHADEMA,wao CCM wana pesa na polisi na mafisadi,sisi CHADEMA tuna MUNGU anayetulinda.
 
Back
Top Bottom