Viwanja: Gezaulole, Kigamboni - Manispaa ya Temeke tarehe ya kubandika majina imepita?

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji viwanja. Katika awamu hii ya pili, inatarajiwa kuuza fomu za maombi ya viwanja vyenye ukubwa na matumizi mbalimbali kwa utaratibu ufuatao:-

i) Fomu za maombi ya kununua kiwanja zitaanza kutolewa tarehe ...11.06.2012 hadi tarehe 15.06.2012 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

ii) Kila Mwombaji atapaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha shilingi elfu thelathini (Tshs 30,000/=) katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa. Fedha hizo hazitarejeshwa.

iii) Mwombaji atajaza nakala 2 za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana.

iv) Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la Mradi ambao walitambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, nao wanatakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule ulioainishwa hapo juu.

v) Orodha ya majina ya waombaji watakaouziwa viwanja itabandikwa katika Mbao za Matangazo za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na pia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia tarehe 29.6.2012:help:

vi) Utaratibu wa kulipia Ankara za malipo ya viwanja pamoja na muda wa kulipia utatolewa sambamba na tangazo la orodha ya waliofanikiwa kuuziwa viwanja na litakalobandikwa katika mbao za Matangazo zilizotajwa hapo juu.

JEDWALI: VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA:banplease:

Na. Aina ya matumizi Gharama kwa kila Mita ya mraba

  1. Makazi pekee (Ujazo wa juu, kati na chini) 8,000
  2. Makazi na Biashara 9,000
  3. Biashara 20,000
  4. Huduma za Jamii 8,000
  5. Ibada/kuabudu 8,000
  6. Viwanda vidogo vidogo (Service trade) 15,000
  7. Makazi maalumu(Housing Estate) 10,000
  8. Viwanja Vyenye nyumba (kwa wenye nyumba waliotambuliwa kabla ya upimaji na walioko ndani ya eneo la viwanja) 3,000

Imetolewa na,

MKURUGENZI W MANISPAA:tea:
TEMEKE

Attachments

  • mkurugenzi.jpg
    mkurugenzi.jpg
    61.5 KB · Views: 161
Tulishapata viwanja wenzio kabla ya hilo tangazo pole ... Mmepigwa changa
 
tunaisubiri plot allocation committee ya manispaa ya temeke ichambue na kuja na majina ya watakaofanikiwa kupata viwanja. alopata kiwanja leo hii na atupe uthibitisho.
 
  • A%20S%20465.gif

umejuaje? wakati atujatangaziwa ;;au ndo ushapata mwenzetu
 
Majina yapo kwenye website ya Temeke municipal council (www.tmc.go.tz). Cha kuchekesha majina yamepangwa kufuata alphabet lakini mheshimiwa mmoja majina yake mawili yanaanza na "M" lakini kwenye list ni wa pili. I smell something fishy here.
 
Aaaah, wamenitosa tena. Naona majina ya Mawaziri wa JK tu hapo..duh, yaani pamoja na kuuziwa nyumba za serikali bado wanaendelea kukaba hadi huku Gezaulole..this is too much.
 
Nchi yetuuuuuuu! iiiinchi yetuuu....

Bila rushwa hupati kiwanja, alinimabia ofisa mmoja wa manispaa....ni kweli sipata.
 
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imepima viwanja 1,800 katika eneo la Gezaulole ikiwa ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mradi wa Upimaji viwanja. Katika awamu hii ya pili, inatarajiwa kuuza fomu za maombi ya viwanja vyenye ukubwa na matumizi mbalimbali kwa utaratibu ufuatao:-

i) Fomu za maombi ya kununua kiwanja zitaanza kutolewa tarehe ...11.06.2012 hadi tarehe 15.06.2012 katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke.

ii) Kila Mwombaji atapaswa kulipia ada ya maombi ya kiasi cha shilingi elfu thelathini (Tshs 30,000/=) katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo mkabala na Uwanja Taifa. Fedha hizo hazitarejeshwa.

