Vituo vya mafuta Dar vyagoma!

BIASHARA YA MAFUTA ITAIFISHWE MARA MOJA

KIONGOZI MKUU wa mgomo wa vituo vya mafuta inavyoelekea ni OILCOM ambao walianza kuficha mafuta ya peteroli kuanzia mwishoni mwa mwaka jana.

Sasa ni Watanzania vs Wauza Mafuta. Zao au zetu. Iweje Marekani bei ya mafuta imeshuka toka dola 4 kwa lita hadi kufikia dola 0.50 na sisi tukubali kufanywa mabwege tu katika nchi yetu tena na wahamiaji na watu wengine wa kupita tuU!

Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba TUTAIFISHE BIASHARA YA MAFUTA UPYA mbona Warussi wameondokana na upuuzi huu na maisha yao yanakwenda kama kawaida.

Tumewapa watu binafsi nafasi lakini wanajifanya kichwa ngumu.

Rais Kikwete na CCM kwa faida yenu na ya Watanzania tafadhali taifisheni BIASHARA YA MAFUTA TANZANIA maana ni WIIIIIZI MTUUUUPU!
 
SHYLOCK HAWA WASHUGHULIKIWE MARA MOJA.

NAKUBALI hoja ya kutaifisha KAMPUNI ZA MAFUTA NA BIASHARA ya usafishaji mafuta nchini.

Zanzibar wanaweza kuanza kwa kujgena kituo cha usafishaji mafuta Pemba na kununua meli moja ya kubeba mafuta na hivyo kuifanya biashara hiyo ya serikali peke yake.

Hapa Bara tuanze kwa kutaifisha OILCOM ambao ndio wanaonesha jeuri na kiburi zaidi na wanaoongoza mgomo wa vituo vya peteroli unaoendelea kote hapa jijini Dar es salaam.

Serikali isifanye mzaha na kina SHYLOCK HAWA -WASHUGHULIKIE mara moja na wasidhani serikali ya Kikwete ni serikali ya kukokotwa na kuburuzwa na kila mwenye kutaka kudhulumu haki za wengine eti!
 
Ninafurahi kwamba mjadala huu umeanza kuwa na 'punch' na nina hakika tunawakilisha hasira ya watanzania wote kwa hawa Shylock!!!!! Wasio na aibu na uchungu wa maendeleo ya nchi yetu na watu wake!!!!!
 
HAWA jamaa wanataka kutupeleka kwenye hali iliyoko katika nchi kama Nigeria. Yaani, wanataka kuanza KUUZA PETEROLI KWA MACHINGA halafu machinga ndio wawe wanawauzia wenye magari.

WAMECHEMSHA. Janja ya nyani kushaonekana bana!!!

Ninaunga mkono hoja RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE TAIFISHA BIASHARA YA MAFUTA MARA MOJA.

Waoneshe wenye kula wananchi UPUTIN wako lakini sio smile yako safari hii!!!
 
I beg to differ. Hii Regulatory body (Ewura) should have also tackled the issue of wholesale prices. (Depots).
Pili kama biashara ya mafuta ni rahisi, serikali should empower TPDC nayo iingie kwenye biashara ya mafuta.
Enzi za Mwalimu tulipanga mpaka bei za nyama kenye butcha. Matokeo yalikuwaje?
 
Nimezungumza na mnene mmoja wa GAPCO amenithinitishia kuwa kuna stock ya kutosha ya mafuta katika depot za makampuni yote makubwa. Anasema hata wao (waagizaji) wameshangazwa na kukosekana kwa petroli wakati ipo ya kutosha kwenye stock zao. Wanahisi kuwa huenda it was a case of bad timing on part of retailers ambao walishindwa kuagiza kiasi cha kutosha kuhimili mahitaji wakati wa weekend iliyopita. Lakini amenihakikishia kuwa hakuna haja ya ku-panic kwa sababu mafuta yapo ya kutosha na yameshaanza kusambazwa
 
“Mafuta si kwetu tu hata depot ya BP hakuna na ndio sababu unaona tunauza dizeli na mafuta ya taa pekee,” alisema mfanyakazi wa Kituo cha BP Fire. Wafanyabiashara wa bidhaa hiyo wamedai mahitaji ya petroli nchini ni makubwa kuliko dizeli na mafuta ya taa na ndiyo sababu yanamalizika mapema.

