Vituko vya Nahodha

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
MUUWAJI AMETULIA TABATA-ZOMBE UNALETA SIASA NANI ALIMUUA HUU NIUHUNISIDHAN KAMA TUTAWEZA KUVUMILIA
KUWA NA MAWAZIRI WAHUNI KWENYE SERIKALI HIII, KIKWETE WAKATI UNACHAGUA LIST ULIMSHIRIKISHA MIRAJI AMA?

SIDHAN KAMA ULIFIKIIRIA KUWA NA WASAANII KAMA HUU ATI LEO NDIO ANAULIZA AALIEWAUA WAHANGA WA MAHENGE, NENDA MCHUKUE
ZOMBE AKAKUONYESHE HADI SEHEMU WALIPOPIGWA NA AKIKATAA BANENI HIZO PU@# MNAZOBANA WATOTO WA WENZENU KAMA
AJASEMA UKWELI

Nahodha: Polisi wasakeni walioua wachimba madini wa Mahenge

Na Hellen Mwango

13th August 2011

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto), akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Polisi anayeshughulikia masuala ya Fedha na Utawala, Clodwig Mtweve, kufuatilia maafisa 2 wa polisi waliotoroka kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili Abdallah Zombe na wenzake.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwatafuta Koplo Saad na Sajenti Frank, kama Mahakama Kuu Tanzania ilivyoagiza watafutwe waliofanya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu wa Mahenge na dereva mmoja wa teksi.

Kadhalika, Waziri Nahodha ameliagiza jeshi hilo kulishughulikia suala kama askari polisi hao bado wanalipwa mishahara na posho.

Alitoa maagizo hayo baada ya kuhojiwa na NIPASHE kwamba suala la kukamatwa kwa askari polisi hao waliotajwa mahakamani kufanya mauaji hayo limefikia wapi.

Wafanyabiashara hao waliouawa ni Ephrahim Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa tekesi Juma Ndugu.

Mahakama iliwaachia huru askari polisi 12 baada ya ushahidi kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao na sasa rufaa yao inasubiri kusikilizwa.

Pia alihojiwa suala la tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam, (wakati huo), Kamishna Msaidizi Abdallah Zombe, kwamba Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ni kinara wa mtandao wa majambazi wa wizi wa magari nchini.

Alisema alisikia tuhuma hizo dhidi ya Lema ambapo aliliagiza jeshi hilo kupata maelezo ya kina kutoka kwa Zombe ili liweze kufanyiwa kazi.

"Naagiza mlishughulikie hilo suala la hawa askari wawili na kuhusu mishahara yao kama bado wanalipwa pia, nataka kupata taarifa yake haraka iwezekanavyo…mimi sikumbuki vizuri kama mahakama ililiagiza jeshi langu kuwatafuta walioua na kama iliagiza mfanye hivyo" alisema.

Aliongeza: "Kuhusu suala la Lema, Zombe alikuwa ofisa wetu mwandamizi ni kitu gani kilimzuia kutoa taarifa hii wakati akiwa madarakani na leo ni nini kimemsukuma kusema haya… naagiza kwa kuwa ni mwenzetu, tukae naye ili atoe taarifa za kina na tuzifanyie kazi."

Waziri Nahodha alikuwa akizungumzia mafanikio ya miaka 50 ya Jeshi la Polisi tangu kupata Uhuru.

Alisema ili kuhakikisha Jeshi la Polisi, Magereza na Idara ya Uhamiaji vinaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya kazi, anahitaji ushirikiano na jamii.

Alisema ofisi yake iko wazi kupokea taarifa za kuaminika iwapo kuna ofisa wake
yeyote anajihusisha na rushwa atamfuta kazi mara moja.
Alisema akipokea taarifa kwa watu watatu tofauti kuhusu ofisa wake kujihusisha na rushwa, hatasita kumuachisha kazi mara moja.

Akizungumzia miaka 50 ya Uhuru, alisema Jeshi la Polisi limefanya kazi ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao unaimarishwa ikiwemo programu ya miaka 10 ya maboresho ya jeshi kwa kulijengea weledi, mazingira bora ya kazi na kuendeleza dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Hata hivyo, alisema bado kuna malalamiko katika sehemu kuu mbili, ile ya upelelezi wa makosa ya jinai ambayo inachukua muda mrefu jambo linaloathiri uendeshaji wa kesi mahakamani.

Kasoro nyingine aliitaja kuwa ni baadhi ya askari wa jeshi hilo kushindwa kusimamia kikamilifu majukumu yao.

"Nimepokea malalamiko mengi kuhusu kuwepo kwa upendeleo katika kupandisha vyeo, jambo hili lisiposimamiwa vizuri linaweza kuwakatisha tamaa askari wanaostahili lakini hawapandishwi vyeo kutokana na utendaji mzuri wa kazi," alisema.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza alisema lina jukumu la kuwahifadhi na kuwahudumia wafungwa na mahabusu ambapo ili kuwajengea wafungwa uwezo linawapatia mafunzo ya ushonaji wa nguo, utengenezaji sabuni, na uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mkonge.

