Viwanja: Gezaulole, Kigamboni - Manispaa ya Temeke tarehe ya kubandika majina imepita?

Mimestaajabishwa na idadi ndogo ya majina iliyotolewa (742) ikilinganisha na idadi ya viwanja 1800 viliyoahidiwa katika matangazo ya awali.Pili kati ya wachache waliopota tunaona baadhi ya majina yakijinyakulia viwanja zaidi ya kimoja kama ionekanavyo hapo chini:
S/NMWOMBAJIUJAZO
52ALLY JUMA MWINSHEHEUJAZO WA CHINI
53ALLY JUMA MWINSHEHEUJAZO WA KATI
54ALLY JUMA MWINSHEHEUJAZO WA KATI
110BALOZI DAUDI MWAWAGO
111BALOZI DAUDI MWAWAGO
112BALOZI DAUDI MWAWAG & ZUHURA DAISYUJAZO WA CHINI
121BONIFAS MSABILA BAHILIUJAZO WA KATI
122BONIFAS MSABILA BAHILIUJAZO WA KATI
209FARAJI RAJABU MANENO
210FARAJI RAJABU MANENOUJAZO WA KATI
401LEAH PROSPER MLIMILAUJAZO WA CHINI
402LEAH PROSPER MLIMILAUJAZO WA KATI
403LEAH PROSPER MLIMILAUJAZO WA CHINI
468MOHAMED BAKARI ALLY MANJAUJAZO WA KATI
469MOHAMED BAKARI ALLY MANJA

Hii ndio Tanzania tuipendayo kwa moyo yote...!!
 
v) Orodha ya majina ya waombaji watakaouziwa viwanja itabandikwa katika Mbao za Matangazo za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na pia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia tarehe 29.6.2012:help:
 
v) Orodha ya majina ya waombaji watakaouziwa viwanja itabandikwa katika Mbao za Matangazo za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na pia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia tarehe 29.6.2012:help:

Du mkuu mbona tarehe ilishapita? Nasikia wanashikilia kwanza ili tukatoe hongo. Kiwanja kwa sasa kinapatikana kwa shilingi laki tano hadi million moja kwa hongo kwa wahusika. Ninaomba sana TAKUKURU ofisi zenu ziko tu jirani na manispaa ya temeke naombeni tengenezeni mtego. Kweli ninasema haya maana yanayoendelea pale sasa hivi ni kutanguliza 500,0000-1,000,000 kulingana na size ya kiwanja unachotaka. Ni habari ya kweli si uzushi. I never lie. Naomba vyombo vya habari chunguzeni hili au kama kuna aliyeomba aende pale ajifanya anatoa pesa ili apate evidence arushe hewani. Too sad!!
 
jamani hayo majina amjamaliza kuchakachua :israel:
 
Baadhi ya wananchi waliofika kusoma majina hayo walisikika wakilalamikia hali hiyo, huku wakisema kuwa kinachoonekana ni vigogo kupendelewa na kuwanyima wananchi wa kawaida.

Katika orodha hiyo, majina yanayosomeka ni pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama; Naibu Spika, Job Ndugai; Waziri wa Mawasiliano, Sanyansi na Teknolojia, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Kwa upande wa Makatibu Wakuu wa Wizara wapo, Dk Florence Turuka (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhan Kijjah; Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omary Chambo na Dk Idris Rashid ambaye ni Gavana wa Zamani wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Pia wamo Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk Didas Masaburi, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa; Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Suleinan Kova.

Wengine ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu; Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh na Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili(MNH),Marina Njelekela.

Kwa upande wa wabunge wamo Dk Augustine Mrema (Vunjo - TLP), Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe; Mbunge wa Kibaha Mjini (CCM), Sylvester Koka; Mbunge wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan; Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Dk Cyril Chami na Mbunge wa Singida Kusini (CCM), Mohamed Misanga.

Wengine ni Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila; Mbunge wa Igunga (CCM), Dk Peter Kafumu na Mbunge wa Bukene (CCM), Seleman Zedi.

Wabunge wa Viti Maalumu (Chadema), Maulida Komu na Suzan Lyimo, Viti Maalumu CCM, Dk Mary Mwanjelwa na Zakhia Meghji ambaye ni mbunge wa kuteuliwa.

Orodha hiyo pia inaonyesha majina ya ukoo yanayofanana na majina ya baadhi ya viongozi ambao ni Miraji Kikwete, Khalfan Kikwete, Juanita Mramba, Suzan Mkapa, Zainab Mkomwa, George Rupia, Maimuna Mfutakamba, Mary Membe, Pharles Ngeleja, Judith Kahama na Wilfred Mwanri
 
Back
Top Bottom