NI toka lini wamejua hawana hayo mafuta??? yani hawakujua kama mafuta yataisha si muda mrefu???
 
Kama ni kweli haya ndio yanaendelea, serikali inayowajibu wa kukagua hifadhi zao zote za mafuta kijiridhisha kwamba mafuta yapo ila wamekataa kuyauza then wawafungulie kesi ya kuhujumu uchumi. Kama hawakuridhika kushushwa kwa bei wangetoa tamko rasmi kwamba hawatauza mafuta na si vinginevyo.

The act mount to econominc sabboutage(spelling haziko sawa) maana wamekataa kwa makusudi ili kucreate demand kubwa na kuuza mafuta kwa bei ya juu.

Mrema tutakukumbuka sana maana watu kama hawa naamini usingewahurumia hata kidogo

Nji hii Bwana Hao ndio walewale waliowachangai wanamtandao na hivyo wanataka warudishe hela zao na pia wanatafuta za kuwapa mwakani!!!Kwani hamjui?
 
SHYLOCK HAWA WASHUGHULIKIWE MARA MOJA.

NAKUBALI hoja ya kutaifisha KAMPUNI ZA MAFUTA NA BIASHARA ya usafishaji mafuta nchini.

Zanzibar wanaweza kuanza kwa kujgena kituo cha usafishaji mafuta Pemba na kununua meli moja ya kubeba mafuta na hivyo kuifanya biashara hiyo ya serikali peke yake.

Hapa Bara tuanze kwa kutaifisha OILCOM ambao ndio wanaonesha jeuri na kiburi zaidi na wanaoongoza mgomo wa vituo vya peteroli unaoendelea kote hapa jijini Dar es salaam.

Serikali isifanye mzaha na kina SHYLOCK HAWA -WASHUGHULIKIE mara moja na wasidhani serikali ya Kikwete ni serikali ya kukokotwa na kuburuzwa na kila mwenye kutaka kudhulumu haki za wengine eti!

Je mnajua kampuni hizo zilichanga Dollar ngapi (achilia mbali EPA) wakati wa kampeni za uchaguzi ndani ya ccm na kitaifa mpaka JK akaibuka kidedea? mkilijua hilo mmepata ufumbuzi wa jeuri yao,
 
Mkuu PM,

Binafsi nimeshangazwa SANA na jambo hili na kujiuliza HIVI TUNAYO SERIKALI KWELI? Nafikia wakati nakata tamaa kabisa.

Issue behind vituo vya mafuta wasibambikizwe wahindi etc, wazalendo wengi tena wanasiasa wanamiliki vituo hivyo kwa migongo ya waarab 'wachukua kamisheni' tu.

Hakuna udhibiti wa soko huria Bongo? Pia siwalaumu wafanyabiashara pekee, nawabebesha lawama zaidi EWURA. Inaelekea hawajui walitendalo, maamuzi yalikuwa ya kukurupuka? Kwa manufaa ya nani? Athari ya hali hii ni kubwa sana kwa uchumi wa taifa. Kifupi ni uhujumu uchumi wa taifa kwa kiwango kikubwa sana. Inasikitisha SANA

Hapana Mkubwa. EWURA wanajua wanalolifanya na wako sahihi kabisa. EWURA wamefanya vikao kadhaa na wamiliki wa mafuta pamoja na TRA kwa kupitia makaratasi yote ya kununulia na kusafirishia mafuta ambayo aghalabu ni ushahidi wa namna bei za mafuta zinavyopatikana, ndipo wakajadili kuhusu bei dira (indicative prices) kulingana na ushahidi wa makaratasi hayo, ambapo pia walikubaliana kuhusu matumizi ya bei hizo pasipo matatizo. Walijadili pia kiasi kilichobaki katika maghala yao pamoja na kilichouzwa. EWURA wamekuwa wakichapisha majadiliano hayo mara kwa mara katika vyombo vya habari na kuelezea maafikiano hayo kwa kila hatua, na hakuna mmiliki wa kituo chochote cha mafuta aliyewahi kukanusha habari hizo za EWURA kuwa sio sahihi. Sasa nashangaa leo wamegeuka na kuficha mafuta.
Suala la kuadimika mafuta ni uharamia wa wamiliki wa vituo vya mafuta kwa kuficha bidhaa kwa makusudi ili kusababisha uadimu na kupanda kwa bei pasipo sababu. Makosa kama haya (price fixing) kwa nchi zilizoendelea ni hatia kubwa sana, sijajua sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu hili.
 