iii) Mwombaji atajaza nakala 2 za fomu ya maombi na kuzirejesha zikiwa zimebandikwa picha 3 za ukubwa wa pasipoti. Mwisho wa kurudisha fomu hizo ni tarehe 18.06.2012 saa 8 mchana.

iv) Wakazi wenye nyumba na mashamba ndani ya eneo la Mradi ambao walitambuliwa kabla ya zoezi la upimaji kuanza, nao wanatakiwa kununua fomu za maombi kwa utaratibu uleule ulioainishwa hapo juu.

v) Orodha ya majina ya waombaji watakaouziwa viwanja itabandikwa katika Mbao za Matangazo za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni na pia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia tarehe 29.6.2012:help:

vi) Utaratibu wa kulipia Ankara za malipo ya viwanja pamoja na muda wa kulipia utatolewa sambamba na tangazo la orodha ya waliofanikiwa kuuziwa viwanja na litakalobandikwa katika mbao za Matangazo zilizotajwa hapo juu.

JEDWALI: VIWANGO VYA GHARAMA YA VIWANJA:banplease:

Na. Aina ya matumizi Gharama kwa kila Mita ya mraba

  1. Makazi pekee (Ujazo wa juu, kati na chini) 8,000
  2. Makazi na Biashara 9,000
  3. Biashara 20,000
  4. Huduma za Jamii 8,000
  5. Ibada/kuabudu 8,000
  6. Viwanda vidogo vidogo (Service trade) 15,000
  7. Makazi maalumu(Housing Estate) 10,000
  8. Viwanja Vyenye nyumba (kwa wenye nyumba waliotambuliwa kabla ya upimaji na walioko ndani ya eneo la viwanja) 3,000

Imetolewa na,

MAJINA HAYA HAPA

[video]http://www.tmc.go.tz/MAJINA%20YA%20WALIOPATA%20VIWA NJA.pdf[/video]

MKURUGENZI W MANISPAA:tea:
TEMEKE
 
Aaaah, wamenitosa tena. Naona majina ya Mawaziri wa JK tu hapo..duh, yaani pamoja na kuuziwa nyumba za serikali bado wanaendelea kukaba hadi huku Gezaulole..this is too much.

ndenga,

..POLE!!

..nimeona mpaka MAREHEMU nao wamepata.

..kuna Daudi Mwakawago[r.i.p] kapata viwanja viwili.

..pia kuna Sekoutoure Mndeme[r.i.p] naye kapata kiwanja.

..maombi yalipelekwa lini??

..pia hawahakiki kabla ya kutoa orodha ya mwisho??

NB:

..pia kuna vigogo kama Halfani Kikwete,Mwandosya,Balozi Seif Iddi, Ghasia,etc etc.
 
Wizi mtupu,
Wameuza jumla ya form 20,000 kwa ajili ya viwanja hivyo tu??
 
UTAKUWA NABII KM ULIVYOTABILI :israel:

..jamani mbona kuna MAREHEMU wamepata viwanja??

..Balozi Mwakawago, na Sekoutoure Mndeme, nao wamepewa!!

..sasa hao ni wale maarufu, nina hakika kutakuwa na wengine kibao, wasiokuwa na majina makubwa.
 
ebwe na marehemu tena?

..jamani mbona kuna MAREHEMU wamepata viwanja??

..Balozi Mwakawago, na Sekoutoure Mndeme, nao wamepewa!!

..sasa hao ni wale maarufu, nina hakika kutakuwa na wengine kibao, wasiokuwa na majina makubwa.
 
majina yaliyotolewa ni ya mradi wa awamu ya kwanza ambayo yanamuda mrefu toka yametoka.naona jf imeingiliwa
 
wajani nilidhani utani juu ya marehemu kupata viwanja angalia hapo

BALOZI DAUDI MWAWAGO
111
BALOZI DAUDIZ MWAKAWAGA
112
BALOZI MWAKAWAGO & ZUHURA DAISY
 
Back
Top Bottom