Viwanja vinauzwa Mbezi Beach

Kitomai

JF-Expert Member
May 21, 2009
1,061
281
Vipo Mbezi Kunguru. Mbezi Kunguru ipo Mbezi juu unapitia njia ya Masana Hospitali, St Joseph Millenium Secondary. Vipo umbali wa km 6.5 kutoka Bagamoyo Road. Vipo katika shamba lenye ukubwa wa ekari mbili na zaidi ambalo linagawanywa katika vipande vya mita 30 kwa 25.

Kila kipande kinauzwa shilingi 8mil. Eneo kubwa la shamba lipo katika mwinuko, hivyo upepo mwanana tokea Bahari ya Hindi unakufikia vizuri. Vipo katika eneo ambalo ujenzi wa makazi mapya unaendelea kwa kasi, unaweza kutazama picha za makaazi mapya ya wakaazi waliopiga hatua kidogo ambayo wewe unaijongea.

Wahi kununua mapema kabla upanuzi wa Bagamoyo Road haujakamilika na barabara iendayo Goda haijawekwa rami, ukarabati wa hizo utaathiri bei ya hivyo viwanja. Huduma za umeme na maji zipo karibu na eneo hilo. Pia lipo karibu na Shule ya Msingi Kunguru.

Mashariti na Vigezo kuzingatiwa

Piga simu namba 0717114409 upatiwe ufafanuzi kabla ya kuinua mguu wako kuja kuvitazama.

KARIBU!
 

Attachments

  • DSC09114.JPG
    DSC09114.JPG
    63.7 KB · Views: 169
  • DSC09115.JPG
    DSC09115.JPG
    49.5 KB · Views: 193
  • DSC09118.JPG
    DSC09118.JPG
    53.2 KB · Views: 204
  • DSC09120.JPG
    DSC09120.JPG
    47.8 KB · Views: 153
  • DSC09121.JPG
    DSC09121.JPG
    42.1 KB · Views: 157
  • DSC09122.JPG
    DSC09122.JPG
    42.7 KB · Views: 152
  • DSC09124.JPG
    DSC09124.JPG
    22 KB · Views: 140
milioni 8 tuuuu kwa bei za sasa kwa plot kule Mbezi Beach ni uongo!!. Labda Mbezi ya kuelekea Moro.
Correct me if I'm wrong
 
Mbezi Beach huwezi kupata plot for only 8 million TSH.
Hebu angalia hiyo bei vema
 
hapo vilipo unakuwa unaiacha mbezi beach unaelekea uelekeo wa mbezi ya kimara
 
Narudia tena, plot kuuzwa only for 8 million TSH maeneo Mbezi Beach ni uongo!!. Kuna harufu ya kuingizana mjini hapa.
 
Unawambia mbezi beach?? Masana yenyewe siyo mbezi beach!! Kwanini usiwambie viwanja vipo Goba??? St Joseph kule ni Mbezi Beach???

watanzania tutaacha lini kujikweza??
 
nilivyo na hasira na matapeli wa viwanja nikona mtu anadanganya hata location ya plot tu..natamani nimpe ya chembe!!! Humu ni magreat thinkers tu ukitaka utapeli nenda kijiweni
 
Mkuu unaongelea mbezi kimala bonyokwa au mbezi beach hii ya mbele ya mwenge? kiwanja milion 8 mbezi beach? ata Tandale upati kwa hiyo bei
 
mbezi beach huwezi kupata plot for only 8 million tsh.
Hebu angalia hiyo bei vema
umeshaambiwa ni mbezi kunguru 6.5km kutoka bagamoyo road. Huelewi nini sasa? Kama unataka kulipa zaidi kalipe ila hiyo bei kwa maeneo hayo pengine iko juu. Nafikiri hayo maeneo huyajui
 
Unawambia mbezi beach?? Masana yenyewe siyo mbezi beach!! Kwanini usiwambie viwanja vipo Goba??? St Joseph kule ni Mbezi Beach???

watanzania tutaacha lini kujikweza??

hilo eneo mi nalifahamu vizuri...hata bure sichukui kiwanja kule....ni eneo ambalo hata umeme haujafika...infact ni Goba..huwezi ukapaita mbezi beach
 
wabongo wagumu kuelewa lugha ya business!viwanja vipo goba!ila muuzaj kapamba kwa kuita mbez beach!hata konda wa daladala huwa anasemaga seat za kulala ndani,wakati gari limejaza mbaya.
 
Back
Top Bottom