Makosa kama haya (price fixing) kwa nchi zilizoendelea ni hatia kubwa sana, sijajua sheria za Tanzania zinasemaje kuhusu hili.

- Mkuu wangu uko karibu sana na ukweli, price fixing inatokea tu knapokuwa na kampuni moja kuruhusiwa na serikali kuwa na nguvu kubwa ya umiliki wa bidhaa flani bila kuwa na sheria za kutosha kuhakikisha competition katika biashara ya ile bidhaa, hili tatizo lipo kwenye makampuni ya simu Tanzania pia,

- Ukisoma vizuri hoja nyingi kwenye hii thread utagundua kuwa this ishu is too complicated kwetu wananchi, ndio maana hata serikali haina clue on it! I mean kuna mpaka wananchi wanaoshauri serikali ijiingize kwenye biashara ya mafuta!
 
Back in the days serikali ilikuwa inaagiza crude oil halafu TIPER inasafisha hapa hapa nchini. Sijui tukaingiwa na PEPO gani tukaamua kuiua kampuni ile na kuachana kabisa na uagizaji wa mafuta.
 
Duuh! Lakini vituo vya SHELL si viko vichache sana kwa Dar?! Kama SHELL wamegoma nafikiri hizo kampuni nyingine kama BP, Agip, GAPCO, TIOT, Caltex, Total, na nyinginezo nyingi tu zinaweza kukidhi mahitaji. Au hapa ulimaanisha SHELI = ANY FILLING STATION??!!

Mzee niliandika kuwa sorce ni michuzi. Nili-copy na ku-paste. Anyway, TZ Sheli = filling station; Colgate = Tooth Paste; Kiwi = Shoe polish, you name it, bora Kiswanglish kinapanda. Kama hujui hivyo kiswanglish tembelea michuzi blog utakumbana nayo at MICHUZI
 
Nimezungumza na mnene mmoja wa GAPCO amenithinitishia kuwa kuna stock ya kutosha ya mafuta katika depot za makampuni yote makubwa. Anasema hata wao (waagizaji) wameshangazwa na kukosekana kwa petroli wakati ipo ya kutosha kwenye stock zao. Wanahisi kuwa huenda it was a case of bad timing on part of retailers ambao walishindwa kuagiza kiasi cha kutosha kuhimili mahitaji wakati wa weekend iliyopita. Lakini amenihakikishia kuwa hakuna haja ya ku-panic kwa sababu mafuta yapo ya kutosha na yameshaanza kusambazwa

Sikubaliani na huyo mnene kusema kuwa bad timing ya hao wauzaji, kama ingekuwa kituo kimoja au hata vitatu lakini kwa vituo vingi kwenye maeneo mengi siyo bad timing, nafikiri wanataka ku create scarcity ili wapandishe bei kwa theory ya demand and supply. Hapa Serikali iingilie kati kuondoa tatizo hili na lisirudiwe tena huko siku za mbele. Tulizoe uhaba wa mafuta katika utawala wa awamu ya kwanza lakini tangu awamu ya pili mpaka hii leo tumesahau kabisa matatizo kama haya tunaomba wahusika wayashughulikie kwa nguvu zote.
 
Una hisa katika hayo makampuni ya mafuta?
hizo indicative prices unazodai zipo chini una theory gani ya kusupport ur argument?
Mkulu nakuheshimu....

Mkuu Bonnie1974, sina hisa ktk. kampuni lolote. Mimi mlaji tu - nachangia hoja kutokana na ninavyojua (data nilizonazo). Siyo theory, ila ukweli ni kwamba ukichukulia avarage pump prices kwingine kama vile Uganda (Sh 2,850 = $ 1.6); Rwanda (Rwf 924 = $ 1.5); Kenya (Sh 90 = $ 1.2) utaona kwamba EWURA wana propose pump prices za chini (at 1$ or below). Inawezekana pengine ndiyo chanzo cha tatizo.
 
