Viwanja vinauzwa Gezaulole Kigamboni na Luguruni kwa Kolimba

Nyati, mradi wa Makazi wa Luguruni upo kwny hatua ya tathmini na hauna athari yoyote kwa wamiliki, mradi wa chuo kikuu cha Muhimbili upo Kwembe, na bahati nzuri nimeushuhudia mchakato kwa karibu zaidi mpk hatua za mwisho za kuwalipa fidia wakazi wa maeneo yatakayoingia kwny umiliki wa Muhimbili! Kwa hy Nyati usihofu, kiwanja changu kipo karibu na makazi ya Mwenyekiti wa CCM Mzee Mbonde, karibu sn!

Bwana Kisusi,
Nadhani utakuwa msaada mkubwa kwa ndugu yangu mmoja.
Alionyeshwa eneo moja huko kwembe (Kwembe Kati) sehemu iitwayo "maduka sita" kuwa mmiliki wake anauza viwanja. Eneo hilo kwa maelezo yake limepakana na eneo la mradi (lililopimwa). Ndugu huyo alisita kulinunua japo wapo ambao wamenunua siku za karibuni hapo hapo kwa huyo mmiliki.
Sasa mkuu, kwa uzoefu wako wa hayo maeneo tumshauri vipi huyu ndugu. eneo amelipenda (about 2000 sqm @ Tzs 8m) ila anahitaji ushauri.
 
mzee viwanja vyako vya kienyeji hatuvitaki, kwa sababu viwanja hivyo vya kienyeji vinapagaisha unaweza kujenga nyumba yako kisha akaja mwingine akaziba barabara ya kuja kwako.
 
Anachotakiwa kufanya ni kutosikiliza maneno ya muuzaji au wapambe, aende ngazi husika km vile ofisi ya serikali ya mtaa, ikibidi afike Wizara ya Ardhi kwa ufafanuzi zaidi. Mradi wa Muhimbili haujachukua maeneo yote ya Kwembe, kuna baadhi ya sehemu za kwembe bado ni ardhi halali kwa makazi ya wananchi. Kwa hy kwa kumsaidia ni kwamba asiishie kuckiliza ushauri wa watu, aende zaidi ya hapo kwa kufatilia kwa uongozi husika.
 
mzee viwanja vyako vya kienyeji hatuvitaki, kwa sababu viwanja hivyo vya kienyeji vinapagaisha unaweza kujenga nyumba yako kisha akaja mwingine akaziba barabara ya kuja kwako.

Pole bwana fidodido, kwa taarifa yako ni kwamba: Gezaulole ni mojawapo ya kijiji chenye mpango bora kabisa wa ujenzi kati ya maeneo mengi ya Dar, kuna mitaa, barabara, na miundo mbinu yote ya huko imeendelezwa, vilevile kwa Mbezi ya Luguruni kwa Kolimba. Kwa hy km hauna hvy vijisenti vya kunishawishi nikumilikishe ardhi yangu piga kimya tu, yaani ipotezee km vp wenye mlungula ndo watasema nami! Baki na fikra zako za kikoloni!
 
Sikia Kisusi,
Biashara inahitaji moyo,
Hata kama mtu sie mnunuzi, kutaja kujua zaidi inasaidia na wengine pia.
Kama mtu katoa reference ukubwa+bei ya vilivyopimwa,
Ulitakiwa uje na ushawishi wa kuwaelewesha wateja wako waelewe.
Hayo mambo ya kudai kwa kua mtu sio mnunuzi basi asikuulize yatakupototezea au kukupunguzia wateja.
Kwa maelezo yako tu ni kua mtu anunue tu huko Gezaulole kisha ategemee huruma ya Wizara.
Tunajua ardhi ni yako una uwezo wa kuweka bei uitakayo, but accept challenges ndo utafika mkuu (he/she???!!)
 
Thanks a lot SHARK!!

