Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,920
- 31,161
Ni vizuri bunge letu likawa na wabunge wasomi lakini sipendi kuwepo na sheria ya kukataza wasiosoma kuwa na haki ya kugombea ubunge,ningependa zaidi wananchi waachiwe nafasi ya kuamua wenyewe wanataka kuwakilishwa na mtu wa namana gani.
Rorya wamemkataa Profesor Sarungi wakamchgua mtu wa darasa la saba,sipendi kuwahukumu vibaya wapiga kura wa Rorya yamkini wamebaini mapungufu ya kuwakilishwa na Mzee Sarungi.Moja kubwa mara nyingi hawa wasomi kama Professor Sarungi hawakai kwenye majimbo yao sana sana wanaishi Dar es Salaam Ostabay na Masaki wapiga kura wanaona hakuna haja ya kumchagua msomi ataeishia kuishi Dar ni bora kumchagua darasa la saba atakaishi na kushiriki kutatua kero za vijijini.Wasomi wa aina ya Professor Sarungi wanawawakilisha wasomi wengi sana ambao mara nyingi wanaenda vijijini wakati wa mchakato wa kuomba kura wakishapata ubunge hawaonekana tena mpaka uchaguzi mwingine.Nadhani hii ni sababu moja kubwa kwanini wananchi siku hizi hawapendi kuwakilishwa na wasomi.