- Mkuu wangu uko karibu sana na ukweli, price fixing inatokea tu kunapokuwa na kampuni moja kuruhusiwa na serikali kuwa na nguvu kubwa ya umiliki wa bidhaa flani bila kuwa na sheria za kutosha kuhakikisha competition katika biashara ya ile bidhaa, hili tatizo lipo kwenye makampuni ya simu Tanzania pia,

- Ukisoma vizuri hoja nyingi kwenye hii thread utagundua kuwa this ishu is too complicated kwetu wananchi, ndio maana hata serikali haina clue on it! I mean kuna mpaka wananchi wanaoshauri serikali ijiingize kwenye biashara ya mafuta!

Nakubaliana na hoja za serikali kujiingiza ktk biashara ya mafuta (ingawa si suluhisho wala suala mwafaka kwa sasa), na nakubaliana na watoa hoja wengine kwamba mafuta yanahusiana moja kwa moja na 'USALAMA WA NCHI'. Tatizo hapa ni kwamba serikali iliua kiwanda cha TIPER bila kufikiri na kutazama mbali zaidi matatizo kama haya ambayo tunakumbana nayo sasa ya uhaba wa bidhaa hii.
 
Serikali nayo imechemka unapoanzisha bifu na hawa watu lazima uwe na plan B ie ua own reserve.
Lazima tutaikumbuka sana TPDC ingekuwepo huu uhuni usingetokea.
Serikali kupitia inteligecia na TRA na EWURA wacheki kama kweli stock imeisha?
Wanajua serikali ya kisanii itawafanya nini?
Discipline has to resume jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Sikubaliani na huyo mnene kusema kuwa bad timing ya hao wauzaji, kama ingekuwa kituo kimoja au hata vitatu lakini kwa vituo vingi kwenye maeneo mengi siyo bad timing, nafikiri wanataka ku create scarcity ili wapandishe bei kwa theory ya demand and supply. Hapa Serikali iingilie kati kuondoa tatizo hili na lisirudiwe tena huko siku za mbele. Tulizoe uhaba wa mafuta katika utawala wa awamu ya kwanza lakini tangu awamu ya pili mpaka hii leo tumesahau kabisa matatizo kama haya tunaomba wahusika wayashughulikie kwa nguvu zote.

Nadhani tayari serikali inachukua hatua kukabiliana na hali hii. Ninapoandika haya, tayari wizara ya nishati ipo kwenye kikao kulijadili hili. Pia, wizara ya viwanda na biashara imewaita wauzaji mafuta wote katika kikao kingine kilichopangwa kufanyika wizarani hapo, nadhani kimeshaanza.
Lakini nadhani cha muhimu katika interventions hizi ni kutafuta suluhishao la kudumu ili tatizo kama hili lisije kujitokeza tena kwa sababu licha ya kusababisha usumbufu, lakini pia linahatarisha maisha
 
Mzee niliandika kuwa sorce ni michuzi. Nili-copy na ku-paste. Anyway, TZ Sheli = filling station; Colgate = Tooth Paste; Kiwi = Shoe polish, you name it, bora Kiswanglish kinapanda. Kama hujui hivyo kiswanglish tembelea michuzi blog utakumbana nayo at MICHUZI

...saloon car=taksii
 
Sheria zilizopo zinatosha kutoa fundisho kwa hio cartel ya mafuta inayosababisha artificial acute shortage of such an essential item. Wengi hapa wamei cite sheria ya uhujumu uchumi ya 1984. HIYO INATOSHA KUTIA HAWA WATU ADABU!

Tatizo letu lingine ni polisi wetu(CID) kufanya kazi kwa mazoea na kusubiri mpaka wapewe maelekezo na wanasiasa ndipo waanze kugather evidence kuwa kuna element ya economic sabotage by hawa wauza mafuta... Haiwezekani vituo vingi vinavyofanya kazi independently vyote viwe vimepitiwa kuagiza mafuta tena vyote siku hiyohiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom