X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,610
- 1,810
Mchanganuo wa jinsi ya kupika vitumbua
Kiasili vitumbua ni chakula ambacho hupendelewa sana na watu wa pwani. Na mara nyingi wamekuwa wakipika kwa kuchanganya na nazi au maziwa nk ili kuvifanya viwe na ladha nzuri zaidi
Mahitaji
1. Mchele wa vip vikombe 2
2.Hamira kijiko cha chai 1
3. Tui la nazi kikombe 1
4. Ute wa mayai 2 (ukipenda)
5. Sukari kikombe 1
6. Unga wa ngano kijiko cha chakula 1
7. Hiriki kijiko cha chai
Maandalizi
1. Loweka mchele katika maji usiku mzima.
2. Chuja maji yote kisha utie mchele katika blender pamoja na tui la nazi, unga wa ngano, hiriki na hamira.
3. Saga hadi uwe laini, mimina katika bakuli, funikia acha sehemu yenye joto ufure hadi ujae mara mbili.
4. Tia sukari na ute wa yai, koroga vizuri.
Choma vitumbua vyako katika moto wa kiasi hadi vipate rangi ya kahawia pande zote mbili.
Tayari kwa kuliwa.
--------
Au
Mahitaji
Unga wa mchele ½ kg
Sukari vijiko 4 vya mezani
Tui bubu la nazi
Mafuta ya kupikia
Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai
Hamira kijiko 1 cha chai
Jinsi ya kuandaa na kupika
Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja
Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako
Weka hiliki koroga hadi Uwe uji mzito.
Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa Yani joto au baridi.
Baada unga kuumuka
Washa jiko weka chuma Cha vitumbua kisha weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto Kisha mimina mchanganyiko kiasi kwenye kikarai maalumu cha kuchomea vitumbua.
Hakikisha Moto sio mkali kitumbuai kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
Ukimaliza kuchoma panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa. Kinywaji utachagua mwenyewe kama ni chau nk.
Michango ya wadau
----Vitumbua (Aina Ya 1)
Vipimo
- 1 Kikombe cha mchele.
- 1 Kijiko cha kulia cha unga wa ngano.
- 3/4-1 Kikombe cha tui la nazi zito.
- 2 Mayai.
- 1 Kijiko cha chai cha hamira.
- 1/2- 3/4 kikombe cha sukari.
- Iliki kiasi upendacho.
Naman Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha na kuroweka mchele ndani ya maji ya baridi masaa manane au siku moja.
- Mimina vifaa vyote ispokuwa sukari, ndani ya blender na usage mpaka mchele uwe umesagika kabisa.
- Mimina sukari ndani ya mchanganyiko na usage tena kidogo tu.
- Mimina mchanganyiko ndani ya bakuli na ufinike. Weka bakuli mahali penye joto ili mchanganyiko uuumuke.
- Mchanganyiko ukisha umuka, weka karai kwenye moto.
- Tumia kama kijiko 1-2 cha chai cha samli kwa kukaangia kila kitumbua.
- Mimina mchanganyiko kiasi kwenye karai kulingana na kikarai unachotumia.
- Kitumbua kikiiva upande mmoja, geuza upande wa pili mpaka kiwe tayari.
- Panga kwenye sahani. unaweza kula vitumbua vikiwa moto au vikipowa.
-----Vitumbua Vya Mchele
View attachment 1606887
Mahitaji
Mchele ......2cups
Tui zito ......1cup
Ute wa yai ......1
Unga wa Sembe ...1 table spoon
Unga wa Ngano …1table spoon
Hamira.........…1 table spoon
Hiliki ..........1 table spoon
Sukari .......½ Cup
Jinsi Ya Kupika
Saga mchele na tui kwenye blender mpaka uwe laini uhakikishe hauna chenga hata kidogo tia yai, hamira na hiliki endelea kusaga. Tia sukari endelea kusaga na mwisho utatia unga wa ngano na wa sembe, saga tena kidogo toa weka kwenye bakuli, acha uumuke.
Ukishaumuka weka kwenye chuma cha vitumbua na uanze kuchoma kwa mafuta pole pole, mpaka uone vimebadilika rangi.
Wapendwa..amani iwe juu yenu!!
I hope u have a great weekend.
Unga wa mchele glass 2 na nusu
Maziwa glass 2
Sukari vijiko 10 vya kulia
Iliki vijiko 2
Hamira vijiko 2
Yai 1
Jinsi ya kutayarisha
Changanya vitu vyote kwenye blender..
Saga kwa dkk 4-6
Mimina kwenye bakuli safi
Wacha viumuke na uchome.
Vitumbua tayari kwa kuliwa