Hapa nahisi mambo ya "kekundu, kekundu........ndiyo waliwao"

Kwaheri.
 
Jamani mi nadhani uhalali au kuthibitishwa kwa viwanja hivyo c tatizo, upo serious na kununua check nami nikupe undani wa yote hayo. Hakuna kiwanja chenye ujanja ujanja wala kilicho kwny hatari ya kuzuiwa na serikali. Kigamboni kuna stop order ya ujenzi ila ukienda wizara ya ardhi wakuu wenyewe wanakwambia nyumba itakayokidhi mahitaji ya mradi itakuwa considered, Shark, jaribu kupita huko Kibada na Gezaulole utazame "wenye nazo" wanachokifanya. Ngonjera ya mradi hata Anna Tibaijuka hana majibu ya kuwaeleza wana Kigamboni, so km nawe ni "mwny nazo" km wenzio kaangushe banda lako tu! Kuhusu bei nadhani unasahau km "inflation rate" ya Tz ipo 16.8 mpk jana, na dola ni 1,720 kwa change ya leo. Jipange mkuu, soko huria, land value appreciation na mahitaji yangu binafsi ndo bases za bei ya viwanja vyangu. NB: MI SI DALALI, NI MMILIKI HALALI WA ARDHI HIYO NA NIMEFATA TARATIBU ZOTE ZA UMILIKI KWA NGAZI YA SERIKALI YA MTAA!

Stop order imetolewa kimaandishi, ruhusa ya ujenzi inatolewa kwa mdomo........hili nalo neno.......tafakari chukua hatua.

Unamkumbuka yule Mkuu wa Mkoa aliyekataa kutoa vibali vya kuligawa shamba moja kule Kagera mwaka jana, akata maandishi, japo Kikwete alisema wapewe wakati akipiga kampeni?
 
Sikia Kisusi,
Biashara inahitaji moyo,
Hata kama mtu sie mnunuzi, kutaja kujua zaidi inasaidia na wengine pia.
Kama mtu katoa reference ukubwa+bei ya vilivyopimwa,
Ulitakiwa uje na ushawishi wa kuwaelewesha wateja wako waelewe.
Hayo mambo ya kudai kwa kua mtu sio mnunuzi basi asikuulize yatakupototezea au kukupunguzia wateja.
Kwa maelezo yako tu ni kua mtu anunue tu huko Gezaulole kisha ategemee huruma ya Wizara.
Tunajua ardhi ni yako una uwezo wa kuweka bei uitakayo, but accept challenges ndo utafika mkuu (he/she???!!)

Sir Burn, mi ni HE tena kipande cha baba, chalenge za wachangiaji wengi nimezipokea, kiukweli cjaweza kuandika kwa kina kueleza ubora wa hvy viwanja, nimetoa namba ya mkononi ili kama unahitaji kupata maelezo ya ziada unipigie, sasa wengi wa wanaotoa mchango hawana mawazo ya kujenga ila ni vishawishi kwa watu wasinunue, kitu ambacho kibiashara hata ukiwa na moyo wa chuma huwezi vumilia. Mi nataraji hao watoa changamoto wajadili hvy viwanja na c kunijadili mimi kwa kuniita tapeli, mlanguzi, laghai na mengineyo waliyotapika kwny michango yao! Kiujumla huwa sisumbuliwi sn na wapiga kelele, natambua nikifanyacho. Hlf ukweli wa biashara ni kwamba: mnunuzi wa kweli atahoji vitu vya msingi na c kuleta kejeli kwny biashara!
 
Nadhani Shark hajafanya vibaya kutaka ufafanuzi na kuweka mambo wazi ili kutoa watu wasiwasi na kuwapa watu taarifa ambazo ni muhimu sana na sio kila mtu anazijua.
Shark kwa maelezo yako mimi binafsi nimepata mwanga na ulewa fulani. Umefanya vizuri sana
 
Back
Top Bottom