TATIZO ULE MGAO AKULA ZOMBE PEKEE NDIO MAANA WAMEKAA KIMYA NI ZAIDI YA ZOMBE KAMAA UNATAAKA KUFWATILIA
 
Kuna watu kama iddi simba na wenzake wanakula rushwa live, umsikii hata siku nahodha akitoa tamko lakini unataka
lichunguzwe swala la lema huku chanzo cha habari hiyo ni mtu ambaye ameshapoteza credibility mbele ya jamii kwa uhalifu aliotenda siku za nyuma.
 
Watanzania wenzangu,nawaomba mnikubalie kwamba nchi yetu haina serikali (mawaziri na rais),haina bunge na haina mahakama.Mtu kama zombe kwa nchi zilizo makini asingeachwa huru na huyu m*zimu nahodha hana hadhi ya kuwa waziri kwa nchi ambazo zimejipanga kimaendeleo,suala la askari waliotoroka kuendelea kulipo mshahara kuhojiwa sasa hv baada ya miaka sita ya mauaji ni kithibitisho cha wazi kuwa serikali inafikiria kwa kutumia MAKALIO
 
Kuna watu kama iddi simba na wenzake wanakula rushwa live, umsikii hata siku nahodha akitoa tamko lakini unataka<br />
lichunguzwe swala la lema huku chanzo cha habari hiyo ni mtu ambaye ameshapoteza credibility mbele ya jamii kwa uhalifu aliotenda siku za nyuma.
<br />
<br />

Kuhusu Simba nahisi jamaa anachukua notes sooner or later ataibuka armed with plenty of notes and no evidence to give. Bana hii ndio Tanzania yetu.
 
MUUWAJI AMETULIA TABATA-ZOMBE UNALETA SIASA NANI ALIMUUA HUU NIUHUNISIDHAN KAMA TUTAWEZA KUVUMILIA
KUWA NA MAWAZIRI WAHUNI KWENYE SERIKALI HIII, KIKWETE WAKATI UNACHAGUA LIST ULIMSHIRIKISHA MIRAJI AMA?

SIDHAN KAMA ULIFIKIIRIA KUWA NA WASAANII KAMA HUU ATI LEO NDIO ANAULIZA AALIEWAUA WAHANGA WA MAHENGE, NENDA MCHUKUE
ZOMBE AKAKUONYESHE HADI SEHEMU WALIPOPIGWA NA AKIKATAA BANENI HIZO PU@# MNAZOBANA WATOTO WA WENZENU KAMA
AJASEMA UKWELI

Nahodha: Polisi wasakeni walioua wachimba madini wa Mahenge

Na Hellen Mwango

13th August 2011

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha (kushoto), akitoa maelekezo kwa Kamishna wa Polisi anayeshughulikia masuala ya Fedha na Utawala, Clodwig Mtweve, kufuatilia maafisa 2 wa polisi waliotoroka kwenye kesi iliyokuwa ikimkabili Abdallah Zombe na wenzake.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwatafuta Koplo Saad na Sajenti Frank, kama Mahakama Kuu Tanzania ilivyoagiza watafutwe waliofanya mauaji ya wafanyabiashara wa madini watatu wa Mahenge na dereva mmoja wa teksi.

Kadhalika, Waziri Nahodha ameliagiza jeshi hilo kulishughulikia suala kama askari polisi hao bado wanalipwa mishahara na posho.

Alitoa maagizo hayo baada ya kuhojiwa na NIPASHE kwamba suala la kukamatwa kwa askari polisi hao waliotajwa mahakamani kufanya mauaji hayo limefikia wapi.

Wafanyabiashara hao waliouawa ni Ephrahim Chigumbi, Sabinus Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa tekesi Juma Ndugu.

Mahakama iliwaachia huru askari polisi 12 baada ya ushahidi kushindwa kuthibitisha makosa dhidi yao na sasa rufaa yao inasubiri kusikilizwa.

Pia alihojiwa suala la tuhuma zilizotolewa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Dar es Salaam, (wakati huo), Kamishna Msaidizi Abdallah Zombe, kwamba Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ni kinara wa mtandao wa majambazi wa wizi wa magari nchini.

Alisema alisikia tuhuma hizo dhidi ya Lema ambapo aliliagiza jeshi hilo kupata maelezo ya kina kutoka kwa Zombe ili liweze kufanyiwa kazi.

“Naagiza mlishughulikie hilo suala la hawa askari wawili na kuhusu mishahara yao kama bado wanalipwa pia, nataka kupata taarifa yake haraka iwezekanavyo…mimi sikumbuki vizuri kama mahakama ililiagiza jeshi langu kuwatafuta walioua na kama iliagiza mfanye hivyo” alisema.

Aliongeza: "Kuhusu suala la Lema, Zombe alikuwa ofisa wetu mwandamizi ni kitu gani kilimzuia kutoa taarifa hii wakati akiwa madarakani na leo ni nini kimemsukuma kusema haya… naagiza kwa kuwa ni mwenzetu, tukae naye ili atoe taarifa za kina na tuzifanyie kazi.”

Waziri Nahodha alikuwa akizungumzia mafanikio ya miaka 50 ya Jeshi la Polisi tangu kupata Uhuru.

