Elections 2010 Vituko vya uchaguzi 2010

Katika kura za maoni za CCM, nec ilimuondoa Bashe hali iliyozua mazungumzo haya:

Swali; Mbona mmemuondoa Bashe kwa kigezo cha kutokua raia wakati uhamiaji wamethibitisha yeye ni raia halali
CCM; Uhamiaji hawana data za ukweli kama sisi na ni wababaishaji
Swali; Wazee wamesema kuwa MKULO si raia halali wa Tanzania, mnalizungumziaje hilo
CCM Hilo si kweli kwani Mkulo ni raia halali wa Tanzania hata uhamiaji wamemthibitisha

Hivyo ndo vituko vya uchaguzi wa mwaka huu na kisha wakampigia magoti ili aokoe jahazi.
 
ATI DR. SLAA HANA MAKAZI YA KUDUMU

Wakuu kuna maneno yanayosemwa kuwa ati Dr. Slaa tangu aachane na upadri ameshindwa kuwa na makazi ya kudumu yaani ameshindwa kujenga nyumba si kijijini kwa baba yake, Karatu Mjini, Dodoma wala Dar.

Kwa mujibu wa wanayoyasema maneno hayo ni kuwa, pengine ni kutokana na utamaduni na imani wanayojengewa watawa na mapadri kuwa huna haja ya kuwa na makazi ya kudumu kwa kuwa binadamu hadumu duniani, ndio maana Dr. ameshindwa kujenga nyumba katika maeneo tajwa hapo juu.

Wasemaji hao wanadai kuwa katika kuthibitisha hoja yao, hata Dr. alipoamua kumchukua Josephine mazima hakumpeleka kwake badala yake alimkodishia appartment kitendo kinachothibitisha kuwa hana makazi yake rasmi.

Wakaenda mbali zaidi na kusema kuwa hata anapokuwa Karatu hufikia katika Hostel zinazomilikiwa na Kanisa mojawapo la mjini Karatu.

Du!!!! Kama ni kweli basi itakuwa ni bonge la soo.
 
Back
Top Bottom