Alisema ili kuhakikisha Jeshi la Polisi, Magereza na Idara ya Uhamiaji vinaendelea kufanya kazi kwa mujibu wa maadili ya kazi, anahitaji ushirikiano na jamii.

Alisema ofisi yake iko wazi kupokea taarifa za kuaminika iwapo kuna ofisa wake
yeyote anajihusisha na rushwa atamfuta kazi mara moja.
Alisema akipokea taarifa kwa watu watatu tofauti kuhusu ofisa wake kujihusisha na rushwa, hatasita kumuachisha kazi mara moja.

Akizungumzia miaka 50 ya Uhuru, alisema Jeshi la Polisi limefanya kazi ya kuimarisha usalama wa raia na mali zao unaimarishwa ikiwemo programu ya miaka 10 ya maboresho ya jeshi kwa kulijengea weledi, mazingira bora ya kazi na kuendeleza dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Hata hivyo, alisema bado kuna malalamiko katika sehemu kuu mbili, ile ya upelelezi wa makosa ya jinai ambayo inachukua muda mrefu jambo linaloathiri uendeshaji wa kesi mahakamani.

Kasoro nyingine aliitaja kuwa ni baadhi ya askari wa jeshi hilo kushindwa kusimamia kikamilifu majukumu yao.

“Nimepokea malalamiko mengi kuhusu kuwepo kwa upendeleo katika kupandisha vyeo, jambo hili lisiposimamiwa vizuri linaweza kuwakatisha tamaa askari wanaostahili lakini hawapandishwi vyeo kutokana na utendaji mzuri wa kazi,” alisema.

Kwa upande wa Jeshi la Magereza alisema lina jukumu la kuwahifadhi na kuwahudumia wafungwa na mahabusu ambapo ili kuwajengea wafungwa uwezo linawapatia mafunzo ya ushonaji wa nguo, utengenezaji sabuni, na uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na mkonge.

TATIZO ULE MGAO AKULA ZOMBE PEKEE NDIO MAANA WAMEKAA KIMYA NI ZAIDI YA ZOMBE KAMAA UNATAAKA KUFWATILIA
Jamani hawa jamaa vipi? mpaka chadema ipige kelele ndiyo wanashituka! kesi imeisha karibia mwaka wa pili cha ajabu leo ndiyo waziri anatoa tamko la kukamatwa wahalifu kweli hii nchi ya mazonge.
AKILI YA KUAZIMA CHANGANYA NA ZA KWAKO
 
Hivi bado anaendelea kuishi New Africa hotel?..maana alikataa nyumba aliyopewa mwanzoni akidai haina hadhi ya 'waziri kiongozi'.
Huyu anatia mashaka maana issue sensitive kama mauaji ya raia anaoneka hana habari nazo kabisaa..
Ama kweli bongo inachosha ukiifikiria
 
huyu alipewa cheo ili kumpoza baada ya zanzibar kubadilisha katiba na kufuta cheo cha waziri kiongozi,.alipewa ubunge wa kuteuliwa,..m.k.were alitaka kumpa na meghji uwaziri lakini watu wakachonga akamtosa but iam sure atampa uwaziri uko mbele ya safari..wazanzibar wengi hawana asili ya kupenda makuu lakini huyu nahodha wa nchi kavu ananishangaza kukataa nyumba,..nina shaka na swaumu yake kama amefunga..pepo ngumu sheikh
 
mauaji yanafanyika miaka kama 6 iliyopita, watu wanaachiwa katika mazingira ya utatanishi hata baada ya ripoti ya madaktari kuthibitisha kuwa walipingwa risasi kutokea nyuma tena kwa pamoja! bado ushahidi haukutosha. Leo unaagiza maaskari kama wanalipwa mshahara au na watafutwe wakamatwe! nchi inaongozwa na watu wasio makini bado unaona tuna serikali hapo? kiini macho na ni aibu hata kujivunia miaka 50 ya jeshi la polisi ambalo limeshindwa kukamata wezi na likiwa viongozi wake waandamizi wakiwa vinara wa uhalifu akiwemo Zombe.
 
Maswali ninayojiuliza ni kwamba, kesi zote zinazohusu wakubwa ambazo ofisi ya DCI imeziendesha, ni kesi ngapi imeshinda? Ukiacha kesi ya Liumba, ni wangapi wamefungwa gerezani? Competent ya wanasheria wake ikoje?
Majibu ya haya maswali yatatusaidia kutoa +ve comment.
 
Ni lini Mheshimiwa Naodha atalitaka Jeshi la Polisi kufuatilia wezi wa Kagoda, meremeta, etc?
 
Pelekeni ushahidi kwa DPP ili kufunguliwe kasi sio kulalama

Ushahidi upi wakati anao? Kila mtu ana mtazamo wake katika masuala mazito na sidhani kama
wananchi wanapoamua kusema basi watakuwa wanalalamika. Mbona mkuu wa nchi analalamika
kila mara lakini hatusikii mkimsema? Nchi hii tunapenda kuishi kinafiki, kutenda tusichosema na
kusema tusichotenda!
 
Back
Top Bottom